Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Dah tumeliwa sheria mpya ya madini ni redundant,
Nawashangaa wanaodhani magufuli ni mzalendo. Figisu zote zile kumbe walikuwa wanatafuta upenyo wa kupiga, inasikitisha inaumiza sana,
Mimi mkiandika hivi nasikitika na machozi yananitoka , yaani huwezi amaini watu wanateseka, wamepoteza kazi, kumbu mhujumu uvhumi kwa kiwango cha laana ndiyo bosi wao
 
MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019
hoja hukosolewa kwa hoja. haya praise team mjibuni zitto kwa hoja.
 
Kama mnadhani Zitto anadanganya, moja ya vipengele alivyoelezea hapo juu document inasema:-

Maelezo hayo yapo kwenye kipengele cha Dispute Resolution! Mnaona hapo ni namna gani endapo itatokea kushindwa ku-solve any dispute, basi issue itapelekwa mbele in accordance to UNCITRAL Conciliation Rules, na sisi, of course, citizens of arguing parties hawatakuwepo kwenye team!

Sasa kama tunatarajia huko mbele watu wata-resolve issues kwa kuzitangatia maslahi yetu basi tuna safari ndefu!

Kuhusu 16% ya shares zetu kuwa Class B Shares, makubaliano yanasema:-Haki za Class A and Class B Shareholders zimeelezewa kwenye Shareholders Agreement, lakini Zitto aliposema kwamba hizo shares zetu huwezi kuziweka hata kuwa dhamana ni kutokana na kipengele kinachosema:- Suala la kwamba lile sharti la Tanzania kumiliki 30% akina Kabudi na Magu wameliuza kwa Wazungu, makubaliano yanasema:- Kwahiyo hiyo 16% itaendelea kubaki hivyo hivyo! Vipi kuhusu suala la kusafirisha madini nje? Makubaliano haya hapa:-Kumbe wanayo unfettered rights ya kusafisrisha madini na makinikia nje ya nchi hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kufanya refining and smelting ndani ya nchi!

Kama ndivyo, kwanini basi tusiwalazimishe hawa Barrick wajenge mtambo wa kuchenjua makinikia hapa hapa Bongo ili wasiendelee kutupiga changa kwa kusafirisha makinikia nje ya nchi?! Makubaliano yanatoa jibu kwa hilo swali, kwamba:-Kwahiyo ndugu yangu french badala ya kukejeli kwamba watu wa humu ni wavivu wa kufikiri, ungefanya maarifa kwanza kuisoma hiyo doc! Sio lazima Zitto akuletee kwa sababu ipo kwenye website ya Acacia lakini ni ndefu, ina 91 pages!

Mkuu Bome-e, maelezo ya sehemu ya ripoti ni hayo hapo juu, na kisha ayaone Mkuu Tangawizi aliyehoji kwenye uzi mmoja kwanini naamini Barrick ndie wameshinda bila kumsahau ruaharuaha!!
This country is fucked, i say fucked baasi namuachia mungu tuu
 
Kiini cha yote haya ni Rais Magufuli kutumia hisia kuaminisha watu makinikia yalikuwa na thamani zaidi ya ile inayosemwa na Acacia.

Wakaitwa maprofessa wasomi wakasema thamani halisi ni zaidi ya mara kumi na kuja na kodi ya $190bn. Dunia nzima ikatuona sisi ni wajinga.

Karibuni haya makinikia yataruhusiwa kusafirishwa. Swali la msingi kila mtu anapaswa kuhoji ni, Je, sasa makinikia yana thamani ipi? Ile ya Acacia au ya Maprofessa?

Ni rahisi sana kujua thamni ya makinikia na ukweli haujifichi. Wasijaribu kuficha!

Ukweli ni kwamba maprofessa wasomi walikosea au walidanganya. Tukisema tuwape benefit of the doubt kwamba walikosea basi wangetoka wazi na kukubali kosa. Hii ingelinda heshima ya maprofessa wetu. Lakini wapo kimya hawana hata aibu kwani ni wazi walidanganya.

Ripoti yao ya uongo hawajawahi kuitoa popote pale. Wakijua kwamba ni uongo, hawajawahi kwenda mahakamani kwa sababu si ushahidi.

Lissu was right to call their report professorial rubbish!

Sasa kwa sababu tayari walishaaminisha wananchi tunaibiwa wakalazimika ku-save face kwa kulazamisha chochote tu ili mradi yaishe. Aibu sana.
Wale maprofesa ni wapuuzi kabisa. Na report zao zilikuwa za ujinga mkubwa. Kila aliye mtaalamu kwenye sekta hii aliona zile report ni wendawazimu mkubwa. Ni sawa mtu akuambie kuwa ekari moja ya zao la mahindi imekuwa inazalisha magunia milioni 1 yenye thamani ya trillion 100. Kila mwenye akili atakuona uliyeyasema hayo ni mwendawazimu.
 
Leta tag
Zitto ametafsiri alichokisoma kwa namna livyoona yeye japo sivyo ilivyo katika uhalisia wake. Msioelewa Kiingereza na/au misamiati/lugha ya uwekezaji katika tasnia ya uziduaji mtachotwa sana na hekaya hizi za akina Zitto.
Leta tafsiri yako, ama ujibu hoja zilizoko mezani. Acha ngonjera.
 
Tuna mwendawazimu anayependa kukurupuka kwa kuwa anajiona yeye ni mungu kila alitakalo huwa vile atakavyo. Janga kubwa la Taifa huyo nduli.
Pascal Mayalla kuya huku
Leo Ni Leo
Pascal nimejitahidi sana kumwambia Barricks na Acacia ni ndugu moja
Kwa ufupi Acacia ameshinda
Shida ya hawa mambumbumbu wanajiona wamewin in other words nchi imeuzwa mchana kweupeeee
Acacia na Barrick wako hivi cheeers 🍺🍸🍾
WaTz wako hivi🙆‍♀️😭😇
 
The professorial rubbish zimeanza kujibu, usifanye mchezo na mabeberu hata ukitoa mimacho kama wa jalalani.Kalamaganda Kabugi hana practical uzoefu wa mikataba ya madini. Yeye alidhani seminar za first year LLB on Family Law. ASEME SASA WAJANJA WA BARRICK WAMEMLA KICHWA PROFESA WA JALALANI
 
Ngoja tuone... Pascal Mayalla pitia hapa...

Cc: mahondaw
@Pascal Mayalla ni muoga sana siku hizi.
hoja za zitto atazipangua kwa style ya kung'ata na kupuliza.

yaani 90% ya atakacho kiandika kitakuwa ni porojo za kusifia utawala wa jiwe na kukosoa hoja za zitto, halafu 10% ya atakacho andika ndio itakuwa halisi ya sakata la serikali+ barrick + acacia.
 
MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019
Kazi tunayo awamu ya bongo movie...
Hawatasaza hata "mafupa!!"
 
“Kwa nchi nyingine hili lingetosha kabisa kuiondoa serikali madarakani”

Na Of course ni kweli kabisa, kama tungekuwa ni taifa la watu wafuatiliaji,waelevu,wenye uchungu na nchi yao na waojua kudai haki zao pasipo kuogopa naamini kabisa mpaka muda huu ninavyoandika hapa John angekuwa tayari ni our EX-president kwa hili na mengine mengi tu ambayo amewahi kuyafanya hivyo tungeunganisha tu na kupata sababu yenye nguvu.

Huu ni zaidi ya uhaini kwa maana ni kuliuza taifa kwa minajiri ya kutafuta sifa za kijinga zisizokuwa na maana wala faida yoyote kwenye maisha ya watanzania.

Yote haya ni kwasababu ya kichwa kimoja kujiona ndio kinaweza kuamua kila kitu hata kwenye mambo kisichokuwa na utaalamu nacho.

Hili battle tangu awali lilionekana ni ngumu kushinda kutokana na approach mbovu tuliyoitumia. Zile recommendations za akina Prof. Osoro yalikuwa ni matakwa ya Magu na hata wao wenyewe walijua ugumu wake ila walitekeleza maagizo tu.

Mpaka Accacia inafikia makubaliano na Barrick tayari walikuwa wameshaona loopholes kwenye sheria zetu mbovu za madini na udhaifu wa negotiators waliochaguliwa kwenda Canada.

Hili suala kwa huu mwisho wake ni fedheha kubwa na aibu, ndugu Mh.ZZk fanya kupeleka hili bungeni kama hoja binafsi na lijadiliwe hili kila mtu afahamu ukweli kuwa tumepigwa na sio kuimba nyimbo za mapambio.
 
@Pascal Mayalla ni muoga sana siku hizi.
hoja za zitto atazipangua kwa style ya kung'ata na kupuliza.

yaani 90% ya atakacho kiandika kitakuwa ni porojo za kusifia utawala wa jiwe na kukosoa hoja za zitto, halafu 10% ya atakacho andika ndio itakuwa halisi ya sakata la serikali+ barrick + acacia.
Akipita hapa atakutupia "like" mambo yaishe...
 
Mkubwa, mimi nadhani ili tuanze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo sharti la kwanza kabisa ni kuviondoa na kuvifuta kabisa vyama hivi vya kisiasa vilivyopigania Uhuru....

Mimi naamini tatizo liko hapo kwa sababu kwa jinsi mambo yalivyo hata umlete nani kuwa kiongozi chini ya mifumo ya vyama hivi kuongoza taifa letu......

Nakuambia atakuja na nguvu za gesi ya soda ya Coca Cola mwisho anauvaa mfumo huu wa kihayawani, naye anakuwa walewale na kulainika kama mkate kwenye chai ya maziwa......

Tena huyu (John Pombe) pamoja na kulazimisha asifiwe hata na mawe nadhani ndiye atakuwa the worst ever president taifa la Tanzania kuwahi kuwa naye....!!

Kwa hili alilolileta Zitto Kabwe, kama ni kweli hata kwa 10%, basi linathibitisha haya niyasemayo....

Kwa sababu haiwezekani kwa mihemko tu Rais wa nchi bila hats kujipa muda was kutafakari mambo ktk engo zote unaamka na kuja na National and International Televised speech dhidi ya watu wa nchi yako na dunia kwa ujumla kuwa umekamata investor mwizi ktk sekta ya madini ktk nchi yako wa $190bn, ukafunga shughuli zake, na kuwaaminisha watu kuwa tutalipwa......!!

Lakini eti, mwisho wa siku mnaishia kuingia makubaliano ya kipuuzi na kishenzi kama haya na badala ya yeye kuilipa nchi, nchi ndiyo inamlipa MTU kama huyu ulichokuwa unakidai na at same time unampa na migodi ya madini yote!!

I predict kuwa huyu bwana ndiye Rais atakayeingia kwenye rekodi ya marais wezi na matajiri kuliko wote. kuwahi kutokea tangu uhuru.....!!

Hakuna namna nyingine unayoweza kuitafsiri hii situation iwapo tu kilicholetwa hapa na mbunge huyu ni KWELI na HAKIKA...

Naamini huu kamwe hauwezi kuwa ni uzushi kwa sbb kama haya makubaliano yamewekwa wazi huko kwenye masoko ya hisa UK na NYSE, basi maana yake ishu hii ni hakika na ni ukweli mtupu na kuwa ndivyo ilivyo!!
Mi naomba account za Bwana yule zichunguzwe na kuwekwa hadharani ili tujue iwapo hazijanoneshwa na Barrick. Si Chief Mangungo alipewa shanga na kioo!!!
 
Ziko tuhuma nyingi tulizo wahi kuaminishwa dhidi ya serekali hii ambazo mwisho wa siku zinakuwa hazina mashiko. Hii nayo itapita kama zilivyo pita nyingine. Niwaulize enyi watetezi wa mafisadi/vinana mmesha isikia serikali upande wake kutolea hili suala maelezo kabla ya kuhitimisha haya mnayo ya tuhumu.

Picha inayojengwa na majizi yenye hasira kwa kukatiwa njia zao za wizi ni kwamba iko namna kama wao walivyokuwa wanafanya huko nyuma katika ufisadi wao. Subirini kwani serikali itatolea ufafanuzi maana serikali ya JPM haija wahi/haitowezekana kujificha katika kivuli cha usiri wa mikataba. Huko kipindi cha nyuma kilicho kuwa cha mafisadi/vinana ndio mbinu hii ya wizi kwa usiri wa mikataba ilitumika.

Serikali ya awamu ya 5 imejipambanua kuwa yenyewe inasimamia maslahi ya nchi kwa niaba ya Watanzania walioipa ridhaa kuwa ongoza ikipigania manufaa yao kwa mikataba ya win-win conditions na hata huu mwisho wa siku tutaliona hili tutakaposikia maelezo ya serikali.

Hii ni hoja dhaifu kutaka watu wanaoji elewa kama wa hapa Jf wafikirie timu ya majaliano haikujua kwamba makubaliano waliyo ya fikia na kusaini yangeliwekwa wazi katika asoko ya hisa.
 
North Mara
hapa mgodi kinu kimefungwa
sababu ni
1. Mazingira
kuna bwawa la maji machafu (TSF)
2. Mgogoro wa Barrick na Acacia
Ila pia General Manager
alikimbia more than two months amekatalia South Africa

Kuna mjaruo mmoja ndiye ana-Act
sasa na hizi taarifa za Zito
Duh hapa njia panda!

coz hapa North Mara Nyamongo
ndiyo tunashuhudia huu mziki

Dhahabu hakuna kutoka zaidi ya Wiki sasa!

kwamba huu wote ni mkwara?
Kiini macho?
maigizo?
Mmh nadhani hadi Jumatatu ndiyo itaeleweka rasmi!

wacha tusubirie
Serikali inaweza nayo kuja na hoja

askari ndiyo wanalinda huku
Wanajeshi pia wapo huku

Acacia wenyewe hawaamini huu mziki hapa wamekimbia tangu Asubuhi

Yaani maswali ni mengi kuliko majibu sasa
But
Offices zao ziwe Mwanza na Dsm
 
Back
Top Bottom