Zitto sawa wahudumu walifungua mlango, je waliwapa abiria wao maboya?

Halafu wahudumu hao wawe mashujaa
 
Mkuu ni propogada ili zimunufaishe nani?
 
Ukiingia kwenye ndege una elekezwa ilipo vifaa vya kujiokoa na jinsi ya kuvaa.
Mhudumu mmoja ana wezaje kuwagaeia abiria wote na viko chini ya kiti chako?
 
Maana yake yale maelekezo kabla ya kupaa hayakufanyiwa kazi
 

Hii hoja imekaa kishamba kishamba sana.
Sio kazi ya wahudumu kukuoatia abiria maboya bali ni jukumu la wahudumu kuelekeza maboya yaliko kwa kila abiria na namna ya kuyatumia inapotokea dharura kama ile.

Maboya hiwekwa chini ya kila siti hivyo kila abiria huelekezwa yalipo.

Si kazi ya wahudumu kugawa maboya tuache uboya
 
Sidhani kama ulishawahi kupanda ndege
Wewe ndiye unatia aibu alivyosema jamaa ni sahihi.
Kabla ndege haijaruka lazima wahudumu watoe maelekezo ya kujiokoa na kuelekeza maboya yalipo
 
Achana na Zitto na mipango yake🤣🤣🤣🤣
 
Wewe ndiye unatia aibu alivyosema jamaa ni sahihi.
Kabla ndege haijaruka lazima wahudumu watoe maelekezo ya kujiokoa na kuelekeza maboya yalipo
Mkuu ni sawa lakini nani huwa anafatilia? Taarifa inasema ndege ilihangaika kutua kwa karibu dakika 20- hao wahudumu na abira walifanya nini- huo mda ulitisha kumpa kila mtu boya- wazembe tuko wengi ila mnapotaka kuilaaumu serikali na kuwaacha wazembe wengine- hapo ndipo naona siyo sawa hata kidogo
 
Mimi mshamba niko nakula ugali wangu leo- wajanja mbona hawakuchukua maboya ambayo kumbe yalikuwa nchini ya viti walivyokalia. Wahudumu mnaowaona bora kuliko mvuvi Majaliwa waliwafungiliaje abiria mlango na kuwaingiza ziwani bila kuchukua tahadhari? Kama hao wajanja kama wewe walitoka na maboya walishindwaje kujiokoa sasa- maana ukiwa na boya wewe kilichobaki kukutisha ni mamba au kiboko vinginevyo uko salama- kwa ufupi wewe ni mshamba zaidi kuliko mimi
 

Ni kweli huwa hatujali lkn sio kosa la wahudumu.
Katika hili labda tumlaumu rubani hakuwa mkweli kwa abiria akiogopa kuleta taharuki.
Kama alifahamu atatua ziwani alipaswa atoe tahadhari na kusisitiza maboya na utulivu.
Kitendo cha kutokuwa muwazi kwangu mimi naona amekwepa majukumu yake.

Mkiwa angani hali ya hewa ikiwa mbaya lazima mtangaziwe.
Mimi niliwahi kukutana na kipindi kigumu sana hewani kulikuwa na mvua kubwa sana na upepo mkali ulioisukasuka Dreamliner lakini rubani alitupa yahadhari kila wakati bila kujali taharuki.
 
Mkuu sasa ni kosa la marehemu wale 19? au hawa waliopona 26? au waliokuwa katika shughuli zao za kila siku ambazo zilikatizwa na habari za kutokea kwa ajali? Ndiyo maana muungozo wa kushughulikia ajali za ndege unakataza kuwa lengo la uchunguzi ziyo kutafuta mwenye makosa ila kujifunza ili kesho ya safari za ndege iwe salama zaidi
 
So huo mlango unavunjwa kwa Kasia? Let's be realistic.

Hiyo ndege uliyopost unaweza nionyesha mlango wa pilots ulipo?

Unawezaje kusema wahudumu hawakuonyesha jitihada? Wakati nao walikua busy kuokoa abiria wapite mlangoni.

Sijakataa Majaliwa alijitoa ila nachopinga ni narrative kwamba yeye ndio alikua pivotal watu 24 kupona. Nadhani ni vizuri kusema wavuvi wote walisaidia ila Majaliwa anapewa zawadi kwa manusura kupoteza uhai wake kuokoa maisha ya wengine.
 
Mkuu ni propogada ili zimunufaishe nani?
Ili lawama Zi divert kutoka kwa serikali maana "TUKIO" limezaa "mashujaa" so inakua blessing in disguise. Ndio maana mitandaoni hakuna anayejadili uzembe wa serikali Kila mtu anajadili nani alifungua mlango na wengine wanajadili jinsi Gani ajali ilikua bahati ya Majaliwa kuheshimika!!

Kazi ya TISS ni kuwa ahead of events to control narrative, na sio Tz tu nmekueleza hata Iraq, USSR, na Finland walitumia fictional stories za "snipers" kama Simon Hayha kujenga narrative kuwa vita ya dunia sio "hasara" Bali uwanja wa "mashujaa" kuonekana!!
 
Mlango upi wa marubani kwenye hiyo ndege? maana umekazana mlango labda mie ndio siuoni.

Kingine Majaliwa kweli alitaka kufa kwenye jitihada hizo ila hakuwa peke yake mitumbwi ilishafika na ikabeba watu maana hata Majaliwa na majeruhi wangekufa kama sio mitumbwi kuwasaidia!!

So Majaliwa ni shujaa kama wale wavuvi na air hostess na yule mchina walivyopambana kuokoa wenzao..nachopinga ni kumkuza huyo dogo kana kwamba Ali act alone!
 
Mkuu hiko kichwa kata ubadilishàne na mbwa mana Dah ni mpuuzi kiufupi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…