Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Profesa Kabudi naomba uje ututafsirie Kipengele 10 (c) mpaka (d)

10 (c)(i). Kwa nini Barrick hawatalazimika kuuza share zao kwa Umma (public) kinyume cha sheria za nchi?
10(c) (ii) Kwa nini Barrick hawatalazimika kujenga kinu cha kuchenjulia dhahabu hapa nchini?
10(d) Serikali itaondoa zuio la makinikia kuondoka nchini, kama tulikuwa tunapigwa kwenye makinikia kwa nini kwanza tusilipwe zile Dola bilion 190 tulizokuwa tunadai?.

Mheshimiwa Kabudi kwenye ripoti ya Mruma iligundua kuwa kwenye Makinikia kuna madini mengine mengi zaidi ya dhahabu hayo je tunayapataje?

dhahabu zetu.png
 
Toka mwanzo nilijua kuwa kwa makosa waliyoyafanya awamu hii, ili kuwarudisha wawekezaji, ni lazima serikali italazimika kuleta vivutio kwa wawekezaji vingi kuliko tawala zilizopita.

Katika masuala ya madini, kwa ujumla, mara nyingi nimesema ni serikali iliyopoteza. Barrick hawajawahi kupata hasara tangu kampuni ianze kutokana na umakini wa watu wao. Falsafa ya Barrick inasema, 'Every best person must work with Barrick'. Kabudi na nadharia zake za darasani, kamwe asingeweza kuwashinda Barrick. Kuna wakati nilisema kuwa hasara aliyoileta Kabudi kwenye sekta ya madini, haipimiki. Kuielezea inahitaji topic inayojitegemea.
Acha kukwepesha maneno. Aliyeleta hasara katika hili ni Rais Magufuli. Kabudi ni bomba tu la kupitishia matakwa ya Magufuli. Hata kwenye korosho, hali ni hiyo hiyo!!!
 
Unajidanganya. Serikali iliyo tayari kuua au kupoteza raia wake ili
mradi mambo yake yasjulikane, unawezaje kusema imejipambanua kulinda rasilimali!!!? This is the worst government ever to exist in this country!!!


Unafikiri kuongoza nchi ni kama vile kufundisha darasa la shule ya vidudu wewe.
 
Mpinzani wa kupinga. Yeye (Zito) awamu ya nne ndiye alikuwa mstari wa mbele kusema kuwa kinana ni mwizi mkuu wa rasilimali za taifa. Kuwa ni jangiri maarufu wa meno ya tembo. Ajabu hivi sasa yeye ndiye mtetezi mkubwa wa Kinana. Hivi huyu binadamu ni binadamu wa aina gani?
Rudi ndani ya mada, pamoja na hilo ukitaka kuwashughulikia watu kuwa straight acha kupita pembeni nafuata utaratibu...
 
Asante sana ndugu Zitto kwa kutufunua macho.
Kilichobaki ni jukumu letu sisi wa Tanzania wenye uchungu na nchi yetu na wala sio wale wanaosema wanatetea wange.

Mungu ataendelea kuwalinda wote mnaotetea raslimali za nchi hizi kwa ukweli bila ya kua na malengo nyuma ya pazia.
Viva Zitto viva Lissu!
Mangungo hatumtaki arudi kwao!
Kweli Mungu awalinde, "Tunaibiwa kwenye Sheria" Mh Tundu Lissu Mungu akupiganie
 
Jamaa anataka kututoa nje ya mstari maana leo rafiki(mzee wa Bumbuli mdogo) clip yake ina trend sana.


Wako watu wenye kuwaona wenzao mabogus kwelikweli, ukitafakari ile zawadi mama mtu aliyo pendekeza huyo chambo wa familia yao atunikiwe.
 
Wamefanya siri wapi? Sheria yenyewe inakataa usiri how possible upande mmoja wafanye siri wakati ni makubalano ya pande mbili. Mbona mnachanganyikiwa mapema hivi zikiwa ni mvua tu za rasharasha bado masika yenyewe kuwanyea kisawasawa.
Tuwekee taarifa ya serikali hapa kuhusu makubaliano yaliyofikiwa!
 
Taifa linaongozwa na genge la majangili, washamba, watu waliochanganyikiwa, short minded!
 
Eti huu ndio utawala unaopanda mradi wa Bagamoyo kwa hoja kuwa ni wa kifisadi!!

Sasa haya makubaliano yana tofauti gani na ya mradi wa kujenga bandari ya Bagamayo?

Kwanini tusihisi mmevunja ule mkataba ili na nyinyi mpate nafasi ya kuingia mkataba mwingine wa kifisadi kama huu mlioingia na kampuni ya Barrick?

Kwa makubaliano haya,hii serikali haipaswi kuaminiwa kabisa!!!!
 
Goli aliyefunga Pascal Mayalla limerudishwa dk ya 87, naona upande wa pili wanapata Penalt ! kila mtu anaomba kipa wetu aucheze huo mpira usijae nyavuni wakati huo huo mchezaji wetu tegemezi nae anagaagaa kwa maumivu makali huenda akatolewa nafasi yake kuchukuliwa na mwingine!!
 
Back
Top Bottom