Uchaguzi 2020 Zitto ni kati ya viongozi wanaotakiwa kubebeshwa lawama, kuzomewa na kupuuzwa kutokana na hotuba zake zilizotaka kuvuruga amani wakati wa kampeni

omegas

Senior Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
111
Reaction score
137
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

MWANASIASA Mkongwe Zanzibar, Baraka Mohamed Shamte, amemtaka kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe, kabla ya kudai kumefanyika maonevu na unyanyasaji, kwanza aileze dunia kiongozi gani wa chama chake aliyewaamrisha wafuasi wake kubeba silaha za jadi na kujiweka tayari kwa mapambano.

Pia amemtaja Zitto ni kati ya viongozi wanaotakiwa kubebeshwa lawama, kuzomewa na kupuuzwa kutokana na hotuba zake zilizotaka kuvuruga amani wakati wa kampeni.

Baraka Shamte, alitoa matamshi hayo jana kisiwani Unguja, kufuatia madai ya Zitto aliyesema kuna watu huko Pemba wameuawa ,kuteswa ,kupigwa na kuumizwa wakati hakuna ushahidi wa matukio hayo na hadi sasa vyombo vya dola havijathibitisha.

Pia alimtaka Zitto asidhani hakuna ushahidi wa matamshi yake alioyatoa kwenye majukwaa ya kisiasa yaliowataka wafuasi wake kuingia mitaani kinyume na sheria ,kuandamana na kupinga matokeo ya Uchaguzi ikiwa chama chake hakitashinda.

“Zitto asicheze ngoma ya wachawi na wanga .Ikiwa anataka kuimba nyimbo za wanga aende ging’ingi akacheze kuliko kuimba mitaani .Asikubali kulishwa uongo na uzushi mdomoni mwake. Maneno yake yenye viashiria vya jinai yapo na iko siku yatawasuta” Alisema Shamte.

Mwanasiasa huyo, alisema Zitto asifikiri wanaoshitakiwa kwenye mahakama za kimataifa ni watawala peke yao badala yake ajue hata viongozi wa upinzani hukabiliwa na mashitaka ikiwa kuna ushahidi au matamshi yaliolenga kuvuruga amani na umoja.

“Mwenyeliti wake Maalim Seif ndiye aliyewataka vijana ACT Wazalendo kubeba mundu, mikuki, mawe, mashoka na mapanga. Akawahimiza wakusanyike kwenye barabara kuu za Michenzani, kuandamana na kupambana na polisi hadi wapewe ushindi ” Alisema.

Aidha kabla ya kutamka maneno hayo, akiwa ziarani kisiwani Pemba mwanzoni mwa mwaka huu ,alisikika akisema wazi wazi mwaka huu liwalo naliwe , kama noma naiwe noma na ikitokea mtu kupigwa au kujeruhiwa asiende polisi badala yake wajibu mapigo.

Shamte alisema Maalim Seif ndiye aliyewaimbisha vijana wa ACT Wazalendo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibandamaiti huku wakimuitikia hawaogopi lakini pia ndiye aliyepania kutaka kuvuruga uchaguzi kwa kuwataka wanachama wake wajitokeze kupiga kura Oktoba 27 kinyume na sheria.

Alisema zitto anapowaomba marais wastaafu kina Joachim Chisamo,Thabo Mbeki na Ulusegun Obasanjo waje zanzibar au Tanzania huku ni kuwazubaisha na kuwapa matumaini yasiokuwepo wafuasi wao baada ya kushindwa vibaya ikiwemo na yeye kupoteza kiti cha ubunge cha Kigoma mjini.

“Kwanza Zitto ayakumbuke alioyasema kwenye majukwa . Yeye na wenzake ndio waliotaka mapema zitokee vurugu . Asidhani wanaoshitakiwa ni watawala tu bali hata upinzani unapovunja sheria hubeba msalaba wa tuhuma zote zitakazothibitika “Alisisitiza Shamte .

Vile vile alisema hata wakati akitaja idadi ya watu anaodai kujeruhiwa huko pemba kwa kusema kwake uongo alikataa kuwataja watu waliopigwa mapanga msikitini jambo ambalo linathibitisha taarifa ya Zitto ilijaa usanii wa kisiasa anaofundishwa na Maalim Seif.
 
Zanzibar ninyi ni wapumbavu sana,mnakubalije kila mwaka wa uchaguzi mnaletewa askari kutoka bara wanakuja kuua ndugu zenu?Mna akili kweli?Kwanini mfe ninyi tu kila uchaguzi?Shwain,haoafu unakuja na bandiko la kipuuzi,jinga kabisa!
 
Zanzibar ninyi ni wapumbav sana,mnakubalije kila mwaka wa uchaguzi mnaletewa askari kutoka bara wanakuja kuua ndugu zenu?Mna akili kweli?Kwanini mfe ninyi tu kila uchaguzi?Shwain,haoafu unakuja na bandiko la kipuuzi,jinga kabisa!
[emoji23][emoji23][emoji23]Mbona wewe mwenyewe uko hapa kila siku unalalama tu kuibiwa na huchukui hatua yeyote na ndio kwanza mgombea wako kakimbia?

Si bora wazenji wanakufa, ukiona hadi wamekufa ujue wakijaribu kupambana!

Sasa nyie hapa mmeambiwa andamaneni mkajificha twitter na jf!

Wengine ndio hao wamekimbilia Kenya kisa eti vitisho tu vya kwenye simu?

Kamwe usijifananishe na wazenji wale ni watu na nusu! Siyo nyie manyumbu ya hapo ufipa.
 

Ati
 
Mimi siwezi kuandamana na wala sitakuja kuandamana kwa jambo lolote!Mimi ni kati ya wale tulioandamana UDSM 2011 kutaka boom litoke 5000 mpaka 7500 kwa siku enzi za JK!

Tulifanikiwa ila almanusura nikose chuo maana kuna masnitch walikuwa wanajifanya kuandamana kumbe walikuwa wanachukua video na picha za waandamanaji!

Nilijieleza masaa mawili mbele ya displinary council,bahati nzuri nilikuwa na mtu upande wangu akanikingia kifua!Tokea hapo niliapa kutojihusisha na maandamano ya aina yoyote!

Mimi naupenda upinzani na nitaendelea kuikosoa serikali hii ya awamu ya 5 mpaka inatoka madarakani!Ungejua nafasi niliyopo ungeshangaa kwanini naunga mkono upinzani!

So relax,no hard feelings na maisha yanaendelea!
 
Umeandika Vizuri Sana ila sidhani huyo Mburura aliyeanzisha bandika atakuelewa...Bado Wajinga na Washenzi ni Wengi katika Taifa hilo so tunayo safari ndefu.
 
Zanzibar ninyi ni wapumbavu sana,mnakubalije kila mwaka wa uchaguzi mnaletewa askari kutoka bara wanakuja kuua ndugu zenu?Mna akili kweli?Kwanini mfe ninyi tu kila uchaguzi?Shwain,haoafu unakuja na bandiko la kipuuzi,jinga kabisa!
Wewe ni mpumavu zaidi ya hao wazanzibari, nyie hapa mnawategemea wazungu na akina Amsterdam kwa kutumia ujinga upi?
Ebu eleza hapa hao mnataka wawasaidie kwa lipi ili muingie madarakani?

Kwa hiyo wao ndo watakuwa wanawaendeshea serikari yenu hao akina Amsterdam?
Jibu hapa uache kiherehere.
 
Hayo ni ya kwako sio ya kwangu! Mimi nimezungumzia tabia ya wazanzibar kuuwawa kila uchaguzi!
 
Zanzibar ni wapumbavu tu, msipoamka mtaendelea kuwa koloni la Tanganyika.

Huyo mwandishi wenu yeye ni mpuuzi aliyechangamka.
 
Ni kweli wakati umefika kwa hawa wapuuzi kina Zitto na Lissu kupuuzwa. Lissu alitaka watu waandamane mitaani cha kushangaza yeye kakimbilia Ubelgiji kwa mabwana zake huku akiacha waandamanaji mtaani wakisubiri kukamatwa.
 
Ni kweli wakati umefika kwa hawa wapuuzi kina Zitto na Lissu kupuuzwa. Lissu alitaka watu waandamane mitaani cha kushangaza yeye kakimbilia Ubelgiji kwa mabwana zake huku akiacha waandamanaji mtaani wakisubiri kukamatwa.
Uwezo wako wa kufikiri ndio imeishia hapo?
 
Ni kweli wakati umefika kwa hawa wapuuzi kina Zitto na Lissu kupuuzwa. Lissu alitaka watu waandamane mitaani cha kushangaza yeye kakimbilia Ubelgiji kwa mabwana zake huku akiacha waandamanaji mtaani wakisubiri kukamatwa.
We ni mpuuzi zaidi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…