Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Zito akiwa raisi kutoka kwenye michezo ya mpira wa miguu by jk tutaingia kwenye mchezo wa kukata kiuno mpaka asubuhi over
 
sasa mbwa ni zito mzinzi ama mtoa hoja?

Huyo mzinzi na wewe mtukana matusi ndio waislam safi????

Pole. Mtafute Mungu wa kweli atawale maisha yako. Hakuna mtu anamwabudu Mungu wa kweli atatukana watu mbwa tena bila hoja!.

upuuzi na dharau hivi wapelekee babayako na mama yako mbwa wewe
hatuwezi vumilia upuuzi wa kiasi kikubwa kama hiki
 







6810127042_e0a19186bb_z.jpg
Na: Frank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma,
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

"Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. "Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.

"Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu. "Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi." Atangaza kugombea urais Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. "Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii," Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; "Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya."

"Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo," alisema Zitto Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46. Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.

"Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu," alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

"CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?" Alihoji Zitto. Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.





"Leo anasema eti Ukawa ni wasaka Tonge " Give me a break Zito Kabwe. Hapo ulikuwa unataka Uraisi ili iweje? Je hicho kilikuwa nini? Je hujioni unatamaa ya fisi??






 
Hata kama katiba ikiruhusu mgombea awe na umri kama wake bado kuna kikwazo kingine.

Kulingana na makubaliano ya vyama vinavyounda UKAWA kusimamisha mgombea mmoja tu, ni dhahiri ndoto za bwana huyu zimeshazimwa...
 
Labda agombee uraisi wa lile kundi lake la kupigia hela NSSF na TANAPA la LEKA DUTIGITE, sio uraisi wa Tanzania

Kwa namna upepo wa kisiasa ulivyombadilikia huyu jamaa sidhani kama hata huo ubunge atapata tena maana huku kabanwa na UKAWA na kule kabanwa na MaCCM, sasa atatoka vipi? Labda ajiunge CCM. Kwa sasa anachoweza kushinda ni nafasi ya DIWANI KATA YA MWANDIGA, ambako ndugu zake watamuonea huruma asitoke kwenye ulingo wa siasa kabisa, hiyo habari za uraisi ni ndoto kama ndoto zingine, hata mtoto wa darasa la pili ukimuuliza unataka kuwa nani ukikua atakwambia anataka kuwa daktari, au Profesa kama Kikwete, mtu hazuiliwi kuota ndoto, muacheni Zitto aote
 
Mbona nimesekia anawabeza ukawa huyu mbona-ameanza kuzeeka ili hali ni damu changa. Kuwabeza ukawa na kudai unahitaji vyama vibadilishane katika kushika dola lazima akili yako inawalakini
 
Kitendo cha Ukawa kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais ndicho kilicho mkela Zitto na kusababisha kubwabwaja maneno ya hovyo kuasi hicho.
 
Zitto Kabwe. Msaka tonge huwa ni yule anayelipwa fedha na Ramadhan Dau wa NSSF. PIA hupokea bakhshish kutoka kwa Nimrod Mkono. Unamjua ni nani lakini?
 
Huyu Zito hana uchungu na nchi hii.Hali anajua tangu alipotoka Nyerere madarakani hakuna kiongozi yoyote kwa maraisi waliofuata waliotetea masikini.Anyamaze kabisa tumechoka na viongizi wanaolinda walarushwa.
 
Mimi nadhani tuendelee kujadili namna ya kuwaondoa hawa mafisadi (CCM) madarakani 2015, kupitia UKAWA, Zitto asituhamishe kwenye hii ajenda ya kuwang'oa mafisadi!
 
Wazo la upofu hiloo!!ukawa washajiunga kuing'oa ccm kwa iyo hakuna mgombea wa chadema mwakani ifahamike yuko wa ukawa tu!!
 
Hata kama katiba ikiruhusu mgombea awe na umri kama wake bado kuna kikwazo kingine.

Kulingana na makubaliano ya vyama vinavyounda UKAWA kusimamisha mgombea mmoja tu, ni dhahiri ndoto za bwana huyu zimeshazimwa...
Kwani yeye yupo Ukawa?
 
Back
Top Bottom