Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Mkuu akina Zito wangesema wahusika wote wa escrow wakamatwe na sio watu wawili tu.
Hivi watu wanaoweza kumfungulia kesi spika wa bunge na raisi wa nchi, wanashindwa nini kuwafungulia kesi hao watu waliobeba hela za escrow kwenye mikokoteni kama kweli ni hela ya serikari na wana amini wanahatia.
 
Huwa nayakumbuka maneno ya Baba wa taifa. "Katiba ya Tanzania imempa madaraka makubwa sana Rais wa Tanzania. Siku akiingia madarakani mwendawazimu, tutapata shida". Hayo ni maneno ya Nyerere. Nitawaletea video clip, ninayo.
Haina msaada wowote.,.mbona yeye alikua anajua na akuweza bdilisha kwa manufaa ya wananchi akiwa Rais pendwa
 
Wewe ndiyo shabiki pumbavu waliokula pesa za kivuko cha Dar Bagamoyo wameshitakiwa wapi? Kivuko kipo wapi sasa? Thamani yake tshs ngapi? Chuki unafiki unavyo wewe mshamba, wapo wapi walitafuna pesa za Richmond? Pesa za Rada, bomba la Gesi, kiwanda Hewa huko Lindi, wapo wapi waliouza nyumba za Serikali wakajiuzia nyumba kibao kienyeji na zingine kugawa kwa hawala ambao hawakuwa watumishi wa Serikali, wapo wapi walio kula Tilion 1.5 kienyeji wakata kumtoa kafara CAG kwa njia haramu? CCM mmetafuna pesa nyingi list ya tuhuma ni kubwa acha kujitoa fahamu kuja hapa kutaka kuwatukana wachangiaji wakati wewe mwenyewe huna kumbukumbu ya madhambi yenu kibao.
Good umelipa za uso hilo li Pimbi halina hamu li kamongo la kijani la Lumumba.
 
Mimi kila siku huwa najiuliza watanzania tumemkosea nini Mungu mpaka akaamua kumleta shetani kupitia ccm sipati jibu?
Na sasa shetani yupo kwa Bashite maana yeye na Le mutuz wanamiliki utitiri wa waganga wa kienyeji toka mataifa mbalimbali kwa minajili ya kumlinda mtukufu na wao wenyewe.
 
Msaliti wa karne. Waliokamatwa si ndiyo hao aliowataja kwa ufisadi?
 
Hivi watu wanaoweza kumfungulia kesi spika wa bunge na raisi wa nchi, wanashindwa nini kuwafungulia kesi hao watu waliobeba hela za escrow kwenye mikokoteni kama kweli ni hela ya serikari na wana amini wanahatia.
Steven wasira anawajua kwa majina mtafute atakutajia ingawa mmoja ni mmiliki wa fish market ya pale Oyestabay
 
Waliotafuna bilion 251 wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi Hewa wamekamatwa?
 
CCM wameona uchaguzi wa mwaka huu umewafika shingoni wameanza figisu zao kama kawaida. Madai ya kubumba na kubambika watu kesi hayajaanza leo wala jana. CCM mnatia aibu sana.
Ni vigumu kesi ya kubambika kueleweka mahakamani
 
Watu sio maji kuwa hayana idadi/hayahesabiki.

Ni vizuri ataje majina ya watu anaodai wamebambikiwa kesi ya uhujumi uchumi ili tuwajue kuliko kuongea lugha za kisiasa.

Kinyume cha hivyo ni kutafuta tambo za kisiasa!
Hiyo hoja tu ya Rais kwamba watu "watubu" makosa yao halafu "warejeshe" kiasi wanachotuhumiwa "kupora", inanuka. ukiangalia watu wamekaa magerezani miaka nenda rudi, halafu mtu anakuja na "proposal" kama hii, unaona tu wazi kwamba kashindwa kuwahukumu ila anataka fedha yao. "wakereketwa" na "wanaharakati huru" mnaweza kuongea vyovyote mnavyotaka, lakini angalau Kamanda Sirro katufungua macho kwamba kumbe wahusika huwa wanasoma mitandaoni na wanajua kwamba wanatenda hayo madhambi.
 
Hivi ile mahakama ya mafisadi iliishia wapi? Mashauri mangapi yalisikilizwa? Mashauri mangapi yalitolewa maamuzi?

Awamu hii siasa imetamalaki kuliko maelezo. Si polisi, si mahakamani, wapi pamenusurika? Kote ni siasa kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom