GE2025 Zitto Kabwe: Wasioshiriki uchaguzi watajutia uamuzi wao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wanajua ila nikatika namna yakukumbushana,Ni kama wale wanaowaambia kua bila reform hakuna uchaguzi,unafikiri wanaowaambia wanakua hawajui hayo?.Hakuna kigeni ila lazima watu waambiane katika namna nzuri.Na katika hili zitto yuko sahihi kwasababu mifano ya chaguzi zinazotolewa mifano ziliharibiwa na magufuli ambaye kwasasa hayupo na aliyepo sasa sioni akiwa na nia yakuingilia mchakato kwa kiwango kile.
Je uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji 2024 ulikuwaje???Je magufuri alikuwepo?
 
Zitto ameshakuwa irrelevant kwasasa. Hana hoja za msingi anaishi kwa umashuhuri wa jina lake ila matendo yake kwasasa yanatia sana mashaka juu ya uwepo wake katika siasa ni kwa maslahi ya nani nje ya masilahi yake binafsi.

Zitto sio mtu mzuri tena.
Zito sio kiongozi wa chama cha ACT tena, ila kiuhalisia ndio kiongozi hadi sasa, kwani ndio mwenye air time kubwa hata kwenye mikutano yao. Na sehemu kubwa nimemfuatilia Zito, ni mtu anayekwazika iwapo cdm itaingia madarakani, kuliko ccm kuendelea kuwa madarakani. Na hata siasa zake ni zile zinazokubaliwa na ccm.
 
Anapewa ubunge kigoma pekee na wazanzibar wanapata ubungr kina jusa
Nakwambia hawezi,Kamanda Siro kapewa ukuu wa Mkoa wa Kigoma kwenda kupambana na wahalifu wa amani Tanzania.Na wahalifu wa amani Tanzania kwa tafsiri ya ccm na masheikh ni vyama vya upinzani.Na Zito Kabwe ni mpinzani kindakindaki ambaye kuwa kwake ACT uhalifu kwa machawa na viongozi wengi wa ccm pamoja na serikali ya mama Samiah.
 
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, akisisitiza kuwa kususia uchaguzi ni kosa kubwa litakalogharimu taifa kwa miaka mingine mitano ya mateso ya kisiasa na kiuchumi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Tukuyu, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya siku ya Jumamosi, Zitto amesema ingawa wananchi wamechoshwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupinga kwao hakutakuwa na maana yoyote iwapo hawatajipanga kushiriki katika uchaguzi kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura.

Zitto amesema kuwa ni wazi Watanzania wamechoshwa na vitendo vya wizi wa kura, upuuzwaji wa sauti zao na ufisadi wa kisiasa unaodhoofisha demokrasia. Hata hivyo, ameonya kuwa suluhisho la hayo yote siyo kukaa nyumbani au kususia uchaguzi bali kupambana kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi.

Katika hotuba yake, Zitto ameonya wale wanaoamini kuwa mabadiliko yanaweza kuletwa bila kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwa na wagombea kutoka vyama mbadala ambao wataweza kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi, huku akisema chama kinachoshiriki uchaguzi ndicho kinachopewa nafasi ya kuleta mabadiliko, si kile kinachokaa pembeni.
Zitto atashiriki kwa niaba yetu, tunamtakia Kila la heri, ila hatutaki kulialia baada ya uchaguzi...
 
H
Nakwambia hawezi,Kamanda Siro kapewa ukuu wa Mkoa wa Kigoma kwenda kupambana na wahalifu wa amani Tanzania.Na wahalifu wa amani Tanzania kwa tafsiri ya ccm na masheikh ni vyama vya upinzani.Na Zito Kabwe ni mpinzani kindakindaki ambaye kuwa kwake ACT uhalifu kwa machawa na viongozi wengi wa ccm pamoja na serikali ya mama Samiah.
Haahaa muda utasema...
 
ina maana Zitto anaona wananchi wanaotaka reforms za msingi ktk chaguzi zetu wanakosea?

Well ubunge atapata, lakini it seems hautokuwa na maslahi kwa umma. Utakuwa ni ubunge wa rhetoric zaidi badala ya kuchukua hatua madhubuti kuondoa kasoro za mifumo feki ya uchaguzi.

mkuu wewe unaamini kabisa CCM wanaweza fanya reforms?
 
Ila kweli...
Kila watu tubaki na slogan zetu. Uzuri hata wakipiga kura watu 100 inatosha, matokeo yanapatikana na mshindi anatangazwa, kwani lazima watu wote wapige kura?

Tunaosema October tuna tick tunasonga mbele. (Kitakwimu tuko milioni 8)

Wanaosema NrNe fresh, endeleeni na utaratibu wenu.

Mnaosema mtashiriki na kulinda kura, kila la kheri, ila msije na malalamiko baada ya uchaguzi [emoji3][emoji3]

Hakuna kitu inauma kubadilishiwa matokeo[emoji3][emoji3][emoji3]
Watawapa majimbo kadhaa biashara imeisha
 
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, akisisitiza kuwa kususia uchaguzi ni kosa kubwa litakalogharimu taifa kwa miaka mingine mitano ya mateso ya kisiasa na kiuchumi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Tukuyu, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya siku ya Jumamosi, Zitto amesema ingawa wananchi wamechoshwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupinga kwao hakutakuwa na maana yoyote iwapo hawatajipanga kushiriki katika uchaguzi kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura.

Zitto amesema kuwa ni wazi Watanzania wamechoshwa na vitendo vya wizi wa kura, upuuzwaji wa sauti zao na ufisadi wa kisiasa unaodhoofisha demokrasia. Hata hivyo, ameonya kuwa suluhisho la hayo yote siyo kukaa nyumbani au kususia uchaguzi bali kupambana kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi.

Katika hotuba yake, Zitto ameonya wale wanaoamini kuwa mabadiliko yanaweza kuletwa bila kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwa na wagombea kutoka vyama mbadala ambao wataweza kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi, huku akisema chama kinachoshiriki uchaguzi ndicho kinachopewa nafasi ya kuleta mabadiliko, si kile kinachokaa pembeni.
Yeye aende tu .Hilo Bunge kibogoyo yeye alishiriki uchaguzi alipata nini.Mwaka huu ukipata hata kiti kimoja sijui.
 
Kwa hiyo anafikiri waliogomea kushiriki uchaguzi hawajui haya yote anayosema yeye??!
Tatizo watu hawwawezi kuingia kwenye mapambano ambayo ulishashindwa tayari kwa wizi wa kura. ukizuia unapigwa kama mbwa koko kuna faida yake sasa
 
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, akisisitiza kuwa kususia uchaguzi ni kosa kubwa litakalogharimu taifa kwa miaka mingine mitano ya mateso ya kisiasa na kiuchumi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Tukuyu, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya siku ya Jumamosi, Zitto amesema ingawa wananchi wamechoshwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupinga kwao hakutakuwa na maana yoyote iwapo hawatajipanga kushiriki katika uchaguzi kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura.

Zitto amesema kuwa ni wazi Watanzania wamechoshwa na vitendo vya wizi wa kura, upuuzwaji wa sauti zao na ufisadi wa kisiasa unaodhoofisha demokrasia. Hata hivyo, ameonya kuwa suluhisho la hayo yote siyo kukaa nyumbani au kususia uchaguzi bali kupambana kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi.

Katika hotuba yake, Zitto ameonya wale wanaoamini kuwa mabadiliko yanaweza kuletwa bila kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwa na wagombea kutoka vyama mbadala ambao wataweza kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi, huku akisema chama kinachoshiriki uchaguzi ndicho kinachopewa nafasi ya kuleta mabadiliko, si kile kinachokaa pembeni.
Hata wangesema watakshiriki,,wangeondolewa na Tume ya uchaguzi kwa kutumia kanuni ya mapingamizi
 
Back
Top Bottom