Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Lumumba bana!!!!mbona mwajadili nyie tu!!?mchukueni kama mnamhitaji sana awe mwenyekiti wenu
 
Kwani ni lazima awe mbunge au Rais? Hawezi kuonesha uzalendo wake kwa namna nyingine?

Tuliosoma pale mlimani tunamfahamu huyu kijana hashauriki. Akiamua la kwake ndilo hilo atakalosimamia. Jambo moja nalo lifahamu kwake, Zito ni mzalendo. Sijui pengine alipopata hela kama alibadilika. Mimi ushauri wangu kwake aendelee kupigana kwenye mfumo ndani ya CDM. Akihama chama ataisha kisiasa, atazidi kupoteza credibility. Nina uhakika kwamba uchuguzi wa mwakani utawaibua vijana wengi charismatic zaidi ya Zito. Nchii hii ina hazina kubwa sana ya watu wenye uwezo.
 
Ukisoma hii ndiyo inadhibitisha kabisa Zitto ni pandikizi la chama cha kifisadi lililo shindwa kufikia malengeo, kwanini ashabikiwe na wana lumumba kiasi hiki!...kama zitto ni mzuri naman hii mchukueuni asaidie chama chenu sisi hatumtaki
 
Zitto hapendwi kwa sababu hatoki kaskazini.

Inaonyesha mmetumwa Zzk si chochote kwa chadema akiwepo sawa asipikuwepo pia ni poa.Mnamdanganya dogo wa watu.nafikiri ameanza kuona alivyoporomoka kulingana na kauli zake za kusema alichonganishwa na Mbowe.
 
Zitto ni ngumi jiwe

kwa wale wanaojua biashara ya daladala kweli Zitto ni JIWE

na moja ya malalamiko ya madereva na makondakta ni kugandwa na jiwe/mawe hadi hesabu kupungua
 
Last edited by a moderator:
Zitto ataendelea kuwa mwanasiasa bora barani Afrika,umri ukishushwa akagombea urais atashinda SAA NNE asubuhi.
 
[h=2]Saturday, February 2, 2013[/h] [h=3]Zitto awaaga wapiga kura wa Kigoma Kaskazini[/h]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: justify"]Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kutokana na kuliongoza jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo, sasa ametangaza rasmi kutowania nafasi hiyo tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.


Alisema kazi kubwa aliyoifanya kwa wananchi wa jimbo lake, imefika wakati sasa wa yeye kupumzika kuweza kupisha watu wengine waweze kuliongoza jimbo hilo, huku akiahidi kuendelea kufanya shughuli za maendeleo pasi ya kuwa mbunge.


Kutokana na kauli hiyo aliiyoitoa mbele ya wananchi katika mikutano yake ya hadhara iliyofanyika katika Kata za Bitale na Mahembe iliyofanyika juzi na jana, iliwafanya baadhi ya wananchi kuangua vilio huku wakipinga hatua yake ya kutaka kutogombea tena nafasi hiyo.


Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, alisema ni muhimu kwa wanasiasa hasa wanaojitambua kutumia nafasi zao kupima uwezo wa namna ya kuwaongoza wananchi kwa kusukuma maendeleo yao, kuliko kutumia muda mwingi kung’ang’ania madaraka.


“Ninachokifanya ndugu zangu ninaomba mjiandae kisaikolojia katika hili, ninatamka wazi kuwa mwaka 2015 sitagombea ubunge tena katika jimbo letu hili la Kigoma Kaskazini na lengo la kufanya hivi ni kutoa fursa kwa watu wengine kutoka ndani ya Chadema nao waonyeshe uwezo wao wa kuwahudumia wananchi.
 
[h=2]Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015[/h]
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Refer to: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/511990-zitto-sitagombea-urais-wala-ubunge-2015-a-17.html

 
Yani post ya kwanza mpaka kumi ni ID za chama.????? Sasa naamini maneno yamzee tupatupa, afanye kukusanya hizo tablets tuu kama vichwa ndo hivyo vya,kutegemewa.

Kweli kabisa, watu saba kwenye ID moja wamejipanga kama domino, wote wanaandika kwa pamoja kisha wanasubiri yule wa kwanza akibinya 'send' na wengine wanafuatia kwa kupokezana
 
Back
Top Bottom