Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Zitto sio tishio kwa Dr Slaa bali anajitanabaisha tu,yeye ndo kapima kina cha maji akaona kirefu

Mkuu, mtu ukishaambiwa you are from nowhere na mmiliki wa chama, basi lazima uone kima kirefu.

Siasa ni kazi za watu, inafanywa kutokana na mahitaji yao. Kama chama kinaona Zitto is from nowhere, kwanini ang'ang'anie?
 
Umenena mkuu awaachie siasa zao za maji taka akina Ben....maana yeye kila siku akiamka anamfikiria Zitto. Huyu jamaaa Ana wivu sana tena anafikiri Zitto akipumzika yeye atapumua na kuwa Kama Zitto laa hasha hawezi kumfikia Zitto hata kwa asilimia 2. Yaan sawa na kufananisha na Tembo na digidigi


Na wewe je na urali wako wa HAMY-D kila siku kumuwaza Slaa??!!

Nchi imegeuzwa ya propaganda na uzushi pasipo umakini wa mahitaji ya wananchi na uchumi wa taifa,kazi ni kutetea madudu ya sirikali!!!!
 
Sio kila mwenye sera mzuri anakijenga chama mwingine anakibomoa siasa ni mchezo mchafu
 
Taarifa toka majira? ni sawa na Uhuru, mzalendo, Mtanzania, jambo leo..........
 
Wote Mh. Zitto, hata mwaka 2010 alianza hivi hivi mara sitaki mara nataka lakini mwisho wake akagombea. Tunasubiri atuletee changamoto kwenye demokrasia ya ndani ya cdm pale watakapoanza kuchaguana.
 
Naona vijana wa lumumba mmeteka topic.
Ukitaka wasahau hadi viatu zungumzia masuala ya SEMBE kama utawakuta. Leo hawatoki kwenye huu uzi tena bado baba lao Ritz hajaiona hii thread lol!
 
Kutokana na principles of demand and supply, habari hii itasababisha bei ya sumu madukani kushuka.

Hahahahaha. Wenye maduka itabidi wafanye market research ya bidhaa nyingine hii itakuwa haina soko tena.
 
Anaye dhania kuwa bila Zito cdm itakufa huyo ni gamba gumu A
 
Wote Mh. Zitto, hata mwaka 2010 alianza hivi hivi mara sitaki mara nataka lakini mwisho wake akagombea. Tunasubiri atuletee changamoto kwenye demokrasia ya ndani ya cdm pale watakapoanza kuchaguana.

Cdm haitaki changamoto za kisiasa. Mamluki ndio mahero kwasasa na walioitoa cdm shimoni they are nothing.
 
Last edited by a moderator:
Vijana wengi wa kitanzania ni wajinga, naona wimbi la vijana hapa JF wakidhihirisha ujinga. Zitto mwenyewe kama kasema kuwa hatagombea urais basi nae namweka kwenye kundi la wajinga.

Sielewi. Kwani Zitto hata akiutaka urais hawezi kugombea 2015 katiba haimruhusu, na pia hata km katiba haimruhusu kabla yaa kutoa dhamira atambue ktk chama kuna mchakato wa kumpata mgombe urais (wapo wengi chadema).

Ukiona mtu anaimba hii chorus ya Zito kusema hatagombea urais ni alama ya ujinga. Ni sawa na Juliana shonza, au mtela aseme nimeahirisha 2015 sitagombea urais. Alafu wewe unaanza kujenga hoja kuhusu hiyo kauli na unasikitika while in a real sense hata wangetaka wasinge weza sababu ya umri.

Zitto amegundua katiba mpya haitamfavor na pia amepoteza ile catch aliyokuwa nayo, siyo vibaya akapumzika labda (aje kuwa waziri km katiba itaruhusu ndicho anachowaza maana rasimu inaonesha mawazir hawatatokana na wabunge).

Zitto hana tofaut na JK. Anapenda kufanya movement within institution in the end apate reward yeye mwenyewe, na aonekane yeye ndio don. Kama jambo halimpi sifa yeye binafsi hawezi kulifanya (ubinafsi na sifa)

Ana tabia ya usaliti. Sasa hapa ni tabia ya watu wa kigoma (wild kaborou, nsanzugwanko, david kafulila)..hata tafuta mtu wa kigoma hapo ulipo wana asili ya kutait.


Pia sio msaada ndani ya cdm..ikumbukwe 2010 wakati wanamnadi Slaa yeye anajinadi kuwa atagombea urais, wakati wenzake wanapambana na wizi wa kura yeye anapigiana simu na Jaki zhoka, wakati wenzake wanalounch M4C yeye yupo na akina Ben sanane,akina juliana shonza wanajenga mikakati ya kumpindua mbowe, wakati wenzao wanaamsha maandamano yeye yupo na cloudsfm anaongea dili na ruge kuanzisha kampuni ya PERA ringtones.

In short Zitto ndani ya chadema hana lolote watu ambao wanakijenga chama wanajulikana. Zitto nadhan anajua kucheza na akili za watanzania wajinga ila sio mimi.
 
Zitto ni hazina Chadema, kuondoka kwake iwe kwa mazingira yoyote yawayo ni HASARA na PIGO kubwa sana kwa Chadema.

Nawahakikishia iwapo hii ni kweli, Chadema itapasuka. Period!
 
Sasa Zitto anaonyesha ukomavu!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Yaan sawa na kufananisha na Tembo na digidigi

Ukitamka neno Tembo majangili mate yanawatoka kwa uchu!

Inasikitisha 2029 Tanzania hakutawepo na Tembo(mnyama mkubwa kupita wote kwa sasa wanaoishi nchi kavu!)

Nani anawamaliza Tembo wetu?
 
CDM watakuja kujua umuhimu wa Zitto baadaye. Zitto ni jembe sana ndani ya CDM Hana siasa za maji taka Kama akina Lissu, Lema na Sugu. Hakuna asiyejua mchango wa Zitto kwa CDM. Hawa vijana akina Lema hawajengi CDM Bali wamekidhoofisha sana chama kwa siasa zao za maji taka. Pumzika kaka pumzika Zitto


nini? umeamka huna pesa ya chai?
 
Ukitaka wasahau hadi viatu
zungumzia masuala ya SEMBE kama utawakuta. Leo hawatoki kwenye huu uzi
tena bado baba lao Ritz hajaiona hii thread lol!

hakika kuondoka kwa zitto chadema ni pigo kubwa kwa chama hicho ingawa kwa upande mwingine kuna watu watapumua
 
Ninachojua kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba ambayo itapita, ZZK atakuwa WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI, (waziri hatakuwa mbunge na atapewa kazi ya uwaziri kwa kuzingatia taaluma yake) KAKA ZZK yupo sahihi na naamini atafanikiwa kufufua uchumi wetu. Maccm mlie tu, 2015 huyohuyo ZITO atapeleka charge mahakama ya ICC kufilisi majangili yote.
 
Back
Top Bottom