Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna kitu kama hicho,
Chuki zenu binafsi
Mtu complex hawezi toa maelezo mepesi kiasi hiki,kwan mbunge hawezi kufundisha???!!!!
Si anakaa Dar jimbo lipo Kigoma sasa atashindwa kuishi Mwanza kwenye vyuo na aendelee huko kanda ya ziwa???!!
If this is true ,he should come out clean!!!!!
Kwa uwezo wake na matumaini ya baadhi ya watu juu yake ni sawa na dereva kugomea safari katikati ya msitu!!!!
Aseme safari ngumu.??????
Gari bovu????!
Uwezo wa kuendesha umeshuka??!!!
Konda na tanboi hawampi ushirikiano safarini???!!!!
Nia ilikuwa sio kufika???!!!
Alitaka tu kuonekana akilitoa basi kituoni????!!!!!
Alitaka kuendesha magari katika kampuni ya kimataifa ila ilikiwa ni lazima aendeshe basi kwanza???
CDM watakuja kujua umuhimu wa Zitto baadaye. Zitto ni jembe sana ndani ya CDM Hana siasa za maji taka Kama akina Lissu, Lema na Sugu. Hakuna asiyejua mchango wa Zitto kwa CDM. Hawa vijana akina Lema hawajengi CDM Bali wamekidhoofisha sana chama kwa siasa zao za maji taka. Pumzika kaka pumzika Zitto
Well said mkuu, Zitto ana kitu kinachomsumbua 'distinction' ambacho kwa kila mtu makini hukihitaji, ila ninavyomuona hadi sasa bado hajaamua ni kipi kati ya siasa na taaluma kitakachomfikisha huko, namshauri awe makini wakati wa kuchagua njia sahihi asipokuwa makini mwisho anaweza kufikiri njia yeyote inaweza kumfikisha, which is very wrong.Honest speaking Zitto hana tofauti na Samwel Sitta, wote ni watendaji wazuri sanaa lakini madumila kuwili na wapenda sifa binafsii.. Sina chuki na Zito wala Sitta na nawakubali sanaa wao kama wao ila as part of team hawa ni majangaa... Hapo ndio kwenye challange CDM inamtumiaje Zitto, chonde viongozi wa chadema hebu kaeni na huyu kijana muone mnaweza kumsaidi vipi ili atimize ndotto zake, kwa fikra zangu ndani ya CDM zitoo anazidi kufunikwa na vijana kama kina Lisuu, Mnyika, Lemaa na 2015 si ajabu akafunikwa moja kwa mojaa.. Siasa ni kazi na Zito ni mmoja kati wanasiasa vijana waliofanikiwa kupitia chadema ila hilo halitoshi kwake (job satisfaction) kuna kikubwa zaidi anakihitaji toka kwa viongozi wenzake (sifa, kutambuliwa kama ana mchango mkubwa ndani ya CDM),, hali tunayoiona sasa hivi ni kama kapuuzwa na hakuna tena kiongozi anayemshobokea... Mbowe na Dr Slaa lazima mkumbuke na jukumu kubwa na kuendelea kuwalea vijana wenu na kuwarudisha kwenye mstari ikiwa ni pamoja na kuwapa majukumu (madaraka) na sio vyeo visivyokuwa na madaraka. Kwa mtizamo wangu na hata ukiangalia Maslow's pyramid Zito anaipenda CDM ila amechoka na hana shida ya hela au mali anachokitaka ni kutambuliwa, kuthaminiwa na kupewa madaraka..
Zito kumbuka una nafasi kubwa zaidi ya kukua ndani ya chadema na kufikia kilele cha mafanikio kama utaweza kujirekebisha na ukafanya kazi kama team na hata pale unapokuwa na tofauti na viongozi wenzako ni busara kusubiri vikao na mkalijadili humo kuliko kutoka na mismamo binafsi kama ya mwenzako sitta na kuwafanya wengine kwenye chama waonekane hawajui nini wanachofanya...
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.
Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.
Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).
"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.
Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.
Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.
Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.
Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.
Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.
Source: Majira
Mtu complex hawezi toa maelezo mepesi kiasi hiki,kwan mbunge hawezi kufundisha???!!!!
Si anakaa Dar jimbo lipo Kigoma sasa atashindwa kuishi Mwanza kwenye vyuo na aendelee huko kanda ya ziwa???!!
If this is true ,he should come out clean!!!!!
Kwa uwezo wake na matumaini ya baadhi ya watu juu yake ni sawa na dereva kugomea safari katikati ya msitu!!!!
Aseme safari ngumu.??????
Gari bovu????!
Uwezo wa kuendesha umeshuka??!!!
Konda na tanboi hawampi ushirikiano safarini???!!!!
Nia ilikuwa sio kufika???!!!
Alitaka tu kuonekana akilitoa basi kituoni????!!!!!
Alitaka kuendesha magari katika kampuni ya kimataifa ila ilikiwa ni lazima aendeshe basi kwanza???
Mhhhh: Mkuu, mbona umesha hukumu kabisa hapo?....ngoja tuone ni mapema mno kutoa maneno makali kama hayo....Lazima kutakua na jambo NYETI tu.
Nicholas, tatizo la uchambuzi wa matatizo ya psychology ni kwamba hakuna mzima. naweza nikachambua word selection yako katika argumentation zako nyingi hapa nikakuta wewe pia ni mgonjwa. Kwa hiyo tofauti zetu ni degrees--au pengine niseme viwango vya kuumwa. Hilo linazusha haja ya kuvumiliana katika ubinadamu wetu. Lakini pia ukifanya individual cost-benefit analysis ya hatma ya mwisho ya maamuzi ya mtu ndiyo hupunguza hukumu ya tendo lenye sura ya wehu. Hii ndiyo dhana inayotumiwa kuruhusu vita.
bottom line ya uamuzi wa zitto ni nini kwake at individual level? kwanza ataepuka migogoro ya kisiasa ambayo ni mingi. anataka kazi isiyokuwa na migogoro mingi. anataka amani at individual level. kuna wehu gani katika kutafuta a peaceful life? nadhani ni vizuri ukifuta kauli....usimwite zitto psychopath. hii kauli si sahihi.
Kiongozi we mbaya yani umepoteza kabisa huyo mlamba miguu ya watu (Benn saanane) huyo mwengine hajielewi wala simshangai (yericko) she is nothing kabisa.hawa vijana kweli ndio chanzo kikubwa cha mimi kuichukia CDM kwasababu inawalea vijana wapenda majungu na kufitinisha, hutumia majina ya watu kupata attentionKabisa,
Na kwa kias kikubwa sana CHADEMA kinapitia wakati mgum sana kwa sasa,asilimia kubwa ya vijana sampuli hiyo wamekimbizia matumain kwa CHADEMA moja kwa moja na kuacha kuhangaika kufanya kazi na kutafuta namna ya kujikwamua na utumwa wa fikra,
Wanadhani kama CHADEMA kikiingia madarakani kitakuwa kinawajaza pesa mifukoni,haitafanya hivyo,
Ikiingia Madarakan kwa ridhaa ya wananchi itachofanya ni kusimamia sera zake na kuahid kile kilichokuwa kinasemwa kwa wananchi,
Wao wanadhani kwa kukaa bila kufanya kazi na kushabikia shabikia basi maisha yao yatabadilika once chadema kikichukua inchi,wanashindwa kuelewa maisha ni haya haya,na kila siku watu wanakufa na kuzaliwa,
Tumaini Makene naomba wewe kama msemaji wa chama uchukue jukumu la kuwakemea hawa waganga njaa na wachumia tumbo wanaodhani kukesha kuwalamba lamba miguu viongoz wa juu wa chama basi itawarahishia maisha hapo baadae,
Mfano ni hawa vijana wababishaji na wenye njaa kali kama Yericko & Saa nane,itoke kauli ya uhakika dhidi ya hawa vijana,
Wanajenga taswira mbovu ya chama ili hali hawana influence yyte na by the way hakuna tuh anaewatambua kwa namna yoyote ile,
Wana kua ni taswira ya chama hali ya kuwa wao wana taswira zao binafsi zilizofifia na kukosa matumain,
Waambie wasitegemee kubebewa na taasis,wajenge identity yao,pia waache ufitini na udanganyifu kwa kutumia nembo ya chama,
WANATIA KICHEFU CHEFU
Habari njema kwa Ben maana yeye kila siku anapambana na Zitto ndani ya CDM badala ya kukijenga chama. Naona huyu Ben anatumika sana na Babu kumpaka matope Zitto.
CDM mbaya wenu sio Zitto Bali ni sera zenu za maji taka zisizokuwa na kichwa wala mkono. Cha moto mtakiona came 2015 na hamtaambulia kitu tuombe uzima.
Ukiwa mwanasiasa Tanzania ni lazima kufanya kazi hiyo hadi ugombee/uwe Uraisi/Raisi?
Ukiwa mwanasiasa Tanzania ni lazima kufanya kazi hiyo hadi siku Mungu atakapochukua Roho yako?
Ukiwa mwanasiasa Tanzania ni lazima kufanya kazi hiyo hadi ugombee/uwe Uraisi/Raisi?
Ukiwa mwanasiasa Tanzania ni lazima kufanya kazi hiyo hadi siku Mungu atakapochukua Roho yako?