Zitto: T249 CMV limemteka Nondo, mmiliki ni Deo Beda

Zitto: T249 CMV limemteka Nondo, mmiliki ni Deo Beda

Zitto amesema “Tunataka Abdul Nondo aachiwe mara moja akiwa mzma wa afya, tafadhali sana, gari inadaiwa parking na tumejua kila mahala gari hiyo inapaki, mwacheni Nondo haraka iwezekanavyo Wapumbavu wakubwa nyie”
Juzi zitto katoa hotuba Kali sana. Naona wamemjibu kwamba hutuwezi kitu we Zitto
 
Gari ya Minja ni ist...Hayo magari yao ya utekaji wanaweka namba bandia za magari ya watu nao ni ujinga mwingine wanao kuja nao. Zitto nae kaingia mkenge
Ningeshangaa kwamba watekaji watakuja na Namba Halisi
 
RPC kutembelea gari lenye namba za usajili wa mashirika ya umma SU kama hili huku amevaa uniform za polisi ameongozana na mpambe bodyguard. Ni mtindo unaosababisha Polisi kudai ni gari la watu wasiojulikana ..


View: https://m.youtube.com/watch?v=izpXJFkZQqo

Anapanda gari la shirika la Umma, kuna sheria inakataza mtumishi wa serikali kupanda gari la shirika la umma?

Tujikite kwenye hoja
 
Anapanda gari la shirika la Umma, kuna sheria inakataza mtumishi wa serikali kupanda gari la shirika la umma?

Tujikite kwenye hoja

Kupanda (lifti) ni tofauti, na kutumia gari yenye namba plate usajili SU kufanya shughuli za kipolisi.

Hapo RPC anakuwa mtu asiyejulikana kwa kutumia gari yenye utambulisho usio sahihi.
 
Magufuli alikuwa mpumbavu. Kushangilia kifo chake ilikuwa ni lazima. Mburumundu wewe.

Na hata yanayoendelea sasa muasisi wake ni huyu huyu Magufuli a.k.a jiwe mshamba wa Chato.
Kwa hiyo Magufuli alimteka Dkt Steven Ulimboka?
 
Namba pengine zimetajwa na watu waliokuwa karibu. Hata hivyo ninavyojua mimi ''wasiojulikana'' wakati wanaenda kuteka huweza kuweka namba yoyote wanayotaka. Siyo ajabu ukasikia namba ya gari unayomiliki wewe imetajwa.
Namba ya kusadikika, ila kuna kitu kinanishangaza kidogo, yani hakuna hata raia walijisumbua kufuatilia hiyo gari?

Kweli utekaji umekuwa jambo la kawaida
 
kwa nafasi ya Nondo, hakuwa na msaidizi hakuwa na body guard, anatembea tu ka mbwakoko, kwanafasi yake hakuweza kupata ticket ya ndege? hakuna gari iliyokuja kumpokea? kwanini hakushuka shekilango akaingia kwenye gari yake? muda mwingine tunamwachia maisha yetu mungu kienyeji mno
 
Tunapoelekea sasa kila mmoja atatembea na siraha yake ya kujilinda bora Wamasai walishazoea kutembea nazo za kujilinda
 
Back
Top Bottom