Zitto Kabwe: Vitabu nilivyosoma Mwaka 2022

Zitto Kabwe: Vitabu nilivyosoma Mwaka 2022

Huyo jamaa sikuhizi kahamia ACT ndiyo maana amekuwa na tabia za kinyonga
Ndio mjifunze kujua dhamira za hao jamaa pale mnapodhani wako upande wenu, huwa wanafanya hivyo endapo tu ndani ya jumba jeupe hatakuwepo "mwenzao" hapo watajidai wanajua kukosoa haswa...

Lakini siku ubao ukibadilika, ndani ya jumba jeupe akaingia "mwenzao" hapo ndipo unafiki wao unapodhihirika, kwa kufumbia macho ujinga wowote toka kwa "mwenzao" au marafiki zake wa karibu.

Hao ni wakuogopa kama ukoma.
 
Hakika elimu haina mwisho na sasa tumepata somo kubwa sana.
 
Dear comrades tunasahau kitu.
Hekima ya mtu ni kukosoa na kusema sifa za mtu. Huo ndio utimilifu ulio mkubwa.
Naamini yeye kueweka hili andiko ni kuleta inspiration ya usomaji vitabu katika jamii yetu. Hayo ya yeye namna gani ana-apply au kubadilishwa na vitabu ni mjadala mwingine.
Binafsio sio shabiki yako, lakini nikupe hongera sana kwa usomaji huu wa vitabu uliotukuka mtani.
 
Yuaja kiongozi ambaye hatatambua MIKOPO mnayokimbizana kutukopea bila ridhaa yetu.

Mtailipa MIKOPO hiyo ninyi na familia zenu Kwa njia zote, mliohusika kokopa na kuziiba pesa hizo kupitia matumizi mabaya ktk miradi mbalimbali.

Ni Hadi kizazi Cha nnne, mtailipa mkiwa jela, mtailipa Kwa magonjwa ya Kila aina yatakayowafuata Hadi kizazi Cha nne. Mapooza hayatakoma ktk vizazi vyenu.
 
Unapoteza muda kusoma mavitabu yasiyo kuwa na maana yoyote kwa wana Kigoma,rudi kigoma kaimarishe fikra za ndugu zako.

Nakuona sasa unajifanya mzanzibari rudi kwenu achana na uzanzibari haukusaidii chochote kwa wanaKigoma
 
Mwaka huu unaomalizika 2022 nimebahatika kusoma vitabu mbalimbali 33 (2021:29, 2020:16, 2019:34). Ulikuwa mwaka mzuri kwa usomaji vitabu na pia mwaka ambao nilibahatika kupata zawadi nyingi za vitabu kutoka kwa marafiki zangu na ndugu zangu.

Nitaanza mwaka 2023, Mungu akijaalia kuvuka salama, nikiwa na karibu dazeni ya vitabu ambavyo sijasoma. Kama nilivyofanya mwaka jana, kutokka orodha ya mwaka huu nimeshatoa orodha ya vitabu 10 ninavyopendekeza watu kuvisoma mwaka ujao kama hawajavisoma.

Vitabu nilivyosoma mwaka huu kwa makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo;

Riwaya
  • Magic of Saida – MG Vassanji
  • I am Semba – Ajeka&Fox
  • The Book of Secrets – MG Vassanji
  • The House of Rust – Khadija Abdallah Bajaber
  • Mtumwa kwenye Nchi Huru – Elizabeth Mramba
  • A Line In The River: Khartoum City of Memory – Jamal Mahjoub
  • We are all Birds of Uganda – Hafsa Zayyan
  • The In-Between World of Vikram Lall – MG Vassanji
  • Next In Line – Jeffrey Archer
  • Tea with Ms. Tanzania – Fayyaz Vellani
  • The Shadow King – Maaza Mengiste
Wasifu/Tawasifu
  • The Chancellor: The Remarkable Odyssey of Angela Merkel – Kati Marton
  • Njinga of Angola: Africa’s Warrior Queen – Linda M. Heywood
  • The Prime Ministers We Never Had: Success and Failure from Butler to Corbyn – Steve Richards
  • 38 Reflections on Mwalimu Nyerere – Ed. Mark Mwandosya and Juma V Mwapachu
  • Hani: A life too short – Janet Smith and Beauregard Tromp
  • Juhudi na Changamoto – Sheikh Ponda Issa Ponda
  • The Bhutto Dynasty: The Struggle for Power in Pakistan – Owen Bennett-Jones
  • Maisha Yangu – Khamis Abdallah Ameir
  • Revolution in Zanzibar: An American’s Cold War Tale – Don Petterson
  • The Tanganyika Way: A personal Story of Tanganyika’s Growth to Independence – Sophia Mustafa
Nchi ya mwaka, India
  • Indian Summer: The Secret History of the End of an Empire – Alex Von Tunzelm
  • Pride, Prejudice and Punditry: The Essential – Shashi Tharoor
  • Mamata Beyond 2021 – Jayanta Ghosal
  • The Rise of The BJP: The Making of the World’s Largest Political Party – Bhupender Yadav and Ila Patnak
  • India in a New Key: Nehru to Modi, 75 years of freedom and democracy – Narain D. Batra
Mchanganyiko
  • Time for Socialism – Thomas Piketty
  • Capturing Hope: The Struggle Continues for a New Malaysia – Mahathir Mohamed
  • Final Reckoning: An Insider’s View of the Fall of Malaysia’s Barisan Nasional Government – Romen Bose
  • The World for Sale: Money, Power and the Traders Who Barter the Earth’s Resources – Javier Blas and Jack Farchy
  • Sudan’s Unfinished Democracy: The Promise and Betrayal of a People Revolution – Willow Berridge, Justin Lynch, Raga Makawi and Alex De Waal
  • From Rebel to Ruler: One Hundred Years of the Chinese Communist Party – Tony Saich
  • Borderland: A Journey Through the History of Ukraine – Anna Reid
Heri ya mwaka mpya 2023

23/12/2022

ILANI: Kila mwaka, nikibahatika na kujaaliwa, huwa ninasafiri pamoja na familia yangu. Kwa muda sasa nchi ninayotembelea huchomoza kupitia vitabu nilivyosoma mwaka huo. Mwaka huu nimeamua kuweka kundi la Nchi ya Mwaka ili kuonyesha vitabu nilivyosoma kuhusu nchi husika. Mwaka 2022 ilikuwa India (Rwanda 2021).
Hongera sana Ndugu. Bila shaka umepata maarifa mengi.
 
Yuaja kiongozi ambaye hatatambua MIKOPO mnayokimbizana kutukopea bila ridhaa yetu.

Mtailipa MIKOPO hiyo ninyi na familia zenu Kwa njia zote, mliohusika kokopa na kuziiba pesa hizo kupitia matumizi mabaya ktk miradi mbalimbali.

Ni Hadi kizazi Cha nnne, mtailipa mkiwa jela, mtailipa Kwa magonjwa ya Kila aina yatakayowafuata Hadi kizazi Cha nne. Mapooza hayatakoma ktk vizazi vyenu.
Inapo mature wanailipa moja kwa moja na hawaniulizi mimi au wewe. Uwepo wetu hauna uhusiano wa moja kwa moja na wao kukopa au kulipa.

Wewe ukisusa hao milioni 61 na ushee wanaobakia wanalipa na serikali inarudisha hiyo mikopo na maisha yanaendelea kama vile mimi na wewe hatupo duniani.
 
Ni
Una muda wa kuchezea wewe yaani pamoja na vitabu hivyo bado unaendelea kununuliwa na kufanya udalali wa kisiasa bado una unafiki wa kumchukia Magufuli huku ukiungana na genge la wafuja Mali akina Malope ndio unatuambia vitabu vinaandika hayo kutwa unadhurula ulaya kwa wakoloni wetu wezi wa Mali zetu kuihujumu nchi ona Sasa tunauzia majrnereta na imeme unakatwa hovyo yaani uzungu mwingi umekupoteza kisiasa
afadhali asome novel za James Hadley Chase zinafurahisha sana na zinakufanya unakuwa mjanja 😂😂😅
 
Mkuu mleta mada mwenyewe hajavielezea hivyo vitabu yeye kataka tu tujue amesoma vitabu vingapi na kuweka majina ya hivyo vitabu, alichokifanya yeye ni show off tu ila wewe unataka sisi ndio tujadili maudhui ya vitabu.

Hata sisi tunasoma vitabu pia ila yeye Zitto kataka kuonyesha wingi wa vitabu anavyosoma kwa mwaka.
Kiukweli sijaelewa hoja yako, "...kataka kuonyesha wingi wa vitabu.."!, Kwa hiyo angefanyaje?
Huu uzi dhima yake ndiyo hiyo, kutuonyesha idadi ya vitabu ulivyosoma.

Hii ni thread ya vitabu, hoja ni vitabu. Kwa nini mnabadili na kufanya hoja iwe ni Zitto?
Ungetaja mapungufu ya vitabu alivyoleta ningeelewa.
 
Mimi mtakwimu ungeniwekea ktk mabano pages za kila kitabu ningefahamu kwa siku ulisoma wastani wa kurasa ngapi.

Ukifika wkt tutafahamu ukweri wa jambo hili - hongera sana lkn
 
Kiukweli sijaelewa hoja yako, "...kataka kuonyesha wingi wa vitabu.."!, Kwa hiyo angefanyaje?
Huu uzi dhima yake ndiyo hiyo, kutuonyesha idadi ya vitabu ulivyosoma.

Hii ni thread ya vitabu, hoja ni vitabu. Kwa nini mnabadili na kufanya hoja iwe ni Zitto?
Ungetaja mapungufu ya vitabu alivyoleta ningeelewa.
Zitto mwenyewe kaweka majina ya hivyo vitabu kisha hakutaka kujadili kuhusu hivyo vitabu.
 
Zitto mwenyewe kaweka majina ya hivyo vitabu kisha hakutaka kujadili kuhusu hivyo vitabu.
Ameona watu hamna interest na vitabu ila mna interest na yeye binafsi..

Unajua maana yake? That proves he is a successful Politician!
 
Ameona watu hamna interest na vitabu ila mna interest na yeye binafsi..

Unajua maana yake? That proves he is a successful Politician!
Watu wamehoji maarifa anayopata kwenye usomaji wa vitabu, nachojua lengo kuu ni kuhamasishana kusoma vitabu ili kuongeza maarifa hivyo kwa nafasi yake Zitto ilikuwa vyema kama angetolea maelezo kuliko kuishia kutaja majina ya vitabu tu na kutokomea hadi anatia mashaka kama amesoma kweli hivyo vitabu vyote.

Angejibu maswali ambayo anaona yanafaa kuyajibu na kuacha asiyotaka lakini sio kukimbia.
 
Watu wamehoji maarifa anayopata kwenye usomaji wa vitabu, nachojua lengo kuu ni kuhamasishana kusoma vitabu ili kuongeza maarifa hivyo kwa nafasi yake Zitto ilikuwa vyema kama angetolea maelezo kuliko kuishia kutaja majina ya vitabu tu na kutokomea hadi anatimia mashaka kama kweli amesoma kweli hivyo vitabu vyote.

Angejibu maswali ambayo anaona yanafaa kuyajibu na kuacha asiyotaka lakini sio kukimbia.
May be you have a point!
 
Dah kweli ZZK watu wamemhara! 😁
Zitto wa mwaka 2014 kushuka chini angeshatukusanya hapa.
 
Huyu jamaa ameishia kutuletea habari hizi.
Sio Yule Tena wa kupigania maslahi ya watanzania.
Kina kipara wamemmaliza kabisa
Lao moja tu kwa Sasa.
 
Back
Top Bottom