PreGE2025 Zitto kugombea Ubunge: Rasmi ACT na CCM waungana kupinga mabadiliko No Reform No Election

PreGE2025 Zitto kugombea Ubunge: Rasmi ACT na CCM waungana kupinga mabadiliko No Reform No Election

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mtu hatari kwenu Chadema ni mamluki Lissu. Ameiua Chadema kwa ubinafsi wake.

Huwezi kuzuia Chama chako kushiriki uchaguzi halafu utegemee kuungwa mkono na vyama vinavyoongoza wanachama wao kutumia haki yao ya kushiriki uchaguzi.

Huwezi kushika dola kwa kususia uchaguzi;vyama vyote makini vinashindana kwenye uchaguzi ili kushika dola.

Kama hutaki kushiriki uchaguzi kaa kwa kutulia, usijifanye mwamba ukajaribu kuzuia uchaguzi utakutana na vyombo vya sheria, utawekwa unapostahili.
🚮🚮🚮🚮🚮 Ahsante kwa mchango na mawazo yako!
 
Zito hana exposure ya upinzani ni kama kafulila tu. Zito ni mzugaji tu na jimbo watampa. CCM wako tayari kuachia majimbo na kata kadhaa ili kufanya mchanganyiko fulani ionekana CHADEMA waligoma bure uchaguzi ulikuwa huru na haki na kina zito na wanazi wengine wataunga mkono kuwa uchaguzi haukuwa na dosasi. Hizi siasa wakadanganye wapuuzi wasiokuwa na hata D moja
 
Zitto anacheza Kete ya udini
Anajua huyu mama ni muislam atamtendea haki , hata hivyo siasa za Zitto ni softness , nilitegemea labda atagombea Urais kama matamanio yake kila mwaka, yeye anaona kwa sasa ubunge utamlipa...Jamaa ni wale msafara wa mamba kenge nao wamo.Kwenye vita usimpleke Zitto atawauza...
 
Zito hana exposure ya upinzani ni kama kafulila tu. Zito ni mzugaji tu na jimbo watampa. CCM wako tayari kuachia majimbo na kata kadhaa ili kufanya mchanganyiko fulani ionekana CHADEMA waligoma bure uchaguzi ulikuwa huru na haki na kina zito na wanazi wengine wataunga mkono kuwa uchaguzi haukuwa na dosasi. Hizi siasa wakadanganye wapuuzi wasiokuwa na hata D moja
Pambana na Hali Yako mama! Achana na zitto we zungumzia tone tone au hiyo sentensi yenu ya kiingereza
 
Hilo zigo ni Zito, siku likipatikana litupiwe baharini lipotelee vilindini.
 
Fisi huwa hashibi na huwa anaamini kuwa yeye pekee ndio anastahili kula.
 
Huyu Jamaa Ni mtu hatari Sana kwenye siasa za upinzani,ukifatilia historia yake ya usaliti,kuvujisha texts,misimamo yake, utagundua kua anakula meza moja na watesi.. katika maandamano yake ya Jana ya kutangaza Nia ya kugombea ubunge Hakukua na polisi wala mgambo Kama wanavyofanyiwa wapinzani,.

Nimefatilia Mahojiano yake mengi Sana,moja maarufu akiwa katika kipindi Cha The Big Agenda akizungumzia Kubakwa kwa uchaguzi 2020,akiwa na data na majina ya watu walioonewa na michezo iliyotumika kufanikisha hilo,akagoma kuutambua ule Uchaguzi,akaita UCHAFUZI..

Leo Chadema wanataka uchaguzi wa haki sheria zifanyiwe mabadiliko #NoReformNoElection Lakini Zitto (Puppet) Ametangaza Nia ya kushiriki Uchaguzi, Tume ileile, Sheria zilezile za 2020. Nini kitabadilika? unafikiri Utashinda? OH nimefahamu, Wamekuahidi Utashinda uchaguzi Kama ACT mlivyo kubaliana na CCM Zanzibar kuongoza? Kwako kushinda sio Tatizo bila Shaka..

Zitto Kawa Mpinzani wa Chadema sio CCM

1: Wapinzani kutoungana kususia uchaguzi kunaipa Nguvu CCM na Serikali kwa kuonekana Hoja za Chadema za kibinafsi sio takwa la upinzani (Personal agenda)..

2: Vita itahama from Udikteta(CCM) vs Upinzani Hadi Chadema Vs ACT

3: Kama mabadiliko Yana faida kwa Wapinzani wote ikiwemo CHAUMA na ACT,tendo la kutoungana ina maana Kuna watu wapo upande wa CCM ambayo kwao mabadiliko Ni taboo..

Katika Time ambayo taifa linatakiwa kuungana,kua wamoja dhidi ya wakandamizaji ,akitokea mtu yeyote awe Sheikh, Askofu, Celebrity ,Mwanasiasa akijaribu ku change narrative Ya kinachopiganiwa, simply yupo upande wa Dikteta.

Na hili suala sio about personality, Dini Wala Ukanda, it's about how narrative warfare works. Muda wa Watu kuungana na kua wamoja, the most effective tool inayotumika na Serikali Ni kuwatenga watu kidini, kisiasa, kiitikadi. Sitoshangaa kusikia Mikutano ya ACT ina baraka za Police na Fedha za serikali zitatumika

Tatizo la ACT wanataka kuchukuwa nafasi kwa kusamahewa. Lakini kupewa viti kwa msamaha hakuta tatua tatizo la kisheria la haki. Hamuwezi kuishi kwa huruma halafu mkategemea kuchukuwa dola ambayo ndiyo mnaiomba
 
Zito ni mpinzani wa yeyote anayemnyima mapato yake binafsi. Maadam safari hii Samia anampa mapato ya kutosha, Zito na ACT ndio waliopangwa kutumika kuudanganya ulimwengu kuwa tanzania kulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi.

Kuwa na msaliti kama Zito kwenye kundi moja la upinzani, ni hatari kuliko kuwa na maadui 100 walio wazi.
 
Lini Zitto alishawwhi kuunga mkono mabadiliko?

Zitto ni CCM to the core, kama ilivyo ACT ni funded subsidiary ya CCM.
Samahani kidogo, mkuu 'Ngurukia'. Pamoja na kukubaliana nawe kiasi, lakini naona waTanzania katika kutaka kujionyesha u-'modest' wetu, mara nyingi tunashindwa kusema kitu sahihi tunacholenga kukisema, pengine kwa uoga tu tusionekane kuwa watu wa kundi fulani.

Ngoja nijaribu kueleza ninavyo mwona Zitto.
Mleta mada akeleza vizuri jinsi Zitto alivyo uona uchaguzi wa 2020 na kuuzungumzia jinsi alivyo uona. Uchaguzi huo ni CCM iliusimamia na iliuongoza, lakini Zitto hakukubaliana na ulivyokwenda, na kwa hiyo hata matokeo yake hakuyaamini.
CCM ya wakati huo Mwenyekiti wake alikuwa nani, na viongozi ngazi mbalimbali walikuwa ni tofauti sana na hawa waliopo sasa?

Twende mbele moja kwa moja hadi 2025. CCM kilicho badilka huko ni kipi katika muda huo wa miaka mitano. CCM sasa inaye Samia kama mwenyekiti; na kwa kweli hakuna mabadiliko makubwa ndani ya CCM hiyo hiyo.
Sasa kinachomtia moyo Zitto na CCM hii ya sasa na kuiona iwe tofauti na ile ya 2020 ni mabadiliko yapi?

Mimi nasema Zitto, kwa sababu zake mwenyewe, anampenda sana Samia, ambaye ni Mwenyekiti wa chama; ambaye ameweka mazingira rafiki kwa wapinzani aina ya Zitto.
Nimemaliza kujieleza.

Lakini swali nililo nalo: kwa nini wapinzani wa aina hii huwa hawapendi kuungana, au kuingizwa moja kwa moja ndani ya CCM?
Kwa sababu wanao umuhimu wakiwa huko huko nje ya CCM, siyo ndani ya CCM.
 
Kwa hesabu za Zito anaona, Hii ndo Nafasi ya ACT kua chama kikuu cha Upinzani.

Hapa anaona hao G55, Wanajichelewesha kuhamia ACT pamoja na hao COVID 19.

Anasahau kua Watu wanao ipigania CHADEMA ni wapenda mabadiriko. Kama CHADEMA haitokuwepo kwenye kinyang'anyiro cha kula basi, Na wao HAWATOONEKANA kwenye Foleni ya kupigia kura
 
Samahani kidogo, mkuu 'Ngurukia'. Pamoja na kukubaliana nawe kiasi, lakini naona waTanzania katika kutaka kujionyesha u-'modest' wetu, mara nyingi tunashindwa kusema kitu sahihi tunacholenga kukisema, pengine kwa uoga tu tusionekane kuwa watu wa kundi fulani.

Ngoja nijaribu kueleza ninavyo mwona Zitto.
Mleta mada akeleza vizuri jinsi Zitto alivyo uona uchaguzi wa 2020 na kuuzungumzia jinsi alivyo uona. Uchaguzi huo ni CCM iliusimamia na iliuongoza, lakini Zitto hakukubaliana na ulivyokwenda, na kwa hiyo hata matokeo yake hakuyaamini.
CCM ya wakati huo Mwenyekiti wake alikuwa nani, na viongozi ngazi mbalimbali walikuwa ni tofauti sana na hawa waliopo sasa?

Twende mbele moja kwa moja hadi 2025. CCM kilicho badilka huko ni kipi katika muda huo wa miaka mitano. CCM sasa inaye Samia kama mwenyekiti; na kwa kweli hakuna mabadiliko makubwa ndani ya CCM hiyo hiyo.
Sasa kinachomtia moyo Zitto na CCM hii ya sasa na kuiona iwe tofauti na ile ya 2020 ni mabadiliko yapi?

Mimi nasema Zitto, kwa sababu zake mwenyewe, anampenda sana Samia, ambaye ni Mwenyekiti wa chama; ambaye ameweka mazingira rafiki kwa wapinzani aina ya Zitto.
Nimemaliza kujieleza.

Lakini swali nililo nalo: kwa nini wapinzani wa aina hii huwa hawapendi kuungana, au kuingizwa moja kwa moja ndani ya CCM?
Kwa sababu wanao umuhimu wakiwa huko huko nje ya CCM, siyo ndani ya CCM.
Umeongea vizuri mkuu Kama swali lako ningekopa niweke kwenye mada yangu,..

Kuhusu Zitto "kumpenda sana Samia" nje ya siasa inasemekana ni marafiki Wazuri kabla ya Urais..
 
Umeongea vizuri mkuu Kama swali lako ningekopa niweke kwenye mada yangu,..

Kuhusu Zitto "kumpenda sana Samia" nje ya siasa inasemekana ni marafiki Wazuri kabla ya Urais..
Ruksa tu mkuu, hilo swali.
 
sasa gentleman,
wewe si ung'ang'ane na nonsense za chama chako, na wengine nao watumie uhuru na haki zao za kikatiba kufanya yao kulingana na mipango mikakati ya vyama vyao?

kwamba mihemko na kukurupuka kwa chama chako kinachoongozwa na vibaka na matapeli wa kisiasa, ukadhani vyama vingine vya siasa vitababaika right?

kua huru kufanya siasa kadiri unavyoona inafaa ndani ya Tanzania.
Chuki binafsi ni kitu mbaya sana 🐒
Akili kubwa sana hii imeongea hapa.
 
Back
Top Bottom