Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Kwa mikataba ya namna hii ni wazi kabisa hii inchi haitakuja kuendelea chini ya uongozi wa CCM. Maana kila siku mikataba yenye tija imekuwa haileti manufaa kwa taifa. Huu uchambuzi wa kina umetuhuzunisha sana watanzania maana ni kinyume na matarajio ya wengi.
 
Mkuu siyo wajinga wote bali wale tulio wapatia nafasi ya kutuwakilisha huko ndiyo waliyo tuuza either kwa kupewa kitu kidogo au kwa kutokufit hiyo nafasi
Ƙama mmegawa rasilimali kwa mabeberu na mnaficha miƙataba mtakuwa watu gani tofauti na kuwa wajinga!
 
Mbona unashindwa kumuhoji the same question yule chumia tumbo Pascally Mayalla ?
Sasa zito angejuwaje haya wakati majadiliano yalikuwa siri kati ya jiwe kabudi na barric yaani kuna watu sijui kwa nini bado wapo hapa kwenye jukwaa zito kajua baada ya barric kuanika mambo LSE Na NSE
 
Wabunge wenyewe kama ni akina Kibajaji basi tutaendelea kuumia tu
 
Kuna walioomba link ya press release ya Barrick pamoja na kwamba inapatikana kirahisi tu na pengine Pasco alishaiweka humu kwenye uzi wake jana. Ni kwamba wenzetu Mlikuwa mnafikiri Pasco anapata wapi taarifa zote za sakata hili kina anapozileta humu jukwaani?

Baada ya kujua pa kuipata hiyo document, mtaisoma kweli? Mtaisoma mtaielewa kwa mwanzo huu mlionyesha?

Ukiachana na hayo, hisa za acacia isiyosajiliwa Tanzania zimeendelea kuwepo sokoni DSE (jana tu zimekuwa top performer) ukiachilia mbali LSE.
 
Haya ni sawa na yale maelezo yao ya kusema hela za escrow account zilikuwa za serikari sijui CAG kasema na nani, ivyo Rugemalila achukuliwe hatua.

Wakati ulikuwa uongo mtupu wa kuwalaghai watanzania; yes kulikuwa na ujanja kwa upande wa Rugemalila lakini wa halali kisheria, miaka mitatu mzee wa watu amewekwa jela huo ushahidi wa zile ni hela za serikari mpaka leo amna na kesi ya kutakatisha pesa ushahidi amna.

Kilichobaki ni kuficha aibu tu baada ya kumfanya mzee wa watu scapegoat kwa kumuacha huko huko jela.

Ndio kama andiko hili upuuzi mtupu sijui unaanzia wapi maana kwenye kichwa chake wawekezaji watakwenda tu nchi hata ambazo sio wanachama wa international trade agreement.

Kuna maswala ya frameworks za hii mikataba na aina zake mfano PSA, Joint Venture, Concession/lecence agreement or Risk services; wetu upi hili uweze jadili sahihi?

Kuna key negotiations issues ambazo kama technicalities za geogology data, commercial ya migodi kama life time, policy stability, economic issues to name a few; uta discuss vipi bila ya kupitia hizo data kwanza?

Halafu finance za mashirika zina utaratibu watu awatoi share tu mpya hilo linaendena na changes in equity ya share holders na ni complicated business kufanya ivyo, hilo si kosa lake ata serikari huwa aifikirii implications za kulazimisha kuuza share kwa makampuni yaliyo sajiliwa nje ya nchi.

In short for the most part ni pumba tupu.
 
Hapa ulikuwa unataka kuongelea kitu gani?
 
Zitto tuwekee hiyo document au tupe linki tukasome wenyewe!
Akiweka nitag mkuu. Watu humu ndani ni wavivu sana wa kufikiri. Zitto alete hiyo link aliosoma yeye ili na sisi tujiridhishe
Kama mnadhani Zitto anadanganya, moja ya vipengele alivyoelezea hapo juu document inasema:-
Maelezo hayo yapo kwenye kipengele cha Dispute Resolution! Mnaona hapo ni namna gani endapo itatokea kushindwa ku-solve any dispute, basi issue itapelekwa mbele in accordance to UNCITRAL Conciliation Rules, na sisi, of course, citizens of arguing parties hawatakuwepo kwenye team!

Sasa kama tunatarajia huko mbele watu wata-resolve issues kwa kuzitangatia maslahi yetu basi tuna safari ndefu!

Kuhusu 16% ya shares zetu kuwa Class B Shares, makubaliano yanasema:-
New OpCo will be owned 84%/16% by a subsidiary of the Acacia Group and a nominee of the GoT respectively. Acacia will hold its shares in New OpCo as Class A shares and the GoT will hold by way of Class B shares.
Haki za Class A and Class B Shareholders zimeelezewa kwenye Shareholders Agreement, lakini Zitto aliposema kwamba hizo shares zetu huwezi kuziweka hata kuwa dhamana ni kutokana na kipengele kinachosema:- Suala la kwamba lile sharti la Tanzania kumiliki 30% akina Kabudi na Magu wameliuza kwa Wazungu, makubaliano yanasema:-
the GoT will not unilaterally seek to increase its share ownership or economic participation rights in the TMCs;
Kwahiyo hiyo 16% itaendelea kubaki hivyo hivyo! Vipi kuhusu suala la kusafirisha madini nje? Makubaliano haya hapa:- Kumbe wanayo unfettered rights ya kusafisrisha madini na makinikia nje ya nchi hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kufanya refining and smelting ndani ya nchi!

Kama ndivyo, kwanini basi tusiwalazimishe hawa Barrick wajenge mtambo wa kuchenjua makinikia hapa hapa Bongo ili wasiendelee kutupiga changa kwa kusafirisha makinikia nje ya nchi?! Makubaliano yanatoa jibu kwa hilo swali, kwamba:-
there will be no obligation on the TMCs to construct beneficiation facilities in country;
Kwahiyo ndugu yangu french badala ya kukejeli kwamba watu wa humu ni wavivu wa kufikiri, ungefanya maarifa kwanza kuisoma hiyo doc! Sio lazima Zitto akuletee kwa sababu ipo kwenye website ya Acacia lakini ni ndefu, ina 91 pages!

Mkuu Bome-e, maelezo ya sehemu ya ripoti ni hayo hapo juu, na kisha ayaone Mkuu Tangawizi aliyehoji kwenye uzi mmoja kwanini naamini Barrick ndie wameshinda bila kumsahau ruaharuaha!!
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza sana ni kwanini Barrick walikuwa wanafukuzia hili swala la kununua Acacia kwa haraka sana. Kumbe kulikuwa na kitu nyuma yake. Pia ni kwanini wasomi wetu wanakuwa butu sana wakati wa kufikia makubaliano? Tatizo ni Lugha ama tatizo ni uelewa wa Mambo wanayozungumzia ama wanapewa Rushwa kutusaliti wanannchi?
 

Duh ebwanaee
Sasa hapo mwanzo tulizuia makinikia ya nini na leo tumefanya nini?
Si tuliambiwa kwenye makinikia ndipo tunapopigwa?
Sasa mbona wazungu wataendelea kukomba tu?

Naona Kabudi na Bosi wake wametafuta namna ya kujikosha kutoka kwenye mess waliyoitengeneza!
Walipitisha sheria bungeni haraka haraka kuwa kesi za madini zitakuwa humuhumu nchini lakini wametoka hapo wameweka waiver maana yake itabidi wakabadiishe ile sheria ya madini?

Kama tulikuwa tumeibiwa DOLA BILIONI 190, JE HIZO TUNAZIPATAJE, NA KAMA TUNASAMEHE KWA NINI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…