[h=2]Saturday, February 2, 2013[/h] [h=3]Zitto awaaga wapiga kura wa Kigoma Kaskazini[/h]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: justify"]
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kutokana na kuliongoza jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo, sasa ametangaza rasmi kutowania nafasi hiyo tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Alisema kazi kubwa aliyoifanya kwa wananchi wa jimbo lake, imefika wakati sasa wa yeye kupumzika kuweza kupisha watu wengine waweze kuliongoza jimbo hilo, huku akiahidi kuendelea kufanya shughuli za maendeleo pasi ya kuwa mbunge.
Kutokana na kauli hiyo aliiyoitoa mbele ya wananchi katika mikutano yake ya hadhara iliyofanyika katika Kata za Bitale na Mahembe iliyofanyika juzi na jana, iliwafanya baadhi ya wananchi kuangua vilio huku wakipinga hatua yake ya kutaka kutogombea tena nafasi hiyo.
Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, alisema ni muhimu kwa wanasiasa hasa wanaojitambua kutumia nafasi zao kupima uwezo wa namna ya kuwaongoza wananchi kwa kusukuma maendeleo yao, kuliko kutumia muda mwingi kungangania madaraka.
Ninachokifanya ndugu zangu ninaomba mjiandae kisaikolojia katika hili, ninatamka wazi kuwa mwaka 2015 sitagombea ubunge tena katika jimbo letu hili la Kigoma Kaskazini na lengo la kufanya hivi ni kutoa fursa kwa watu wengine kutoka ndani ya Chadema nao waonyeshe uwezo wao wa kuwahudumia wananchi.