Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Viongozi wa Upinzani tulikaa pamoja tukakubaliana kwa Upande wa Urais asimame Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Viongozi wa Upinzani tulikaa pamoja tukakubaliana kwa Upande wa Urais asimame Tundu Lissu

Suala la kujitoa nilishalifikiria lakini kwa sasa naona halitasaidia sana kwa sababu ile ile kwamba, kuna uwezekano mkubwa NEC wameshapa makaratasi, na hata kama zoezi halijakamilika, watasema tu wameshachapa ili mradi tu Membe asiondolewe kwenye karatasi za kupigia kura!

Lakini kwa upande mwingine, ma-CCM hayaaminiki haya kwahiyo inaweza kuwa risk kujitoa moja kwa moja!!! Nasema hayaaminiki kwa sababu Lissu akiyabana kisawasawa kiasi cha kukosa pumzi, wala hayaoni aibu haya kutumia kila hila kama ile ya kumsimamisha kufanya kampeni na hata kusema amekiuka hili na lile na hivyo anaondolewa!!

So, huku Membe kajitoa, TL anapigwa zengwe la kufa mtu... what next?! Kama ma-CCM yaliweza kufuta uchaguzi kule ZNZ baada ya kuona yamebanwa hata kupumua hayawezi unadhani yanaweza kushindwa kumpiga ban mgombea?!
Hivyo unadhani Lisu akipigwa ban na mi ccm, Membe anaweza kuwa mbadala?!

Membe sidhani kama anaweza kumreplace Lisu, nakuhakikishia wakimpiga Lisu ban watu hawatapiga kura kabisa.
 
Aondoe jina kwenye karatasi za kupiga kura, ili wasituibie kura za Lisu kumpa Membe, ili ionekane kashindwa na membe!
Mbinu hizi sijui kama mnazielewa, utashangaa Membe ana 10% halafu Lisu 6% , Magufuli 80% na mtaambiwa membe alikuwa anakubalika zaidi.
Ha ha ha.. saivi wizi wa maccm hautakuwa rahisi Kama miaka ya nyuma
 
Zitto anajua Lissu ataambulia patupu!!! Anachofanya...ni kumpa coverage ya kutosha Lissu, ili mwisho wa siku Lissu apoke uenyekiti Mbowe na Lissu awe mwenhekiti wa chama. Kisha baadaye Lissu aungane na Zitto ku- merge Chadema na ACT!! Na wakishafanya hivyo, Zitto ataaanda mpango kamambe wa kukipoka Chama hicho na yeye sasa kuwa Mkuu wa mambo yote, na ataanza kuwadhiaki wote bila kijali juhudi zao za siasa kwenye mipango hiyo!!! Kwa maneno mengine Zitto anataka kurudi Chadema kwa njia nyingine!!!!

Msitoe macho...! Mnashangaaa nini!? Kwani hamumjui Zitto Ha ha haaa!!!! Watani wamechanganyikiwa ....ha haha ahaaa! ( Yote hayo nawaza kipindi hiki...!)

Ndiyo mambo ya siasa hayo ( Je. Hapa nchini ama nchi nyingine Conspiracy theories ni kosa la jinai!?)
Ramli?
 
Watumishi wote kura kwa lissu.

Mmeteswa sana miaka 5 bila kupata stahiki zenu!!
 
Kitu Magufuli anasahau au anafanya kusudi ni kwamba;Watanzania hawataki kubaguana kwa kutumia
Kabila
Dini
Ukanda
Uvyama
Sasa ninachokiona kwa kiongozi huyu anajitahidi kutugawa kwa kutumia vyama. Naona upinzani unatumia nafasi hiyo kutuunganisha,
Ninavyo ona mimi kwa Tanzania kutugombanisha kwakutumia vyama imegonga mwamba, labda polisi wabariki hili lakini najiuliza na nimekosa majibu nikuulize mgombea wa Polepole iwapo utabahatika kuwapata washindi wote watokane na chama chako lengolako nini?hapo baadae!
Kinachomsumbua magu si kabila yake,wala roho mbaya wala background yake isipokuwa ni uwezo wake mdogo
 
Hizo nchi ulizozitaja sasa niishie hapo
Hamuambiwi ukweli kuhusu majimbo uishiehapo kwamba hawatumii majimbo au?kama niswala lajimbo hilikuendelea kulikolingine jekwani hivisasa mikoa inalingana kimaendeleo? Swala ilitakiwa wamuulize namna atakavyo yaendesha majimbo siokubisha bisha tu toka uhuru maji maji mmeshindwa ondokeni
 
Sawa kabisa. Lakini wamechelewa sana. Kwenye uraisi kuna kura zitapotea sana kwenda kwa Membe sababu jina litakuwepo.
Wamechelewa sana hawa kuungana.

Membe hata angembea bado angepata kura chache sana za wapinzani, sana sana anaweza kugawa za wanaccm maana ndio amekaa huku toka ujanani hadi uzeeni.
 
Kiongozi wa cha chama cha ACT-Wazalendo taifa Zitto Kabwe amesema endapo wananchi wa mkoa wa Katavi watawachagua viongozi wa upinzani watahakikisha wanaletea mabadiliko katiko sekta ya afya, maji na elimu.

Ameyasema hayo alipokua akizungumza na wananchi wa manispaa ya Mpanda katika uwanja wa Sikonge na kusema kuwa a endapo watapata ridhaa upinzani watahakikisha wanatatua kero za wakulima sambamba na kuboresha maisha ya watanzania.

Aidha amewaomba wananchi wa jimbo la Mpanda mjini kumchagua mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Rhoda Kunchela na kusema kuwa wao kama vyama upinzani wameona ni vyema kusimamisha wagombea wanaoweza kumshinda mgombea wa CCM.

Akizungumzia nafasi ya urais kiongozi huyo amesema viongozi wa upinzani wamekaa kwa pamoja na kuona ni vyema kumsimamisha mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Tundu Lissu.

Chanzo: Mpanda Radio
TL anatosha. Tuliwapiga chenga wale wahuni wa satan campany.
 
Hivyo unadhani Lisu akipigwa ban na mi ccm, Membe anaweza kuwa mbadala?!

Membe sidhani kama anaweza kumreplace Lisu, nakuhakikishia wakimpiga Lisu ban watu hawatapiga kura kabisa.
Issue sio kuweza kum-replace bali HAKUTAKUWA na choice nyingine! Choice pekee inaweza kuwa watu kuingia barabarani na kuwa tayari kwa lolotei!

Katika hilo, Watanzania usiwategemee!!

Watu wasipopiga kura, hiyo wala haitawasumbua CCM kwa sababu hawana aibu ya kuendesha uchaguzi wa upande mmoja! Tumeshahudia mambo sawa na hayo kule Zanzibar mara mbili, na mwaka jana kwenye uchaguzi wa serikali za mita!

Je, umeona CCM na serikali yake wakilionea aibu suala hilo kiasi cha kubadilika?!
 
Atakae mpigia Membe ni nani na wanachama wa AcT washaambiwa wampigie Lissu?
Labda zihesabike kwake kwa kuiba ili kupunguza za Lissu but vinginevyo sidhani kama atapata kura hata laki moja
Umeshapatikana mwanya wa bao la mkono
 
Umeshapatikana mwanya wa bao la mkono
Mkuu bao la mkono linazidi kupotezewa nafasi, wanaumia kichwa hawajui itakuwaje. Mapumziko ya gafra ili kuangalia namna bora yakuliwezesha, ila awamu hii mambo ni tofauti kabisaa
Magwiji wa mambo hayo walitengwa nao wamejitenga na kususia😂😂
 
Mkuu bao la mkono linazidi kupotezewa nafasi, wanaumia kichwa hawajui itakuwaje. Mapumziko ya gafra ili kuangalia namna bora yakuliwezesha, ila awamu hii mambo ni tofauti kabisaa
Magwiji wa mambo hayo walitengwa nao wamejitenga na kususia😂😂
Kama jina na sura ya Membe yatakuwepo kwenye karatasi ni kuhesabu maumivu
 
Back
Top Bottom