Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

dosama

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
912
Reaction score
957
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).

"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.

Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.

Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.

Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.

Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.

Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.

Source: Majira
 
A twist of the tongue.... only few we'll be able to understand this...... come the day when words will match the deeds... as for me.... I'm out...!

Mkuu,

Inaelekea umekatishwa tamaa na kutokutekelezwa kwa kauli ya Mbowe kuwa hatagombea tena uenyekiti.
 
CDM watakuja kujua umuhimu wa Zitto baadaye. Zitto ni jembe sana ndani ya CDM Hana siasa za maji taka Kama akina Lissu, Lema na Sugu. Hakuna asiyejua mchango wa Zitto kwa CDM. Hawa vijana akina Lema hawajengi CDM Bali wamekidhoofisha sana chama kwa siasa zao za maji taka. Pumzika kaka pumzika Zitto
 
Source Majira

Mbunge wa kigoma kaskazini bwana Zitto Kabwe kafichua siri nzito na kudai hana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 na wala hatagombea ubunge ila anataka kutafuta chuo na awe mwalimu wa chuo na analenda sasa kufundisha maswala ya uchumi na mazingira ndio dhamira yake

Mtu complex hawezi toa maelezo mepesi kiasi hiki,kwan mbunge hawezi kufundisha???!!!!
Si anakaa Dar jimbo lipo Kigoma sasa atashindwa kuishi Mwanza kwenye vyuo na aendelee huko kanda ya ziwa???!!

If this is true ,he should come out clean!!!!!

Kwa uwezo wake na matumaini ya baadhi ya watu juu yake ni sawa na dereva kugomea safari katikati ya msitu!!!!

Aseme safari ngumu.??????
Gari bovu????!
Uwezo wa kuendesha umeshuka??!!!
Konda na tanboi hawampi ushirikiano safarini???!!!!
Nia ilikuwa sio kufika???!!!
Alitaka tu kuonekana akilitoa basi kituoni????!!!!!
Alitaka kuendesha magari katika kampuni ya kimataifa ila ilikiwa ni lazima aendeshe basi kwanza???
 
Mengi yataibuka tusubiri tu.
 
katiba mpya imepatikana au jamaa amelishwa maneno?kulikuwa na thread inayomhusu kuwa hatazungumzia mambo haya mpaka katiba mpya ipatikane
 
katiba mpya imepatikana au jamaa amelishwa maneno?kulikuwa na thread inayomhusu kuwa hatazungumzia mambo haya mpaka katiba mpya ipatikane

Thread za humu zingine ni za kizushi tu, Katiba mpya inahusiana vipi na maisha ya mtu binafsi?
 
Sipati picha jinsi gani Dr Slaa atakavyo furahishwa na hii habari. Babu relax, Zitto is no longer your threat.

Naona Babu atakwenda honeymoon tena Israel na kimwana chake cha kihaya kupumzika. Maana watakuwa wamepumua sana. Na wanazi wengi wa CDM hii ni furaha sana kwa ndugu yangu Molemo, Ben Saaanane na wengine wenye mrengo kwa kushoto juu ya Zitto. Maana na wao wanafikiri sasa wanaweza pumua na kujipatia vyeo ndani ya CDM. Yaani mi sijuwi kazi ya akina Ben na wenzake ndani ya CDM na umuhimu wa Zitto kwa siasa za nchi. Zitto ni mtu makini huwezi fananisha na Ben hata kidogo na kwa hakika watajuta baadaye.
 
Mtu complex hawezi toa maelezo mepesi kiasi hiki,kwan mbunge hawezi kufundisha???!!!!
Si anakaa Dar jimbo lipo Kigoma sasa atashindwa kuishi Mwanza kwenye vyuo na aendelee huko kanda ya ziwa???!!

If this is true ,he should come out clean!!!!!

Kwa uwezo wake na matumaini ya baadhi ya watu juu yake ni sawa na dereva kugomea safari katikati ya msitu!!!!

Aseme safari ngumu.??????
Gari bovu????!
Uwezo wa kuendesha umeshuka??!!!
Konda na tanboi hawampi ushirikiano safarini???!!!!
Nia ilikuwa sio kufika???!!!
Alitaka tu kuonekana akilitoa basi kituoni????!!!!!
Alitaka kuendesha magari katika kampuni ya kimataifa ila ilikiwa ni lazima aendeshe basi kwanza???

Basi limejaa chawa mpaka kwenye kiti cha dereva. Basi hilo uking'ang'ania kuliendesha unaweza kuliangusha wakati wa kujikuna...
 
Back
Top Bottom