Zitto: Tozo za miamala ziondolewe kwa sababu kuna hela ya IMF

Zitto: Tozo za miamala ziondolewe kwa sababu kuna hela ya IMF

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema tozo za miamala ziliwekwa na serikali katika bajeti ya serikali ya mwaka 2021/2022 ili kuwezesha ujenzi wa madarasa nchini.

Hivi karibu Serikali imepata fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) ambazo zimetangazwa kutumika kujenga vituo na madarasa nchi nzima. Zito ameshauri serikali kuzipunguza au kuziondoa tozo.

Zitto amezungumza hayo akiwa katika mahojiano Times FM
 
Wewe nae ni mpuuzi,kwamba fedha za IMF ndio zitamaliza changamoto ambazo zinatatuliwa kwa fedha ya miamala?

Inajiongelesha kwa sababu umekosa ku trend siku nyingi. Huyo Zito kule kwao Kigoma hadi kesho ni mavumbi matupu,hakuna huduma za afya za maana hadi wamama wanalala wa 2 kwenye vitanda na huduma ziko mbali ..

Wewe Zito utakuwa ni mjinga Sana kwa sababu unaishi Mjini huna hata huruma na watu wa Vijijini.
 
Zitto nae low thinker, hili wazo butu kabisa. Tozo ni nzuri sana na itaisaidia sana serikali kutatua matatizo yetu kwa kiwango kikubwa sana sanaaa, wazungu sio watu wa kuwategemea kila siku. Tozo ni endelevu, but IMF money is one time.

Hili wazo la hovyo kabisa just to get political cheap popularity.
 
Walitwambia sijui zitajenga madarasa, sahizi wanasema pesa za huko kwa mabeberu ndiyo zitajenga swali pesa za tozo zi wapi?????
 
Tusi-attack Personality.., tuongelee issue at hand...

Kama tozo ni Maumivu..., na haya maumivu watu waliambiwa wavumilia ili kukamilisha jambo fulani (yaani short time pain for long term gain).... Sasa kama hilo jambo limekamilishwa kwa njia nyingine kwanini maumivu yaendelee ?

Au haya maumivu ndio yatakuwa ya milele ?, Ukizingatia Maumivu haya yamepunguza transactions na ufanisi, kwahiyo in short hayakuwa na Tija na pesa hizo zingeweza patikana kwenye vyanzo vingine bila kuathiri watu kufanya miamala
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema tozo za miamala ziliwekwa na serikali katika bajeti ya serikali ya mwaka 2021/2022 ili kuwezesha ujenzi wa madarasa nchini.

Hivi karibu Serikali imepata fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) ambazo zimetangazwa kutumika kujenga vituo na madarasa nchi nzima. Zito ameshauri serikali kuzipunguza au kuziondoa tozo.

Zitto amezungumza hayo akiwa katika mahojiano Times FM
Kwa ufupi kabisa na bila kupoteza muda wenu nasema - huu ni mfano halisi na hai wa MAWAZO TEGEMEZI!
 
Ukiandika ujinga wako wa kupotosha utajibiwa,afu sikariri id za watu na deal na content..

We kwa ujinga wako unaona ni sawa serikali isitishe tozo eti kuna hela ya IMF,una akili timamu kweli wewe?
Nini Kazi ya Tozo?

Kwahio ukijinyima ili umalizie nyumba yako.., lakini ukapata pesa sehemu ya kumalizia nyumba utaendelea kujinyima ?, Je ukifa kwa Kwashiakooo ni nani atafaidika na nyumba yako?
 
Ukiandika ujinga wako wa kupotosha utajibiwa,afu sikariri id za watu na deal na content..

We kwa ujinga wako unaona ni sawa serikali isitishe tozo eti kuna hela ya IMF,una akili timamu kweli wewe?
Hilo la "kusitisha" lina uhusiano gani na huko atokeapo Zitto, kama ulivyokueleza na kumlaumu yeye kana kwamba ndiye hufuja hela zinazopelekwa huko kwao!

Unapokuwa na akili ya tope huwezi kutambua "content" kama unavyodai hapa. Sihitaji "kukariri" kujua nani hutoa 'content' gani, ni sehemu ya ufahamu (comprehension) ya hiyo 'content'. Kama wewe siku zote 'content' zako ni za kipuuzi, utafahamika kwa hali hiyo.
 
Kwa hiyo tozo zinaenda kujenga choo ya Mwigulu au? Acha upumbavu,kama huoni inavyohusiana Baki hivyo hivyo na ujinga wako.
 
Back
Top Bottom