Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,189
- 128,283
Tofauti na hapo mtamfanyaje mkuu?Zitto nakushauri kaa kimya, tuijenge nchi plz, uwe na kumbukumbu jembe.
Tofauti na hapo mtamfanyaje mkuu?Zitto nakushauri kaa kimya, tuijenge nchi plz, uwe na kumbukumbu jembe.
Zitto nakushauri kaa kimya, tuijenge nchi plz, uwe na kumbukumbu jembe.
Kwa mikataba ya namna hii ni wazi kabisa hii inchi haitakuja kuendelea chini ya uongozi wa CCM. Maana kila siku mikataba yenye tija imekuwa haileti manufaa kwa taifa. Huu uchambuzi wa kina umetuhuzunisha sana watanzania maana ni kinyume na matarajio ya wengi.MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO
Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).
Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.
Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.
Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.
Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.
1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO
Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.
Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.
2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M
Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.
Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.
3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.
Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.
Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.
4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote
Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).
Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.
5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria
Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.
Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.
Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa
Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.
Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.
Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.
Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.
Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019
Ina maana sisi ni wajinga?
Ƙama mmegawa rasilimali kwa mabeberu na mnaficha miƙataba mtakuwa watu gani tofauti na kuwa wajinga!
Sasa zito angejuwaje haya wakati majadiliano yalikuwa siri kati ya jiwe kabudi na barric yaani kuna watu sijui kwa nini bado wapo hapa kwenye jukwaa zito kajua baada ya barric kuanika mambo LSE Na NSE
Kwa mikataba ya namna hii ni wazi kabisa hii inchi haitakuja kuendelea chini ya uongozi wa CCM. Maana kila siku mikataba yenye tija imekuwa haileti manufaa kwa taifa. Huu uchambuzi wa kina umetuhuzunisha sana watanzania maana ni kinyume na matarajio ya wengi.
Haya mambo ya kila kitu alijikuta anaishia kusoma mwaka kwenye vioo vya ndege! eti nalo ukawa mtaji wa kisiasaYeye ni mwana siasa lazima aguse kila tukio lolote la kisiasa
Hapa ulikuwa unataka kuongelea kitu gani?Mpinzani wa kupinga. Yeye (Zito) awamu ya nne ndiye alikuwa mstari wa mbele kusema kuwa kinana ni mwizi mkuu wa rasilimali za taifa. Kuwa ni jangiri maarufu wa meno ya tembo. Ajabu hivi sasa yeye ndiye mtetezi mkubwa wa Kinana. Hivi huyu binadamu ni binadamu wa aina gani?
Zitto tuwekee hiyo document au tupe linki tukasome wenyewe!
Kama mnadhani Zitto anadanganya, moja ya vipengele alivyoelezea hapo juu document inasema:-Akiweka nitag mkuu. Watu humu ndani ni wavivu sana wa kufikiri. Zitto alete hiyo link aliosoma yeye ili na sisi tujiridhishe
B: in the event that the dispute is not resolved through negotiation within 30 days, the parties may refer the dispute to conciliation in accordance with the UNCITRAL Conciliation Rules. The conciliator will be independent of the parties, and will not be a national of Tanzania, the United Kingdom, Canada or the United States. If a conciliator is not appointed within 14 days of acceptance of a request for conciliation, the President of the Singapore International Arbitration Centre will appoint the conciliator. A conciliator can make proposals to the parties as to how they might resolve any dispute, but cannot make any binding decision. To resolve a dispute through conciliation the parties would have to reach an agreement, recorded in a binding agreement; and
Maelezo hayo yapo kwenye kipengele cha Dispute Resolution! Mnaona hapo ni namna gani endapo itatokea kushindwa ku-solve any dispute, basi issue itapelekwa mbele in accordance to UNCITRAL Conciliation Rules, na sisi, of course, citizens of arguing parties hawatakuwepo kwenye team!C: Upon issuance of a notice of arbitration commencing the arbitration, the parties shall seek to mutually agree on the arbitral seat or legal place of arbitration. The seat shall be in a jurisdiction which is internationally recognized and experienced in handling complex international commercial arbitration (not being Tanzania, a state which is a member of the East African Community, the UK, Canada or the United States) and is a party to the New York Convention of the Recognition and Enforcement of Foreign Arbitral Awards, 1958.
Haki za Class A and Class B Shareholders zimeelezewa kwenye Shareholders Agreement, lakini Zitto aliposema kwamba hizo shares zetu huwezi kuziweka hata kuwa dhamana ni kutokana na kipengele kinachosema:-New OpCo will be owned 84%/16% by a subsidiary of the Acacia Group and a nominee of the GoT respectively. Acacia will hold its shares in New OpCo as Class A shares and the GoT will hold by way of Class B shares.
Suala la kwamba lile sharti la Tanzania kumiliki 30% akina Kabudi na Magu wameliuza kwa Wazungu, makubaliano yanasema:-(i) Class B shares may only be issued to, held by or transferred to the GoT shareholder and may not be pledged, charged or otherwise disposed of (whereas the Class A shares are transferable to: (a) a financial institution by way of a pledge to secure bona fide debt; (b) an affiliate (with GoT shareholder consent, not to be unreasonably withheld); or (c) a third party (subject to the GoT shareholder’s right of first refusal and with Government consent, not to be unreasonably withheld or delayed), provided, in each case, the transferee enters into a deed of adherence);
(ii) regardless of the number of Class B shares in issue, the Class B shares will at all times be deemed to represent 16% of the shares holding voting and economic rights in the TMC (being collectively, the Class A shares and the Class B shares);
(iii) a holder of Class B shares will not have any pre-emption rights over any allotment of new Class A shares and its proportionate interest will not be affected by such allotment (whereas a holder of Class A shares has pre-emption rights over any allotment of new Class A shares); and (iv) the holder of Class A shares will elect from amongst the directors appointed by them, a chairman of the board of the TMC (whereas a holder of Class B shares has no such right).
Kwahiyo hiyo 16% itaendelea kubaki hivyo hivyo! Vipi kuhusu suala la kusafirisha madini nje? Makubaliano haya hapa:-the GoT will not unilaterally seek to increase its share ownership or economic participation rights in the TMCs;
Kumbe wanayo unfettered rights ya kusafisrisha madini na makinikia nje ya nchi hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kufanya refining and smelting ndani ya nchi!the TMCs will have the unfettered right to export minerals (including doré and concentrates) until refining (in the case of doré) and smelting (in the case of concentrates) are available in Tanzania and the GoT will provide assistance so all required authorisations and/or waivers be granted to theTMCs so as to facilitate export of doré and concentrates;
Kwahiyo ndugu yangu french badala ya kukejeli kwamba watu wa humu ni wavivu wa kufikiri, ungefanya maarifa kwanza kuisoma hiyo doc! Sio lazima Zitto akuletee kwa sababu ipo kwenye website ya Acacia lakini ni ndefu, ina 91 pages!there will be no obligation on the TMCs to construct beneficiation facilities in country;
Kama mnadhani Zitto anadanganya, moja ya vipengele alivyoelezea hapo juu document inasema:-
Maelezo hayo yapo kwenye kipengele cha Dispute Resolution! Mnaona hapo ni namna gani endapo itatokea kushindwa ku-solve any dispute, basi issue itapelekwa mbele in accordance to UNCITRAL Conciliation Rules, na sisi, of course, citizens of arguing parties hawatakuwepo kwenye team!
Sasa kama tunatarajia huko mbele watu wata-resolve issues kwa kuzitangatia maslahi yetu basi tuna safari ndefu!
Kuhusu 16% ya shares zetu kuwa Class B Shares, makubaliano yanasema:-Haki za Class A and Class B Shareholders zimeelezewa kwenye Shareholders Agreement, lakini Zitto aliposema kwamba hizo shares zetu huwezi kuziweka hata kuwa dhamana ni kutokana na kipengele kinachosema:- Suala la kwamba lile sharti la Tanzania kumiliki 30% akina Kabudi na Magu wameliuza kwa Wazungu, makubaliano yanasema:- Kwahiyo hiyo 16% itaendelea kubaki hivyo hivyo! Vipi kuhusu suala la kusafirisha madini nje? Makubaliano haya hapa:-Kumbe wanayo unfettered rights ya kusafisrisha madini na makinikia nje ya nchi hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kufanya refining and smelting ndani ya nchi!
Kama ndivyo, kwanini basi tusiwalazimishe hawa Barrick wajenge mtambo wa kuchenjua makinikia hapa hapa Bongo ili wasiendelee kutupiga changa kwa kusafirisha makinikia nje ya nchi?! Makubaliano yanatoa jibu kwa hilo swali, kwamba:-Kwahiyo ndugu yangu french badala ya kukejeli kwamba watu wa humu ni wavivu wa kufikiri, ungefanya maarifa kwanza kuisoma hiyo doc! Sio lazima Zitto akuletee kwa sababu ipo kwenye website ya Acacia lakini ni ndefu, ina 91 pages!
Mkuu Bome-e, maelezo ya sehemu ya ripoti ni hayo hapo juu, na kisha ayaone Mkuu Tangawizi aliyehoji kwenye uzi mmoja kwanini naamini Barrick ndie wameshinda bila kumsahau ruaharuaha!!