Zitto: "Majibu ya Sumari ni 'ovyo ovyo'"; atakiwa kufuta kauli!

Zitto: "Majibu ya Sumari ni 'ovyo ovyo'"; atakiwa kufuta kauli!

But more than that, I despise the myopic thinking holding that two wrongs do make a right.

If Zitto wants to have the support of thinking people, he should stand by his words for their own merit and appropriateness, not on a relative comparison towards a CCM imbecile's hogwash.Doing the latter will be stooping down to the imbecile's level.
Umeniwahi mkuu.
** Blushing **
 
Mh. Zitto na Mh Dr. Slaa::

Shukrani za pekee kwa kuweza kusema kile ambacho kinagusa asilimia kubwa ya watanzania especially vijijini.

Bravo na mungu awabariki kwa kututetea sisi watanzania maskini ingawaje mnapigwa vita huko bungeni na kwingine.
 
Nimesema ukweli zitto alikuja na uwongo wake tukaangalia golden oppotunity katika maswali ya moja kwa moja akashindwa kujibu akakimbilia kwingine toka siku hiyo nikaona ahaa ndio maana kule kigoma walimchagua na hawaletei chochote na hata hawa vijana sijui kwanini wanatoa support kwa waongo , wavuruga nchi na wachonganishaji kama hawa ---

we dogo si undelee kuchangia kule kwenye jukwaa la teknolojia na wenzako akina JOSM.huku acha watu wenye akili zao waendelee ,...we dogo unaboa bana yaani ungekua unakunywa pombe ningesema ni mawazo ya kilevi sasa bitter lemon tu zinakuletea mawazo ya ajabu hvi ungekua unakula kitu ungekuaje?
 
Nakuunga mkono Zito,hakuna kuwaogopa hao wazandiki wanaonea wapinzani....muda wao umefikia....wataacha tu.
 
kwa kweli hili ndio bunge na hii ndio kazi ya wabunge wengekuwa hivi toka enzi za utawala wa mheshimiwa Mkapa basi mambo mengi yangekuwa sawa mawaziri wetu wameliangamiza sana taifa hili hawajali maslahi ya taifa na ndio maana wanalifanya bunge kama mahali pa mashala.

Mh Zitto bravoo katika hilo usifute kauli yako kwani huyo meremeta ni "boooom shell" tunasubiri lipasuke inauma pale masula ya utaifa yanapojadiliwa mwingine analeta kejeli utafikiri yeye sio mtanzania hawa baadhi ya mawaziri wa nchi hii hawana uzalendo kabisaaa!!!

Hebu angalia Uingereza kashifa kidogo tu za mawaziri imebidi waachia ngazi lakini utamaduni huo hapa bongo hakuna mpaka wakaliwe kooni na siku likilipuka mheshimiwa Zitto hakikisha wahusika wote wa meremeta kizimbani hiki keki hata kama ndogo lazima tule wote we mpaka leo kuna sehemu tanzania hii wanafunzi wanakaa chini hawana madawati majengo yao ya shule hayastahili kusomea halafu yule babu yetu juzi anasifuu tu!

Pale bungeni yule naye kaishiwa na ndio maana harudi bungeni tena huo huko CCM hawamtaki na kinachomfanya kusema yale ya juzi kwa kuwa alikula mkopo wa benki kuu jambo ambalo linamtesa mpaka leo moyoni heshima yake kwishine siku nyingi si afadhali angenyamza kwani kama huna la kuongea ni lazima useme bungeni awaachie jimbo vijana mwakani na unajua huwezi mponda mtu ambaye ulimega keki wakati wa uongozi wake na akakuangalia tu sasa mh Zitto bravo
 
What I understood from Zitto’s response to Sumari is not the fact that he called the Minister “ovyo” but the answers he provided were not satisfactory. ‘Careless’ is what “ovyo” can be translated to, as close to that in English, and it’s an opinion too. If Tanzanian MPs have reached a point of reproving someone for simply being opinionated, tena to matters of fact then they seriously should not be in that house. If I am not contented with your answers, and on top of that the manner in which you communicated them was so sloppy I can’t tell you that??? How would I accomplish that? And who does Sumari think he is anyway?? Zito is representing the people and so he is their voice, if people are not satisfied with the government and they talk nonsense then he surely should let them know wasirudie au waje na majibu mazuri.
 
yeah! kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani mjengoni...mara nyingi wabunge wa sisiEmu wanabeza wapinzani kwa kusema hawana sera na hata wayasemayo ni propaganda...ni vizuri sana kutumia takwimu za serikali kuikosoa ,hivyo ndo inavyofanyika duniani kote....wabunge wa sisiEmu wanaodai kupinga ufisadi nadoubt kidogo uzalendo wao..mtu anawalaani mawaziri,anaponda mgawanyo mbovu wa rasilimali i mean kwenye budget,anasisitiza kuwa serikali haifanyi kazi yake ipasavyo na MWISHO anamalizi naunga mkono hoja 100%?????!!!!tena wengine ni maprof na wengine ni madr. Mungu iponye Tanzania
 
Tumewekewa hansard record ya Mh. Zitto.

Wengine tungeomba, tafadhali, record ya maneno Waziri Sumari, sentensi au paragraph nzima, neno kwa neno.

"tungeomba, tafadhali" ndiyo nini? Kama hutaki kuomba usiombe, kama unataka kuomba wewe omba tu, kama unampango wa kuomba baadaye subiri hadi ukiwa tayari, sasa "tungeomba, tafadhali" ndiyo tuelewe nini? hii lugha siyo ngumu hivyo. Halafu "wengine" manake yake nini?

Halafu hizo komakati ya "tungeomba, tafadhali" ndiyo zinafanya kazi gani hapo?; hiyo "nge" kwenye "tungeomba" inavunja kabisa neno "tafadhali".

Halafu, unasema "record ya maneno (ya) Waziri Sumari ambayo inatosha kujumuisha "sentensi, au paragraph (ambayo ina sentensi), neno kwa neno (ambayo imo kwenye "record ya maneno").

Hivyo "record ya maneno" inatosha.

unaweza kurudia kauli yako katika lugha inayoeleweka ikimaanisha ulichotaka kumaanisha?
 
"tungeomba, tafadhali" ndiyo nini? Kama hutaki kuomba usiombe, kama unataka kuomba wewe omba tu, kama unampango wa kuomba baadaye subiri hadi ukiwa tayari, sasa "tungeomba, tafadhali" ndiyo tuelewe nini? hii lugha siyo ngumu hivyo. Halafu "wengine" manake yake nini?

Halafu hizo komakati ya "tungeomba, tafadhali" ndiyo zinafanya kazi gani hapo?; hiyo "nge" kwenye "tungeomba" inavunja kabisa neno "tafadhali".

Halafu, unasema "record ya maneno (ya) Waziri Sumari ambayo inatosha kujumuisha "sentensi, au paragraph (ambayo ina sentensi), neno kwa neno (ambayo imo kwenye "record ya maneno").

Hivyo "record ya maneno" inatosha.

unaweza kurudia kauli yako katika lugha inayoeleweka ikimaanisha ulichotaka kumaanisha?

Duu huu uwanja wa TUKI na BAKITA nye!
 
Huyu Sumari ni naibu waziri wa fedha , na wakati huo huo anamiliki kampuni kubwa inayouza hisa hapo nchini (Solomon Stockbrokers). Mimi hili jambo aliingii akilini hata kidogo, kwani hiki ni kielelezo cha conflict of interest. Kwa maneno mengine, ofisi yake ndio inayoregulate biashara yake ! Sisi wadanganyika tunategemea ya kuwa manufaa ya umma yatatetewa na huyu muungwana .Only in Tanzania ...
 
Tuwe fair kidogo si wabunge wote wa CCM butu, kuna wale akina mama Malecela Ann Kilango, KImaro, Seleli, Mwakyembe etc etc wanasimamia ukweli

Hawa ndio wa hatari kuliko hata hao wanaoonyesha sura zao kamili. Hawa ndio wanafiki na ndumilakuwili wanaofoka na kutoa povu leo, lakini mwisho wa siku wanaungana na wenzao kupitisha miswada na bajeti za wizi na ya kitapeli. Toka lini maji na mafuta yakachanganyikana kilaini hivyo ?
Selelii, Kilango, na Ole Sendeka,
Mporogomyi, Kimaro na Mwakyembe
Mwambalaswa, Mpendazoe na Shibuda
Shelukindo, Chegeni na Zambi
hivi tuwaeleweje ?
Acheni kelele zenu za kinafiki
wote mwaogelea kwenye uchafu.
Hivyo wote ni wachafu
 
Mh. Zitto,
Mkuu najua unapitia pitia hapa...kwanza hongera.. unajua tena mijitu miingine inahitaji kupigwa bakora ipate kutia akili.. mkuu imefika hiyo..
Isipokuwa kama watang'ang'ania basi wape kwani Ujumbe umeshafika, kama yule kijana alomlamba Mwinyi ganja la uso.. Kinachottetewa hapa ni heshima!. Hivyo fanya uungwana itakapobidi, usifanye hasira wewe kwani wewe ndiye unatakiwa ku enjoy all of this!

Kuna sehemu moja umezungumzia Umaskini na kwamba serikali ilikuwa imepanga mkakati wa KUPUNGUZA umasikini na figure mlizotoa ningependa sana kuelewa mmetumia kipimo gani?.
Nasema hivi kwa sababu kama kwa ujumla (average) pato la mwananchi ni dollar 1, huyo maskini mnayemzungumzia pato lake linaanzia kima kipi haswa maanake ikiwa average ni dollar moja sijui hesabu hizi zinakwenda vipi hadi kutoa hesabu kubwa ya wananchi ktk umaskini...umaskini wa Mtanzania huhesabika akiwa na kipato cha kiasi gani?

Ningependa kuelewa ongezeko hilo toka 11,000,000 hadi 12,700,000 liantokana na kipimo cha pato lipi senti ngapi ndizo kipimo cha umaskini.. maanake hatuna mfumo mzuri wa kodi ambao utamlazimu kila mwananchi kujaza kila mwaka..Na zaidi ya yote kodi nyingi ni za makisio tena siku kwa siku ya biashara na hakuna final tax form za mwaka kwa kila raia.. Ukilipa kodi ndio imetoka.. uwe mfanyakazi wa serikali au shirika hutakiwi kisheria kujaza form za kodi kila mwaka kuonyesha pato lako against kodi uliyolipa kama unatakiwa kulipa zaidi ama kurudishiwa kodi uliyolipa zaidi..
Je, hizi hesabu za kufikia 12,700,000 zimepatikana vipi?..Na utaweza vipi kupunguza umaskini ikiwa huna hesabu ya pato la kila mwananchi!..
 
hongera sana kwanza kwa zitto kabwe kwa kutetea maslahi ya nchi.inaonesha mwenyekiti ni ovyo nae pia pamoja na wabunge wa ccm wengine ambao wanafikiri wako bungeni kwa maslahi ya chama na sio nchi (wananchi).mimi naona tuchapishe karatasi zinazoelezea kazi ya mbunge nini na tukawape wabunge bure hili wajue manake naona kuna wabunge wengine hawajui kazi yao nini.
 
Huyu Sumari ni naibu waziri wa fedha , na wakati huo huo anamiliki kampuni kubwa inayouza hisa hapo nchini (Solomon Stockbrokers). Mimi hili jambo aliingii akilini hata kidogo, kwani hiki ni kielelezo cha conflict of interest. Kwa maneno mengine, ofisi yake ndio inayoregulate biashara yake ! Sisi wadanganyika tunategemea ya kuwa manufaa ya umma yatatetewa na huyu muungwana .Only in Tanzania ...

Rufiji sasa hapo ndiyo kuna conflict of interest kwani inahusu kile sheria yetu inakiita "maslahi ya kifedha"..
 
Alosema Zito hayatoshi inatakiwa waziri anapoongea pumba atokee mbunge mmoja kichaa amtandike kiatu kama alichopigwa bushi ndo tanzania itaendelea.Mbunge sio mtu bali ni watu.Hivyo alichotamka Zito wametamka wananchi wa kigoma na watanzania wote.Serikali yetu ni ovyo,tena ovyooooooooooo.Majambazi na mafisadi watupu,hawapendi kuguswa na maslahi yao.Hongera sana Zito kwa ushajaa wako uwapo bungeni na nje ya bunge letu mfu.
 
Mimi kinachonishangaza sana mbunge wa CCM anasimama anapondaponda budget halafu anasema "naunga mkono asilimia mia"Sielewi hapo naomba muongozo!! Naona hao vijana wadogo wa upinzani wanaakili sana wanajieleza na hoja zao zina substance
 
Rufiji sasa hapo ndiyo kuna conflict of interest kwani inahusu kile sheria yetu inakiita "maslahi ya kifedha"..



Mwanakijiji na Rufiji!

Asante kwa kuliona hilo!!! Conflict of interest haipo kwenye kamusi ya CCM na serikali zake kwani wana CCM ambao wote kuanzia Mwenyekiti wao JMK aka Matonya wana abuse au wanavunja sheria in and out na kwa sababu ya ubabe wao waTZ makondoo nao wanakaa kimya!! Wote wanaopiga kelele huko bungeni from within CCM it's usanii per se!! It is part of the ccm strategy!!

I once said baada ya yule mpuuzi Alhaj Ali Hassan Mwinyi kudanganyika na kufuta Azimio la Arusha na kuleta azimio la Zanzibar (utajirisho wa viongozi )that is when mambo yaliharibika and what you see its only the tip of the iceberg!

Viongozi wote wa CCM wamekosa mandate ya kuwa viongozi ila wanatumia misuli ya dola kujitajirisha lakini iko siku mambo yatabadilika kama sio sasa hata the next 10 to fifteen years!! Tunakumbuka Karamagi na BUZWAGI pomoja na Lowasa... Lowasa na TICTS!!! mASHA NA mAKAMPUNI YOTE YA MADINI!!! mKAPA NA kIWIRA NA sTANDARD cHARTERED aliko na hisa!!! Yona na NBC !!

Leo hii Kingunge na Parking za Dar!!! Nasikia hata Nyumba aliyouziwa yule Mmakonde amepewa kibali na CCM na wachina wanaporomosha hapo Ghorofa la kutisha au ni zile pesa za madini alizochukua!!!au za kutoka jeshini!! What high degree of double standards!! Ni the famous Maokolo Majogo!!
 
Zito mwendo Mdundo,hakuna kuondoa kauli yako, kauli ilikuwa ya Msingi.Mimi ni CCM LAKINI UKO SAFI SIMAMIA KAULI YAKO.
 
Back
Top Bottom