Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Bado tuna safari ndefu sana ila nafurahia kuona baadhi ya Watanzania wameanza kuwa bold kupambana na huyo dhalimu. Sijui matokeo ya huu mpambano yatakuwa yepi lakini naomba sana yawe ni chanya kwa Tanzania na Watanzania ili tuondokane na huyo nduli wa chato.

..halafu majitu haya ndiyo mchana kweupe yanatuma magaidi kwenda kumuua Tundu Lissu.

..Usd 300 million hata watulipe kila mwaka kwa miaka 600 bila riba bado hawawezi kumaliza deni la usd 190 billion tulilotangaziwa na Tume za Prof.Mruma na Prof.Ossoro.

Cc BAK, MTAZAMO
 
..halafu majitu haya ndiyo mchana kweupe yanatuma magaidi kwenda kumuua Tundu Lissu.

..Usd 300 million hata watulipe kila mwaka kwa miaka 600 bila riba bado hawawezi kumaliza deni la usd 190 billion tulilotangaziwa na Tume za Prof.Mruma na Prof.Ossoro.

Cc BAK, MTAZAMO
Kiongozi ukisoma ile ripoti unaweza usiamini! Nakumbuka mara ya kwanza niliisoma asubuhi ya leo lakini niliishia njiani kwa kudhani ile ripoti ambayo nilifowadiwa ni fake hadi baadae kabisa nilipokuja kui-verify na kuona kumbe ipo kwenye website yao!
 
Watu kama Zito ndiyo walitakiwa wapite bila kupigwa lakini utasikia Lusinde kapita bila kupigwa. Hii nchi ni ya ajabu sana! Sijui urais ni bahati, tukisema unatoka kwa Mungu tutakuwa tunamkosea kwa sababu hakuna Mungu atakayependa tuliwe kiasi hiki!!
 
Zito huo no ujinga kwani kama unge yasema hayo kabla ya hili sekeseke kufika note huku ungepata hasara gani.?
Sasa unaongea sahizi tuta kusaidiaje?
Auwewe unafurahi tukikosea we we ukosoe uonekane Wa maana sisi tupate hasara tuwe tayari tumeliwa!.nimekudharau kuanzia Leo!
Kosa si la ndugu Zitto, kosa ni la hao wanaokataa kupata ushauri mapema sana kutoka kwa akina Zitto, na hata wakina TAL. Sasa tatizo unakuja kukutana lao mwishoni, je hapo ni nani wa kulaumiwa? Na uwe una kumbukumbu sahihi pia ile Panel ya watu wa majadiliano ilifichwa na haikutakiwa kujulikana, je unaweza jiuliza ni kwa nini?
 
Kama mnadhani Zitto anadanganya, moja ya vipengele alivyoelezea hapo juu document inasema:-

Maelezo hayo yapo kwenye kipengele cha Dispute Resolution! Mnaona hapo ni namna gani endapo itatokea kushindwa ku-solve any dispute, basi issue itapelekwa mbele in accordance to UNCITRAL Conciliation Rules, na sisi, of course, citizens of arguing parties hawatakuwepo kwenye team!

Sasa kama tunatarajia huko mbele watu wata-resolve issues kwa kuzitangatia maslahi yetu basi tuna safari ndefu!

Kuhusu 16% ya shares zetu kuwa Class B Shares, makubaliano yanasema:-Haki za Class A and Class B Shareholders zimeelezewa kwenye Shareholders Agreement, lakini Zitto aliposema kwamba hizo shares zetu huwezi kuziweka hata kuwa dhamana ni kutokana na kipengele kinachosema:- Suala la kwamba lile sharti la Tanzania kumiliki 30% akina Kabudi na Magu wameliuza kwa Wazungu, makubaliano yanasema:- Kwahiyo hiyo 16% itaendelea kubaki hivyo hivyo! Vipi kuhusu suala la kusafirisha madini nje? Makubaliano haya hapa:-Kumbe wanayo unfettered rights ya kusafisrisha madini na makinikia nje ya nchi hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kufanya refining and smelting ndani ya nchi!

Kama ndivyo, kwanini basi tusiwalazimishe hawa Barrick wajenge mtambo wa kuchenjua makinikia hapa hapa Bongo ili wasiendelee kutupiga changa kwa kusafirisha makinikia nje ya nchi?! Makubaliano yanatoa jibu kwa hilo swali, kwamba:-Kwahiyo ndugu yangu french badala ya kukejeli kwamba watu wa humu ni wavivu wa kufikiri, ungefanya maarifa kwanza kuisoma hiyo doc! Sio lazima Zitto akuletee kwa sababu ipo kwenye website ya Acacia lakini ni ndefu, ina 91 pages!

Mkuu Bome-e, maelezo ya sehemu ya ripoti ni hayo hapo juu, na kisha ayaone Mkuu Tangawizi aliyehoji kwenye uzi mmoja kwanini naamini Barrick ndie wameshinda bila kumsahau ruaharuaha!!
Basically kinachoelezewa kwenye dispute resolution agreement ni ‘stabilisation clause’ hawa watu wameanza biashara ya uwekezaji kwenye natural resources before nchi nyingi kupata uhuru, zikiwa hazina wataalamu na wakajifunza pia mambo ubadilika baada ya uhuru na uelewa wa serikari katika hayo maswala.

Hiyo clause ilikuja kama kinga miaka ya 60’s kulinda mitaji yao na sasa imekuwa industry norm kwenye uwekezaji wa natural resources duniani kwamba sheria mpya zithiathiri mikataba iliyo live, that is not to say a country can’t negotiate new terms wakishtuka kwenye share of the profits kama wamepunjwa mno.

Lakini hakuna mkataba wa natural resources duniani usiokuwa na hiyo clause regardless of framework inayotumika. Ndio maana serikari imeshindwa kubadili na hata kwenye gesi itakuweko tu huo ni utaratibu unaoeleweka kimataifa na sehemu ya hiyo clause inaelezea wapi migogoro itasuluhishwa.

Issue ya share ni complicated kuelezea but basically wanachosema shares zetu ni protected na non diluting in any circumstances; za kwao zinaweza. Mfano wakitaka capital kupitia soko la hisa by way of issuing new share capital ni hizo 84% zao tu ndio zinahusika za serikari sio sehemu in other words change in equity of ordinary shares azihusiani na 16% za share za serikari.
 
Mhe. Zitto, una maana Lisu ameibuka kuwa Mzalendo namba moja!!!? Hawa wazalendo feki waliokuwa kwenye "Vita ya uchumi iliyo mbaya kuliko ile Vita nyingine" wametuingiza mkenge!!!? Hivi wanadhani Wazungu Ni shoga zao!!!? Ulipowaambia kuwa wanahangaishwa na "ushamba na ulimbukeni," hawakukuelewa. Sasa watakuwa wamejua kuwa hawana lolote zaidi ya kuwapigia "Mabeberu" magoti!!!?
 
Lusinde kibajaji, Msukuma, Mlinga, Nkamia, Kingwangala nk njooni huku tujadili hii ripoti huku huyu Zito analeta upotoshaji...
 
..halafu majitu haya ndiyo mchana kweupe yanatuma magaidi kwenda kumuua Tundu Lissu.

..Usd 300 million hata watulipe kila mwaka kwa miaka 600 bila riba bado hawawezi kumaliza deni la usd 190 billion tulilotangaziwa na Tume za Prof.Mruma na Prof.Ossoro.

Cc BAK, MTAZAMO
tume ilitengeneza professorial rubbish
 
..tuliaminishwa kwamba Tundu Lissu ni msaliti.

..na alipaswa kutangulizwa au kuuwawa.

..Je, kati ya waliosaini makubaliano haya na Tundu Lissu, yupi ni msaliti kwa nchi hii?

..aliyesaini makubaliano haya ni kibaraka wa mabeberu na barrick au ni mzalendo?

Cc Pascal Mayalla, Mag3

Kiini cha yote haya ni Rais Magufuli kutumia hisia kuaminisha watu makinikia yalikuwa na thamani zaidi ya ile inayosemwa na Acacia.

Wakaitwa maprofessa wasomi wakasema thamani halisi ni zaidi ya mara kumi na kuja na kodi ya $190bn. Dunia nzima ikatuona sisi ni wajinga.

Karibuni haya makinikia yataruhusiwa kusafirishwa. Swali la msingi kila mtu anapaswa kuhoji ni, Je, sasa makinikia yana thamani ipi? Ile ya Acacia au ya Maprofessa?

Ni rahisi sana kujua thamni ya makinikia na ukweli haujifichi. Wasijaribu kuficha!

Ukweli ni kwamba maprofessa wasomi walikosea au walidanganya. Tukisema tuwape benefit of the doubt kwamba walikosea basi wangetoka wazi na kukubali kosa. Hii ingelinda heshima ya maprofessa wetu. Lakini wapo kimya hawana hata aibu kwani ni wazi walidanganya.

Ripoti yao ya uongo hawajawahi kuitoa popote pale. Wakijua kwamba ni uongo, hawajawahi kwenda mahakamani kwa sababu si ushahidi.

Lissu was right to call their report professorial rubbish!

Sasa kwa sababu tayari walishaaminisha wananchi tunaibiwa wakalazimika ku-save face kwa kulazamisha chochote tu ili mradi yaishe. Aibu sana.
 
Back
Top Bottom