A controvesial CHADEMA MP from Kigoma North constituency has once again tested the wrath of Union Parliament today, after refusing to detract his ownstatement that " majibu aliyotoa waziri Sumari kwa Mh. Slaa ni ya HOVYOHOVYO..." pamoja na pressure ya wazi toka kwa two CCM MPs wakiomba mwongozo wa Mwenyekiti, Zitto aligoma katakata kufuta kauli yake na kudai kwamba wabunge kadhaa (nadhani akimaanisha wa CCM), wameshaongea kauli za kutatanisha katika bunge hili lakini hakuna hatua zilizochukuliwa..alimalizia kwa kusema "NIPO TAYARI KWA LOLOTE" kabla hajendelea kuchangia mjadala wa budget..
=============================
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia kuhusu ufisadi. Kamati ya Bomani nitaiomba kuinukuu katika masuala ambayo alisumbuliwa sumbuliwa Dr. Slaa juzi hapa. Alisema hivi Kamati ya Bomani ilipendekeza hivi Kwa kuwa malipo ya Dola za Marekani 132,000,000 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Netbank ya South Africa hayana uwiano dhahiri na mkopo wa Dola za Marekani 10,000,000 zilizokuwa zimekopwa na Kampuni ya Meremeta kutoka Netbank Serikali ifanye uchunguzi kuhusu malipo hayo. Hii ni taarifa ya utekelezaji wa ahadi za Serikali ambao Waziri Mkuu aliitoa mwaka jana, taarifa hiyo inasema ukurasa 23. Taarifa ya Serikali inasema Uchunguzi unaendelea, uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha za Serikali kupitia Benki Kuu kwa Kampuni ya Meremeta na Tangold unaendelea, Julai mwaka 2008, Taarifa ya Serikali ambayo Waziri Mkuu ameitoa hapa. Juzi Waziri Sumari anamjibu ovyo ovyo tu Mbunge hapa, tena Katibu Mkuu wa Chama kinachokua kuliko vyama vyote Tanzania anamjibujibu tu.
[MHE. KABWE Z. ZITTO]
What is a contradiction kati ya taarifa ya Serikali na majibu ambayo Mawaziri wanayatoa. CAG anafanya uchunguzi kuhusu Meremeta na nilichokiomba ni kwamba Serikali isiingilie Sheria ya Ukaguzi inasema kwamba CAG ana uhuru wa kufanya uchunguzi wowote, CAG ame-confirm kwamba anafanya uchunguzi kuhusu Meremeta na tunaiomba Serikali isingilie mpaka taarifa hiyo inapokuja, lakini hapo hapo Serikali
MWONGOZO WA SPIKA
MHE. PONSIANO D. NYAMI: Kanuni 68 na pia ningepata utaratibu. Katika kuongea kwa Mheshimiwa aliyekuwa anachangia sasa hivi sidhani kama ni uungwana. Ukiacha heshima aliyonayo na umri unavyokwenda kitendo cha kusema Waziri anajibu ovyoovyo, maana yake Serikali inajibu ovyoovyo na kwa maana hiyo ni kutokufikiria majibu wanayoyajibu. Lugha hiyo ni ya kuudhi sana na haipaswi kuwa ni lugha ya Bunge na haipaswi kukaa ndani ya Hansard.
Ninaomba maneno hayo ayafute na aombe radhi. (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa, nitamruhusu Mheshimiwa aendelee bila ya kuyatumia hayo maneno kwa sababu hayapendezi.
WABUNGE FULANI: Asiendelee
MWENYEKITI: Naomba niendelee kuongea asiendelee kuyatumia na yafutwe kwenye Hansard, naomba uyafute hayo maneno ovyoovyo halafu uendelee kuchangia.
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge hapa alitaka Mawaziri walaaniwe hakufuta kauli yake. Kuna Mbunge hapa leo asubuhi amemshambulia waziwazi Waziri wa Utumishi Mheshimiwa Hawa Ghasia hakuna mtu aliyesimama kuweza
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabwe Zitto naomba ukae.
MHE KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, maneno haya sitayafuta.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge usibishane na Kiti, nilichotaka ufanye ni kwamba ufute maneno yako halafu uendelee kuchangia, usianze kubishana na kuanza kutoa reference ya mambo yaliyopita, naomba ufute hiyo tu hiyo ovyoovyo halafu uendelee kuchangia. Tafadhali sana.
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu ambayo Waziri alimpatia Mbunge wa Karatu yalikuwa ni ya ovyoovyo nasimamia maneno yangu na niko tayari kwa lolote ambalo Meza itakayoamua. (Makofi)
MWENYEKITI: Naomba uendelee sasa na mchango wako na hatua zaidi zitafuata kuhusiana na hiyo kauli yako. (Makofi)
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho.
MWONGOZO WA SPIKA
MHE. DR. ZAINAB A. GAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Waziri Kivuli wa Wizara hii alipokuwa anazungumza alikatazwa kuzungumza baadhi ya mambo pamoja na Meremeta, leo inaruhusiwa tena lile lile alilokataza Naibu Spika, linazungumzwa, naomba Mwongozo wako.
MWENYEKITI: Ahsante nadhani ni sahihi katika kumbukumbu kwamba Mheshimiwa Waziri Kivuli alipokuwa akiongea masuala yote yaliyohusiana na Meremeta alitakiwa ayafute na yaondolewe kwanye Hansard. Kwa hiyo Mheshimiwa Zitto Kabwe utamalizia bila ya kuyazungumza tena masuala hayo kwa sababu uamuzi ulikwishakutoka wakati ule kwamba hayo masuala hayatazungumzwa humu ndani.
Mheshimiwa Kabwe endelea.