Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Me kama kijana noma sana,chezea chaga wewe,kila utaemkuta tanzania mzima serekalini au nje lazima awe cdm,shughili zote za katibu mkuu akiondoka anapewa mnyika afanye eti kwasababu ni wa kilimanjaro mpare.
Kwani john mnyika ni mpare?
 
Sina hakika kama kweli zito amefikia maamuzi haya! kama ni kweli nadhani sitakosea nikisema kijana mwenzetu amekurupuka, huko vyuoni anakotaka kukimbilia anakujua vizuri? Ni kweli ameona panamfaa zaidi? Binafsi namuona kama muoga na mtu asiyeaminika, matamshi yake katika siku za karibuni yamekuwa yakijichanganya sana, nashindwa kujua chanzo cha hali hii kwa kijana mwenzetu. Kama ni kuogopa kung'olewa kucha na kumwagiwa tindikali na, au virungu na mabomu ya polisi, basi hafai kuwa mwanasiasa, siasa ni ujasili na kujitoa muhanga mpaka lengo lifikiwe!
 
ni wazi zitto amepima na kuiridhisha kuwa hana mvuto tenma hata kidogo ndani ya siasa za tanzania na ameamua kujitoa mapema.kujihusihsa kwake na hyjuma dhidi ya chama kama vile kufadhili PM79MASALIA) na aina nyingine kama kushawishi wagombea wa cdm kujitoa katika mbio za ubunge 2010 vinatosha kabisa kumueleza kuwa hatakiwi tena.SAFARI NJEMA
 
Zitto umewahi kusikia amekamatwa toka awe mbunge?ni mtu makini siasa sio kufanya maandamano ya sio na msingi wowote Zitto ni msomi hakurupuki na nimzalendo wakweli sema amekosea kwenda chadema
 
Mtu complex hawezi toa maelezo mepesi kiasi hiki,kwan mbunge hawezi kufundisha???!!!!
Si anakaa Dar jimbo lipo Kigoma sasa atashindwa kuishi Mwanza kwenye vyuo na aendelee huko kanda ya ziwa???!!

If this is true ,he should come out clean!!!!!

Kwa uwezo wake na matumaini ya baadhi ya watu juu yake ni sawa na dereva kugomea safari katikati ya msitu!!!!

Aseme safari ngumu.??????
Gari bovu????!
Uwezo wa kuendesha umeshuka??!!!
Konda na tanboi hawampi ushirikiano safarini???!!!!
Nia ilikuwa sio kufika???!!!
Alitaka tu kuonekana akilitoa basi kituoni????!!!!!
Alitaka kuendesha magari katika kampuni ya kimataifa ila ilikiwa ni lazima aendeshe basi kwanza???
ki ukweli CHADOMO wanampaka matope sana huyu mtu lakini mbele ya umma he is miles ahead of you CDM
 
ki ukweli CHADOMO wanampaka matope sana huyu mtu lakini mbele ya umma he is miles ahead of you CDM

Ahead of????ondoa neno you hapo!!!!

Kama he is miles away ndo aoneshe muda ukifika yeye mwenyewe amewaambia msiwaamini wanasiasa sasa wewe hii maneno yako unayotoa hapa unatumia kipimo gani
 
Ahead of????ondoa neno you hapo!!!!

Kama he is miles away ndo aoneshe muda ukifika yeye mwenyewe amewaambia msiwaamini wanasiasa sasa wewe hii maneno yako unayotoa hapa unatumia kipimo gani
ndugu namaanisha nilichoandika na kinaeleweka kama nimekugusa changia kwa busara sio kuwa biased.... CHADEMA is a "legal person" hivyo neno you lipo mahala sahihi......JF ni forum huru kwa watu huru wenye mtazamo huru........., jenga hoja, ushishambulie hoja ya mwenzio...........nyau wewe
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).

"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.

Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.

Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.

Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.

Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.

Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.


Source: Majira
Mnafiki mkubwa ondoka,umetoa siri nyingi za chama,mdini,mshirikina na nchonganishi.ONDOKA HARAKA SANA.
 
mtoto kigeugeu huyu kwanza alishasema hivo hivo 2010
 
CDM watakuja kujua umuhimu wa Zitto baadaye. Zitto ni jembe sana ndani ya CDM Hana siasa za maji taka Kama akina Lissu, Lema na Sugu. Hakuna asiyejua mchango wa Zitto kwa CDM. Hawa vijana akina Lema hawajengi CDM Bali wamekidhoofisha sana chama kwa siasa zao za maji taka. Pumzika kaka pumzika Zitto
amekaririwa kuwa hagombei ubunge au urais na hajasema kama anaachana na siasa au chadema sasa majuto yako wapi hapo?
 
Pole sana Zitto, bado tunakuhitaji kaka.
 
Mbona unapenda kuchokonoa mambo ya ndani ya wazee? sasa unataka aache kwenda na kimwana aende na wewe? Jadili siasa siyo mapenzi,ebo!
 
CDM watakuja kujua umuhimu wa Zitto baadaye. Zitto ni jembe sana ndani ya CDM Hana siasa za maji taka Kama akina Lissu, Lema na Sugu. Hakuna asiyejua mchango wa Zitto kwa CDM. Hawa vijana akina Lema hawajengi CDM Bali wamekidhoofisha sana chama kwa siasa zao za maji taka. Pumzika kaka pumzika Zitto
wew majitaka mwenzake Zitto kakifanyia nini CDM?AU PLATFORM YA CDM IMEMUWEKA HAPO ALIPO?ASSUME CDM HAIPO NANI ZITTO?
 
Bora! au ndo anarudi ze magamba? au ameshaahidiwa 'ukuu wa wilaya'? kwani kazi aliyoifanyia ni kubwa anahitaji kufarijiwa!:rip:
 
"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.
Bado natafakari Waraka wa mabadiliko 2013 kuwa MM ajifanye anaachana na masuala ya kugombea ili kuwapumbaza kina Mbowe.
 
Chadema ni chama ambachokwahakika kiewavuta watu wengi ndani na nje ya nchi.
Kazi hiyo imetokana na hoja zenye mashiko za watu kama zito.mnyika.mdee.mgimwa nk.hatujakipenda chadema kwaajili ya mjina hivyo maamuzi ya jazba hayata kijenga chama bali yatakizorotesha.
 
hilo lilikuwa limeandikwa kwenye waraka sababu kuwafanya viongozi waliopo wabweteke na lingine lilikuwa kuibua mabo ya ruzuku ili wanachama waone viongozi waliopo ni mafisadi ili kujisafishia njia ya kwa mwenyekiti bila kujua anaharibu chama!! Taamaa ya madaraka ni mbaya sana
 
Back
Top Bottom