Zitto: Tozo za miamala ziondolewe kwa sababu kuna hela ya IMF

Zitto: Tozo za miamala ziondolewe kwa sababu kuna hela ya IMF

Wangapi wamelipa Kodi kwa miaka 60?..unadhani mzungu atakupa hela ya kukufanya uendelee?..rasilimali tunazo,uwezo was kukufanya zitupe Tina tunao?...ifike mahali tione aibu kuomba na tuchangie kuikwamua nchi yetu
Kuna mtumiaji asiyelipa Kodi ?

Angalia Risiti yako kila ukinunua bidhaa..., unadhani zile VAT n.k. ni Mapambo ?, Unadhani bila kodi bidhaa zingekuwa bei ambayo ipo ?
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema tozo za miamala ziliwekwa na serikali katika bajeti ya serikali ya mwaka 2021/2022 ili kuwezesha ujenzi wa madarasa nchini.

Hivi karibu Serikali imepata fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) ambazo zimetangazwa kutumika kujenga vituo na madarasa nchi nzima. Zito ameshauri serikali kuzipunguza au kuziondoa tozo.

Zitto amezungumza hayo akiwa katika mahojiano Times FM
Kwa hili nakuunga mkono Zitto, jana nimesikiliza hotuba ya raisi Uhuru Kenyata wa Kenya wakati wa kuadhimisha siku ya Mashujaa, nimefurahishwa sana na hotuba ya Uhuru kwanza kwa kutumia hiyo pesa ya Covid kutoka kwenye mashirika ya Kimataifa wameweza kujenga mahosipitali na kuboresha miundo mbinu, katika kitu atakachokumbukwa Uhuru ni ujenzi wa miundo mbinu nchini humo ni kama vile alivyofanya mwendazake hapa nchini, miundombinu hasa barabara ndio uti wa mgongo wa taifa lolote lile ili liendelee, pia kwa kutumia pesa hiyo hiyo ya UVIKO Uhuru amesema anataka kuwapunguzia mzigo wa maisha wa Wakenya kutokana na mdororo wa kiuchumi kwa kupunguza gharama za umeme, kurudisha tena ''ajira kwa vijana'' na kuamuru benki kupunguza riba kwa wakopaji ,pia kutakuwa na mifuko ya kusaidia kupunguza bei za pembejeo kwa wakulima, huyo ndio raisi bana, hatujasikia kuwa sasa anaanzisha tozo za ajabu ajabu. Huu ni wakati kama kweli mnaona UVIKO ipo na hali ya kiuchumi kwa wananchi imekuwa mbaya basi ili kutusaidia muondoe hayo MATOZO yasiyo na tija katika ustawi wa mwananchi wa kawaida, kutegemea tozo kwenye simu kuleta maendeleo ni moja kwanza kumkwamisha mwananchi wa kawaida lakini pia ni vigumu kupata maendeleo kama nchi kwa kutegemea tozo za miamala. Mwaka 2025 uwe ni mwaka wa kurudisha vichwa vingi kutoka upinzani kama akina Zitto na wengineo,kwa hali hii inabidi nianze kufikiria kubadili gia angani juu ya mtizamo wangu wa kisiasa!
 
Madini, Utalii, Nchi Kubwa, Kilimo vyote ni nini kama sio vyanzo ?

Kama waliopo madarakani wanshindwa kutumia hivyo vyanzo ili kuweka sawa maisha ya mtanzania huenda kuwepo kwao hapo ni makosa
Wewe una akili kuliko wote waliowahi kuwa madarakani?
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema tozo za miamala ziliwekwa na serikali katika bajeti ya serikali ya mwaka 2021/2022 ili kuwezesha ujenzi wa madarasa nchini.

Hivi karibu Serikali imepata fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) ambazo zimetangazwa kutumika kujenga vituo na madarasa nchi nzima. Zito ameshauri serikali kuzipunguza au kuziondoa tozo.

Zitto amezungumza hayo akiwa katika mahojiano Times FM
Kukopa ni utumwa. Tozo ziendelee mpaka kieleweke. Acha wapinzani wapate agenda.
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema tozo za miamala ziliwekwa na serikali katika bajeti ya serikali ya mwaka 2021/2022 ili kuwezesha ujenzi wa madarasa nchini.

Hivi karibu Serikali imepata fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) ambazo zimetangazwa kutumika kujenga vituo na madarasa nchi nzima. Zito ameshauri serikali kuzipunguza au kuziondoa tozo.

Zitto amezungumza hayo akiwa katika mahojiano Times FM
Ni kweli anachosema Zitto, mkopo wa IFM ni wa mara moja, ila hizi tozo zikiendela kwa muda na usimamizi ukawa mzuri zitatusaidia kwenye mambo mengi, mengineyo mfano ni Bima ya Afya kwa wote
 
Wewe nae ni mpuuzi,kwamba fedha za IMF ndio zitamaliza changamoto ambazo zinatatuliwa kwa fedha ya miamala?

Inajiongelesha kwa sababu umekosa ku trend siku nyingi. Huyo Zito kule kwao Kigoma hadi kesho ni mavumbi matupu,hakuna huduma za afya za maana hadi wamama wanalala wa 2 kwenye vitanda na huduma ziko mbali ..

Wewe Zito utakuwa ni mjinga Sana kwa sababu unaishi Mjini huna hata huruma na watu wa Vijijini.
Miaka 60 ya uhuru unamlaumu huyo Zitto kwamba ndio amekuwa akiitawala hii nchi na kushindwa kushughulikia hayo, au tukueleweje sijui.

Assume kwamba COVID-19 isingekuwepo hayo mambo wangeya shughuliaje?
 
Hakuna asiyetaka kulipa Kodi. Ila kabla hilo halijaanza kuanze uwajibishaji viongozi wote wanaofuja kodi zetu. Haiwezekani nihangaikie kulipa Kodi halafu mijitu inalipana mamia ya mamilioni, na bado hawatosheki wanafanya ufisadi kila kona.

Wapunguze matumizi ya serikali, kuwe na uwazi wa hela zote zinatumika vipi then tukifika hapo tulazimishane kulipa Kodi.

Kulipa tu Kodi kibubusa ni kuwanufaisha wachache wakati mamilioni ya watanzania Kodi zao haziwafaidishi ipasavyo.
Hilo ndio tatizo! Tozo zetu inabidi tuweze kuziona daily tumechangia bei gani kwa uwazi na matumizi yake yawe documented!

Maswala ya kulipishana tozo halafu waziri flani na genge lake wanadokoa hela na kuamua kuanzisha kampuni ya usafirishaji kimya kimya sio ambayo tunataka!
 
Kuna mtumiaji asiyelipa Kodi ?

Angalia Risiti yako kila ukinunua bidhaa..., unadhani zile VAT n.k. ni Mapambo ?, Unadhani bila kodi bidhaa zingekuwa bei ambayo ipo ?
Bila Kodi hakuna serikali,lakini Tanzania una shida ya mikono mingi kwenye sahani moja,yaani wategemezi ni wengi,kwa hyo wengi hawalipi kodi
 
Bila Kodi hakuna serikali,lakini Tanzania una shida ya mikono mingi kwenye sahani moja,yaani wategemezi ni wengi,kwa hyo wengi hawalipi kodi
Hata unaodhani hawalipi Kodi wanalipa..., Kila bidhaa unazonunua zina kodi lukuki ndani yake, Usafiri kuna Kodi, Bidhaa Ukinunua kuna Kodi..., achilia mbali hizo nyingine...

Hata kama bila kutoa pesa watu waliopo migodini huko mazingira yao na vyanzo vya maji vinachafuliwa na uchimbaji nazo ni kodi kwao....
 
Una elimu duni ya fedha na uchumi
 
Una elimu duni ya fedha na uchumi
Naam huenda ni ukweli usemayo lakini niambie ni kiumbe gani hapa nchini anaweza akakwepa Indirect Taxes ?, Unavyosema watanzania hawalipi Kodi nimekuuliza ni mnunuzi gani asiyelipa Kodi ? Hata asipokatwa kwenye Income Tax atakatwa kwenye Consumption Taxes...

Pili kwa hio migodi inayopatia taifa mapesa ya kumwaga unadhani waliopo kwenye maeneo hayo na kusumbuliwa na uchafuzi huo (hio impact ya afya yao na gharama is a higher price to pay) kuliko hata hio mirahaba wanaotoa hao wachimbaji... (Mkazi huyu anayekongoroka afya ananufaika vipi )?
 
Nimekwambia Tanzania una shida ya mikono mingi kwenye sahani moja,yaani mhemeaji mmoja anabeba kundi kubwa,anaelipa Kodi hapa no mhemeaji,watoto waliomaliza vyuo na hawana ajira wakika kwa wazazi na ndugu ni wengi,Hawa hawalipi kodi
 
Back
Top Bottom