Point, sasa hao nyumbu wa NRNE wacha wahangaike na upumbavu waoKiongozi Mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe, ameendelea kutoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025 ili kurejesha nguvu ya wananchi bungeni, akisema kutoshiriki uchaguzi ni sawa na kukubali kuendelea kuwepo kwa Bunge kibogoyo lisilo na uwezo wa kuisimamia Serikali.
Akihutubia siku ya Jumatatu Julai 7, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Songea, mkoani Ruvuma, katika mwendelezo wa Operesheni Majimaji ya chama hicho, Zitto amesema sheria kama ile ya Usalama wa Taifa ziliweza kupitishwa kwa sababu ya ukosefu wa wabunge waliokomaa kimtazamo na kisheria.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika hotuba yake, Zitto amegusia pia ongezeko la vitendo vya utekaji vinavyodaiwa kufanyika sehemu mbalimbali nchini huku akilitaja tukio la kutekwa kwa Mdude Nyagali na wengine kama ushahidi wa hali mbaya ya usalama na haki za binadamu.
Amewatahadharisha wananchi dhidi ya wito wa kutoshiriki uchaguzi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wanaodaiwa kukata tamaa ya mabadiliko, akisema wito huo ni hatari na una manufaa kwa CCM pekee.
OKTOBA TUNATIKI
OKTOBA TUNATIKI
sijamuelewa huyo zito kabwe, anatofautisha vp usalama wa taifa na polisi? kwani polisi kuna ambao hawavai magwanda pia na wanaofanya kazi za uchunguzi wanaweza kukivamia muda wowote na kukushika bila sare kama wanakuhitaji isitoshe wote bosi wao ni mmoja waziri wa mambo ya ndani hivyo sidhani kama ni sahihi kusema kwamba usalama wa taifa hawaruhusiwi kukamata kwani polisi pia kuna watu wa usalama ambao hawavai magwanda
Ni kweli hujamuelewa. Anasema hivi; sheria ilikuwa haiwaruhusu TISS kukukamata wewe. Polisi wasiokuwa na magwanda watakukamata wewe kwa kujitambulisha kwa majina yao, kituo chao cha kazi, kukuonyesha kitambulisho cha kazi, watakwambia kosa lako, Kisha wanakukamata.sijamuelewa huyo zito kabwe, anatofautisha vp usalama wa taifa na polisi? kwani polisi kuna ambao hawavai magwanda pia na wanaofanya kazi za uchunguzi wanaweza kukivamia muda wowote na kukushika bila sare kama wanakuhitaji isitoshe wote bosi wao ni mmoja waziri wa mambo ya ndani hivyo sidhani kama ni sahihi kusema kwamba usalama wa taifa hawaruhusiwi kukamata kwani polisi pia kuna watu wa usalama ambao hawavai magwanda …
Haahaa zitto aweke akiba ya maneno, baada ya uchaguzi hatutaki kusikia ameibiwa kura Wala kura feki..Kiongozi Mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe, ameendelea kutoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025 ili kurejesha nguvu ya wananchi bungeni, akisema kutoshiriki uchaguzi ni sawa na kukubali kuendelea kuwepo kwa Bunge kibogoyo lisilo na uwezo wa kuisimamia Serikali.
Akihutubia siku ya Jumatatu Julai 7, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Songea, mkoani Ruvuma, katika mwendelezo wa Operesheni Majimaji ya chama hicho, Zitto amesema sheria kama ile ya Usalama wa Taifa ziliweza kupitishwa kwa sababu ya ukosefu wa wabunge waliokomaa kimtazamo na kisheria.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika hotuba yake, Zitto amegusia pia ongezeko la vitendo vya utekaji vinavyodaiwa kufanyika sehemu mbalimbali nchini huku akilitaja tukio la kutekwa kwa Mdude Nyagali na wengine kama ushahidi wa hali mbaya ya usalama na haki za binadamu.
Amewatahadharisha wananchi dhidi ya wito wa kutoshiriki uchaguzi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wanaodaiwa kukata tamaa ya mabadiliko, akisema wito huo ni hatari na una manufaa kwa CCM pekee.
Ni kweli hujamuelewa. Anasema hivi; sheria ilikuwa haiwaruhusu TISS kukukamata wewe. Polisi wasiokuwa na magwanda watakukamata wewe kwa kujitambulisha kwa majina yao, kituo chao cha kazi, kukuonyesha kitambulisho cha kazi, watakwambia kosa lako, Kisha wanakukamata.