Zitto Kabwe: Wahariri waulizeni CHADEMA wana mikakati gani ya kumtoa Mbowe jela

Hichi kiloandikaa hapa hakina uhusiano na aliyoyasema Zitto leo kwenye kikao na wahariri. SIJUI KWA NINI MWANDISHI KAAMUA KUANDIKA ambayo hayakusemwa.
Kuhubiri haki na kusimamia haki ni vitu TAFAUTI sanaaa
 
Zitto ni mnafiki sana.

Ni ngumu kumuelewa wenzake wanapigania Katiba Mpya yeye analeta vitu visivyoeleweka kwenye vyombo vya habari ili kutuliza upepo,nakumbuka hata wakati joto la Uchaguzi mdogo kule Arumeru limepanda yeye ndiyo alikuja na Agenda ya yeye kugombea Urais watu basi tu kuharibu upepo,ni ngumu kumuelewa huyu mtu.

Anachotafuta Mbowe aombe Msamaha apate umaarufu kuwa yeye ndiyo alimtoa baada ya kumuombea Msamaha,vipi msamaha ukikataliwa?
Na ukiomba Msamaha maana yake si umekubali kosa?Itakuwa na Madhara gani kisiasa kwa Mbowe na chama chake Zitto haoni hilo?

Ndiyo maana wengi wanasema anatumika.
 
Njia pekee ya kuisafisha Serikali na wakubwa wake kwenye hii kesi ya Mbowe ni kufanikisha jitihada za Mbowe kuomba msamaha.. Nje ya hapo, ikitokea kesi ikafika mwisho, Mbowe atakuwa maarufu zaidi ya Serikali. Na hakuna anaetaka hilo litokee, lkn pia hawana ushahidi wa kumtia hatiani. Hivyo msamaha inabakia ndo njia pekee salama. Zitto anacheza ngoma anayoijua. Katumwa.
 
Hao mawakili wanaomtetea mbwe nani anawalipa.
 
Zitto aisee kama issue ni kumuombea msamaha Mbowe ili aweze kutoka sio sahihi mbona kuna wafungwa wengi tu wa makosa ya ugaidi wako jela kwanini hatuwaombei msamaha kwenye mamlaka husika ili wasamehewe wakaungane na familia zao.Kama ana hatia wacha ahukumiwe then akitumikia kifungo Rais akiona kuna umuhimu wa kumsamehe atamsamehe kusiwe na double standard wote ni watanzania tuna haki sawa.kuna magaidi wako gereza la kisongo huu mwaka wa 10 kama sikosei anza na hao kiongozi mkuu kuwaombea msamaha ili waungane na familia zao au hao sio kaka zako kama Mbowe.Acha siasa mkuu.
 
Zitto ni mnafiki na shetani mkubwa, CHADEMA wanazo mpaka taarifa za Zitto akichonga na maafisa wa serikali kuhakisha kesi inayomkabili Mbowe iishie kwa Mbowe kufungwa kimahakama.


Hizi ni tuhuma kubwa na nzito sana, hebu tuwekee Ushahidi hapa.
 


Hakuna Ushahidi kwamba Zitto alimuombea Mbowe msamaha kwa Rais Samia, hotuba ya Zitto mbele ya Samia ipo.
 
Zito ni muoga tangia chadema ndo maana hukuwah kumuona akikaa lockup alizidiwa hd na wale mabinti waliopo bungeni sasa ambacho hakijui ni kwamba Mbowe hana cha kupoteza walishamuharibia vitega uchumi bado yupo imara na hatawapigia magoti
 
Kuna jambo moja nina uhakika nalo..wengi wanamzungumzia ZZK kiushabiki....Zitto anajua kijacho! Anajaribu kunusuru jahazi..unfortunately hapewi support! Muda ni daktari mzuri sana!
Jahazi kuzama si jambo la ajabu kwani kuna kiwango cha judiciary kuwa compromised.LAKINI ikiwa kweli Mbowe alifanya ugaidi ni halali yake kufungwa.
Hivi kweli Zitto anaweza kuwaombea msamaha magaidi halisi waliopo rumande?
 
Mimi sijawahi muamini ZZK. Toka tupo kwenye viunga vya Galanos,yeye mbele mimi nyuma na badae UDSM mpaka Ubunge wake huko Kigoma,mpaka leo na hata milele.
 
Kwani Rais anaruhusiwa kuingilia uhuru wa mahakama? Au hao chadema wana ruhusa ya kuingilia uhuru wa mahakama?

Labda kuna ambalo hatulifahamu na ingekua vizuri kama bwana Zitto angetufahamisha
Hii ni hoja muafaka.
Mawakili Wasomi tusaideni tafadhali.
Kesi ya Jinai inapokuwa inaendelea Mahakamani, kabla ya hukumu, mtuhumiwa anaombewaje msamaha kwa Rais?
Au Zitto Zuberi Kabwe anaongelea kuomba msamaha kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu, DPP?
Au anapendekeza kuendelea kuvunja Katiba ya Nchi kwa Rais kuingilia mamlaka ya DPP?
Naomba ufafanuzi wa Wataalam wa Sheria humu JF.
Au Zitto Zuberi Kabwe hajui alinenalo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…