PreGE2025 Zitto kugombea Ubunge: Rasmi ACT na CCM waungana kupinga mabadiliko No Reform No Election

PreGE2025 Zitto kugombea Ubunge: Rasmi ACT na CCM waungana kupinga mabadiliko No Reform No Election

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katika wanasiasa wanafiki, haka ka jamaa ni numberi one.

Ni kazee ka kuuma na kupuliza - kazee ka kuwinda fursa.

Hamna upinzani humo, full kaole.
 
Katika wanasiasa wanafiki, haka ka jamaa ni numberi one.

Ni kazee ka kuuma na kupuliza - kazee ka kuwinda fursa.

Hamna upinzani humo, full kaole.
Ila slaa aliyetokea "mchana kweupeee" na Sasa kurudi tena kufanya kikamilifu kazi yake aliyotumwa si mnafiki, au sio? Wowote wengi waliohama huko na kwenda kujiunga ccm si wanafiki usipokuwa Zitto tu. Chadema mna shida gani na zitto manina zenu nyie?!!!!! Akiwala viboga mtamlaumu?!!!!!
 
Huyu Jamaa Ni mtu hatari Sana kwenye siasa za upinzani,ukifatilia historia yake ya usaliti,kuvujisha texts,misimamo yake, utagundua kua anakula meza moja na watesi.. katika maandamano yake ya Jana ya kutangaza Nia ya kugombea ubunge Hakukua na polisi wala mgambo Kama wanavyofanyiwa wapinzani,.

Nimefatilia Mahojiano yake mengi Sana,moja maarufu akiwa katika kipindi Cha The Big Agenda akizungumzia Kubakwa kwa uchaguzi 2020,akiwa na data na majina ya watu walioonewa na michezo iliyotumika kufanikisha hilo,akagoma kuutambua ule Uchaguzi,akaita UCHAFUZI..

Leo Chadema wanataka uchaguzi wa haki sheria zifanyiwe mabadiliko #NoReformNoElection Lakini Zitto (Puppet) Ametangaza Nia ya kushiriki Uchaguzi, Tume ileile, Sheria zilezile za 2020. Nini kitabadilika? unafikiri Utashinda? OH nimefahamu, Wamekuahidi Utashinda uchaguzi Kama ACT mlivyo kubaliana na CCM Zanzibar kuongoza? Kwako kushinda sio Tatizo bila Shaka..

Zitto Kawa Mpinzani wa Chadema sio CCM

1: Wapinzani kutoungana kususia uchaguzi kunaipa Nguvu CCM na Serikali kwa kuonekana Hoja za Chadema za kibinafsi sio takwa la upinzani (Personal agenda)..

2: Vita itahama from Udikteta(CCM) vs Upinzani Hadi Chadema Vs ACT

3: Kama mabadiliko Yana faida kwa Wapinzani wote ikiwemo CHAUMA na ACT,tendo la kutoungana ina maana Kuna watu wapo upande wa CCM ambayo kwao mabadiliko Ni taboo..

Katika Time ambayo taifa linatakiwa kuungana,kua wamoja dhidi ya wakandamizaji ,akitokea mtu yeyote awe Sheikh, Askofu, Celebrity ,Mwanasiasa akijaribu ku change narrative Ya kinachopiganiwa, simply yupo upande wa Dikteta.

Na hili suala sio about personality, Dini Wala Ukanda, it's about how narrative warfare works. Muda wa Watu kuungana na kua wamoja, the most effective tool inayotumika na Serikali Ni kuwatenga watu kidini, kisiasa, kiitikadi. Sitoshangaa kusikia Mikutano ya ACT ina baraka za Police na Fedha za serikali zitatumika
Zito akili nyingi anatafuta chakula. Siasa ndo sehemu pekee yenye uhakika wa kula kwa raha zote
 
Zito akili nyingi anatafuta chakula. Siasa ndo sehemu pekee yenye uhakika wa kula kwa raha Zote
Mtu ambae Hana maadili, muongo,msaliti,Mwizi,hawezi kua na akili..Kua na akili Ni package ya vitu vingi..waafrica masikini sababu hatuna akili..na sifa za juu hizo ndio zinatutambulisha
 
Zitto ni msaka fursa aka msaka tonge na ndiyo maana kqjitenga kabisa na wote wanaodai kwamba uchaguzi huwa hauko huru.

Yeye anaona kila mkitu huwa sawa na ndiyo maana anagombea Ubunge Kigoma mjini na tunza post yangu kama mabafiliko hayatafanyika basi atapewa na ndiye atakuwa KUB.

Watu kama hawa walikuwepo hata wakati wa kupigania Uhuru wa nchi. Mnakaa kikao cha siri jamaa anakwenda kuchoma utambi wote kwa wazungu wanakuja wanawadabua ka kuku bandani.
 
Mtu hatari kwenu Chadema ni mamluki Lissu. Ameiua Chadema kwa ubinafsi wake.

Huwezi kuzuia Chama chako kushiriki uchaguzi halafu utegemee kuungwa mkono na vyama vinavyoongoza wanachama wao kutumia haki yao ya kushiriki uchaguzi.

Huwezi kushika dola kwa kususia uchaguzi;vyama vyote makini vinashindana kwenye uchaguzi ili kushika dola.

Kama hutaki kushiriki uchaguzi kaa kwa kutulia, usijifanye mwamba ukajaribu kuzuia uchaguzi utakutana na vyombo vya sheria, utawekwa unapostahili.
Japo mimi sio mwanasiasa ila Muwe hata na huruma kidogo.
 
Yaani atashangaa anaporudisha form yake ,paap ofisi ya msimamizi wa uchaguzi inafungwa na anamwambia hatuna nafasi ya kupokea form yako .Wakifanikiwa kupokea ,watamwambia imekosewa .Za CCM huwa hazikosewi .Mara paap hana kitambulisho cha mjasiriamali .Yaani nchi hii sijapatia mfano.Anyway bila reform ,sipigi kura kwa kweli WAJIPITISHE TU.
kwake haiwezi kutokea kwakuwa ni maelekezo wasiojuka kusoma ni chadema tu hata kama wama Phd
 
Back
Top Bottom