Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

CCM bila kumjadili Tozzi hamlali, lichukueni liwe limwenyekiti wenu, nyambaf
 
wadandiaji wa siasa mtakoma mwaka huu, mbowe kujiunga na chama kingine cha upinzani endapo atakosa uenyekiti.

Hapo kwenye Blue ulikutana naye wapi akakuambia hayo???? au ni keyboard imekataa kushirikia na ubongo?????
 
zitto,anakosea sana anaposema hauni mtu mwenye sifa za kuwa rais zaid yake,jaman wana JF,kiongozi mwenye sifa cku zote anapendekezwana watu na si kujipendekeza wewe kuwa unaweza kuliko wote.tabia yake hii imewwkwaza sana viongozi wenzake ndan ya cdm,yeye anajua kila kitu ndani ya chama,nafasi ikitokea yeye anataka awe yeye.mawazo yake ni potofu sana,huwezi wewe ukajiona unajua zaid au unasifa zaid kuliko wenzako.HATA KAA AWE RAIS.............................TIME WILL TELL!
 
MWANZONI MWA MASAKATA YAKO NA CHADEMA, NILIAMINI SI KWELI WATU WANAKUFITINI, NA KUKUONEA GERE, LAKINI KWA MAANDISHI YAKO HAYA NA KUGEUKA GEUKA KAMA KINYONGA LEO NIMEAMINI 100% WEWE ULIYAFANYA HAYO YANAYOSEMWA NDIO MAANA LEO UNAWEWESEKA, MARA SIUTAKI UBUNGE, MARA URAIS, MARA KIGOMA MJINI, MARA KUFUNDISHA , HUELEWEKI DOGO WEWE NI POPO AMAA...zitto uraisi utausikia tu bwana mdogo kwa akili yako hii ya kujiona wewe ndiye kila kitu kimasters hicho kinakupa kiburii.,.hivi kwewnye wasomi na wewe upo?? Kweli dogo??, unadhani kuongoza nchi ni rahisi kama kumtongoza huyo diva, bwanamdogo mtu makini huchaguliwa na kupendekezwa na watu baada ya kumpima kwa kina. Tabia yako ya kujiona unajua kila kitu imekupoteza soon katika siasa, ndani ya miaka 2 ijayo utakuwa kama mrema mzee wa kilalacha. Ungetulia ungefika mbali sana, sasa umeanza kutapata kama kuku anayetaka kutaga , ulitoa maneno ya hovyo sana dhidi ya chama ooh ni cha kihafidhina, nimeanza na vifaranga namtafuta mama yao.. Si undoke chadema sasa hata ukijadiliwa uanachama wako ili iweje kama hukipendi chama ondoka.. Wewe si maarufu ondokaaaaaaa.....unauzalendo gani bwana mdogo, unaumakini gani bwana mdogo.. Unaona waliokubeba na kukupa majukumu ya kuiua chadema, leo hawana hamu na wewe..vip bado unamawasiliano mazuri na lukuvi, wasira, au kimei??.. Siku zako za kung"aa zimekwisha. Hizo ndio siasa za bongo mtafute john cheyo akupe ushauri amewezaje kuwa mbunge mmoja wa maisha na chama chake. Kwisha habari yako, waliokudanganya wako wapi???. Bure kabisa wewe....
 

kabwe-zitto-zuberi_300_288.jpg


"KUGOMBEA urais mwakani ni suala nililoulizwa na watu wengi pamoja na vyombo vya habari, ni kweli nautaka urais, nataka kwa sababu naamini ninao uwezo na pia changamoto za nchi hii nazijua vizuri," anasema Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto kwa kujiamini.

Zitto ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) tangu akiwa kijana mdogo, akiwa na miaka 16. Anasema angependa kuwa Rais wa nchi hii kwa sababu anaamini ana uwezo mkubwa wa kutumikia nchi; anajua vizuri changamoto za Watanzania na nia yake hiyo ni ya dhati.

"Mimi ni tofauti kabisa na viongozi wengine wanaojifanya wameombwa na wazee au vijana kugombea uongozi, mkiwaambia watuoneshe hao watu waliowaomba kugombea, hawataweza kuwaonesha. Mimi ninaamini uwezo ninao wa kuwa Rais," anasema. Zitto alizaliwa Septemba 24, 1976 mkoani Kigoma na baadaye kupata Shahada ya Kwanza ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kutoka hapo aligombea ubunge na kuwa Mbunge wa jimbo hilo mwaka 2005. Anasema ingawa angependa kugombea urais, Katiba ya sasa inaeleza sifa za mtu anayetaka kugombea urais, ni lazima awe na umri wa kuanzia miaka 40 ambayo yeye hana.

"Katiba sasa hivi inasema ili mtu agombee urais, anatakiwa kuwa na miaka 40… sijui kuna nini kwenye hili kwa sababu nchi kama Kenya, Malawi, Marekani, Rwanda, Burundi, Msumbiji na Afrika Kusini ni miaka 35," anasema Zitto.

Zitto anasema kama hali itabaki hivyo, atamuunga mkono mgombea anayeijua nchi vizuri kwa sababu Tanzania inahitaji Rais atakayewaunganisha Watanzania na siyo anayewagawa, na mtu huyo aoneshe kabla ya kuchaguliwa ni namna gani atatekeleza hilo.
Hata hivyo Zitto anasema hawezi kusema kuwa amezaliwa kuwa kiongozi, ila jamii imemtengeneza kuwa kiongozi ambaye sasa anaamini uwezo alionao ni mkubwa, katika kutatua changamoto za Watanzania.

Novemba 22 mwaka jana, Zitto aliingia katika mgogoro na chama chake ambapo alisimamishwa uongozi katika chama na kuondolewa katika nafasi ya Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, baada ya kutuhumiwa kuhusika na njama za kuhujumu chama hicho.

Kuhusu fununu kwamba ana mpango wa kujiunga na chama kipya cha siasa, Zitto anasema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu lina kesi iliyoko mahakamani mpaka pale uamuzi utakapotolewa na mahakama katika kesi hiyo.

"Siwezi kusema lolote kuhusu kuanzisha chama kipya au kujiunga na chama chochote, kwa sababu nasubiri uamuzi utakaotolewa na mahakama katika kesi hiyo," alisema. Anasema kwa kuwa yeye ni mwanasiasa na anataka aendelee kubaki kwenye jukwaa la siasa ila anasisitiza hawezi kusema ni chama gani atajiunga nacho, na kama hilo likitokea, haitakuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Watanzania wasiwe na haraka, wasubiri tu lakini kwa sababu mimi ni mwanasiasa nitaendelea kuwa kwenye majukwaa ya siasa ingawa siwezi kusema ni chama gani, na haitakuwa chama kilichoko madarakani," anasema Zitto. Wengine waliosimamishwa uongozi na Zitto ni Profesa Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Viongozi hao wawili, wamejiunga na chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT), ambacho Zitto anahusishwa nacho. Akizungumzia uwepo wake ndani ya Chadema, Zitto anasema amekuwa akikitumikia chama hicho tangu akiwa na miaka 16 na sehemu kubwa ya maisha yake ametumikia chama hicho na hajawahi kuingia katika chama chochote.

"Nimetoa jasho kubwa katika ujenzi wa Chadema, nimeimarisha mambo yangu mengi na mengine kuyasimamisha kabisa kwa ajili ya ujenzi wa chama," anasema Zitto. Kuhusu madai kwamba amekuwa anatumiwa na CCM, Zitto anasema tuhuma hizo ni maneno tu au siasa nyepesi za baadhi ya watu zisizo na mashiko yoyote.

"Hivi mbunge anayetumiwa na CCM anaweza kupeleka hoja bungeni kutaka kumuondoa madarakani Waziri Mkuu, anaweza kupeleka hoja bungeni ya kuhakikisha mikataba yote inakuwa wazi ikiwemo ya gesi?" Anahoji. Anasema wanaotoa madai hayo, ni vyema wajitokeze na kusema wamefanya nini kwa ajili ya taifa lao kwa sababu amejitoa katika mambo mengi ikiwemo kukosoa Serikali iliyoko madarakani na kuisimamia.

Zitto anasema yeye ni kiongozi anayeamini nchi inahitaji mfumo wa vyama vingi wenye nguvu, akiamini kwamba kutegemea chama kimoja ni hatari katika uhai wa nchi na usimamizi wa rasilimali zake.

"Kupitia nafasi yangu ya mbunge, nimefanya kazi za hatari kusimamia Serikali, ili iwajibike na kwa kufanya hivyo nimepambana na watu wenye nguvu. "Nimepambana katika migodi ya madini na mambo ya gesi na kwa kufanya hivyo nimepambana na watu wakubwa na kampuni kubwa za wenye fedha. Hata Mungu akinichukua leo hii nitaridhika tu, nikijua nimefanya kazi yangu," anasema Zitto.

Zitto anasema anatamani kuingia darasani kufundisha kwa sababu ndio mwito alionao sambamba na kusoma vitabu mbalimbali hata hivyo anasema siasa haijampa nafasi hiyo. "Natamani sana kuingia darasani kufundisha, ninapoona wenzangu wanafundisha, wanaandika najisikia furaha sana ningefurahi na mimi nije kupata fursa hiyo lakini siasa haijanipa kabisa fursa hiyo," anafafanua.
Zitto anasema msimamo wake kuhusu Bunge Maalumu la Katiba ni kuahirishwa kwa bunge hilo kwani bila maridhiano, hakuna Katiba itakayopatikana kwa maridhiano ya kisiasa hata kama itakuwa na maridhiano ya kisheria. Hata hivyo Zitto anasema ingawa haridhishwi na mwenendo wa Bunge hilo, yeye si sehemu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu vyama vinavyounda umoja huo, ni pamoja na Chadema ambacho ana kesi nacho.

Anasema ana maono tofauti na CCM na pia Ukawa kuhusu muundo wa Muungano kwani kwa mtazamo wake ni kuwa na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati Zanzibar na Tanganyika zikiongozwa na mawaziri wakuu.

"Mimi sijawahi kuwa Ukawa wala katika kundi lolote lile la Bunge Maalumu la Katiba, isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa washirika wake," anasema katika mahojiano hayo.

Zitto anasisitiza umuhimu wa kupata Katiba lakini anatoa angalizo kuwa kwa hali ya sasa, kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana, ambapo wameamua kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Zitto anakubaliana na hatua ya sasa ya kuendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, baada ya Katiba ya sasa kufanyiwa marekebisho kadhaa yatakayohusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ili iwe huru na ionekane kuwa huru na kuondoa watumishi wa halmashauri za wilaya, miji na vijiji katika kusimamia uchaguzi.

Mabadiliko mengine anayokubaliana nayo ni kuruhusu mgombea binafsi na kuondoa mafuta na gesi kama jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano. Pamoja na mambo ya siasa, katika maisha nje ya siasa Zitto ni mlezi wa kundi la wasanii wa Mkoa wa Kigoma la Kigoma All Star ambalo linaendesha kampuni ya Lekatutigite.

Anasema hanufaiki kwa namna yoyote katika kundi hilo na wakati mwingine inabidi atoe fedha zake kusaidia msanii ndani ya kundi na furaha yake ni kuona wasanii hao wanafanikiwa. "Nimewafungulia Saccos wasanii hao ili waweke amana na kukopeshana pale msanii anapohitaji fedha mfano za kutengeneza video na atakapoanza kupata shoo, anaanza kurudisha fedha pole pole, leo mimi nipo lakini kuna siku Zitto sitakuwepo," anasema.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu ndoa, alikataa kabisa kuzungumzia suala hilo na kusisitiza kwamba muda utakapofika ataoa na mke atajulikana kwa wakati huo. "Siwezi kutaja jina la nani nitamuoa just like that, mimi ni Muislamu na maadili yetu hayaruhusu kutangaza uchumba, unatangaza ndoa na wanaopenda kujua watamjua, sijaoa kwa siri kwasababu sina sababu ya kufanya hivyo," anasema Zitto.

CHANZO:
Habari Leo
 
Huyu ni mwislamu wa aina yake kwahiyo maadili ya kiislamu yanaruhusu uzinzi? Zitto Kabwe utaacha lini uzinzi?
 
urais wa lekadutigite umemshinda yaani kumuongoza linex.baba levo.omari madipozi.mondi na c&o kashindwa sasa urais wa hii nchi atauweza
 
Urais kwa watu wanaoshinda kwenye disco mpaka saa 11 alfajiri!zitto unatania hauwezi.
 
Huyu ni mwislamu wa aina yake kwahiyo maadili ya kiislamu yanaruhusu uzinzi? Zitto Kabwe utaacha lini uzinzi?
upuuzi na dharau hivi wapelekee babayako na mama yako mbwa wewe
hatuwezi vumilia upuuzi wa kiasi kikubwa kama hiki
 
Labda urais wa wasafi clasic tena ampokonye domo diamond achukue yeye na Diva
 
upuuzi na dharau hivi wapelekee babayako na mama yako mbwa wewe
hatuwezi vumilia upuuzi wa kiasi kikubwa kama hiki

mkuu naona maajabu kidogo,kuna mbwa kapost humu?kajuaje kusoma na kuandika?katumia lugha gani?


kwanini usiseme tu ustahimilivu wako ni mdogo badala ya kutumia "hatuwezi"?mbona wote hatujasema mbwa?
 
upuuzi na dharau hivi wapelekee babayako na mama yako mbwa wewe
hatuwezi vumilia upuuzi wa kiasi kikubwa kama hiki

Hivi Zitto na Diva wanafanyanye kama siyo uzinzi? Na yule mtoto wa Zitto Kabwe Chachage siyo mtoto wa Zinaa? Au nipe ilmu kwenye dini ya kiislaamu ukizini kama anavyoendelea kuzini Zitto Kabwe ukizaa mtoto huyo mtoto anaitwaje?
 
upuuzi na dharau hivi wapelekee babayako na mama yako mbwa wewe
hatuwezi vumilia upuuzi wa kiasi kikubwa kama hiki


Yesu akusaidie ndugu,

Unamwita mwenzako mbwa?
Baba yake na mama yake
wamekukosea nini?

Siyo njia sahihi ya kumrekebisha
mtu hii.
 
Back
Top Bottom