Zitto: Mazingira ya Siasa ni Magumu, Sarakasi za Msajili na CHADEMA hazina Afya, Kuna Ukandamizwaji

Zitto: Mazingira ya Siasa ni Magumu, Sarakasi za Msajili na CHADEMA hazina Afya, Kuna Ukandamizwaji

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akifanya Mahojiano na Clouds Media leo Mei 28, 2026

"Inaonekana wazi kwamba mazingira yetu sasa hivi ya watu ambao bado wako active kwenye siasa mazingira ya siasa ni magumu. Mnaona sarakasi za msajili na na chama cha Chadema ambazo hazina afya kwa sababu mmetoka kwenye kwenye jambo baya sana kupata kutokea katika historia ya nchi yetu la Oktoba 29.

Mmeenda kwenye ripoti, moja ya taasisi ambayo CHADEMA imeilaumu sana ni ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa mambo ambayo iliyafanya wakati wa uchaguzi, kwa mfano sisi mgombea wetu wa urais alizuiliwa kwa kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa. Alafu watu wameenda mahakamani, mahakama imewapa uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa ghafla wameanza msajili anaandika barua mjeleze kwa nini msisifuatiwe, yaani unaona kabisa kwamba wanarudia yale yale ambayo yalipelekea ile hali ambayo tulikuwa nayo mwaka 2000, October, yaliyopelekea Oktoba 29."


 
Back
Top Bottom