Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Nilipata nafasi ya kumfahamu zitto Kabwe kwa kiasi kidogo wakati akiwa ni mwanachama wa CHADEMA.
Yeye na Julius Mtatiro wakati huo akiwa CUF, walikuwa wananivutia hasa walipokuwa wanachambua mada za uchumi na maendeleo ya jamii.
Mtatiro yeye alitoka kwa hoja ya kuchoka kusubiri fursa akiwa upinzani. Nakumbuka alikuwa humu lakini alipojiunga tu na CCM, Posts na mabandiko yake yote aliyokuwa anaikosoa Serikali na CCM aliomba vifutwe.
Zitto Kabwe yeye aliachana njia na CHADEMA na kwenda ACT-Wazalendo, ambako yupo mpaka sasa.
Zitto ni mtu aliyeonekana atakuja kuwa kiongozi mkubwa mbele ya safari. Na kuna wakati alisema mara tu akifikisha umri wa kugombea Urais angegombea.
Sasa naona kama zitto kapoteana kisiasa. Kuna jambo lolote lile zitto anaweza kufanya kurudisha umaarufu wake wa kisiasa?