Zitto: Umeme wa Gesi ungezalisha MW 3,500 zaidi ya wa Maji

MPUNGA MMOJA

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
304
Reaction score
401
Uchambuzi wa ripoti ya CAG ulofanywa na chama cha ACT WAZALENDO inasema tulidharau na kuutupa mradi wa umeme wa gesi ambao tulishakopa fedha China wenye wenye uwezo wa kuzalisha MW 3500 tukakimbilia mradi mpya wa umeme wa Maji wenye kutoa MW 2110 kwa gharama ya Tillioni 6 matokeo yake tumekopa madeni mara mbili kwenye lengo moja.
 
Hiyo gesi anamiliki nani, na bei ya huo umeme ingekuwa kiasi gani?
 
Tukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.

Uliona wapi kiongozi anamfukuza mfanyakazi mwenye mkataba wa kazi kwa kuwauliza watu waliopo kwenye mkutano, 'Nimtumbue sasa hivi au nimwache?; Wananzengo nao wanajibu, "tumbua"; halafu mfalme anasema, "Kabwe, nimekwishakutumbua". Kweli unaamini huyo ni kiongozi anayeweza kutafakari kabla ya maamuzi?
 
Gas hapana, labda kama ingekuwa serikali ndo wanachimba wenyewe!

Nitapinga wote wanaopiga kelele za umeme wa gas! Sababu kubwa ikiwa gas inachimbwaa na makampuni binafsi tena ya nje! Wao ndo wanapanga bei gani wauzie Tanesco! Tanesco hawatakuwa na control na huu umeme kwa hiyo wananchi tutauziwa kwa bei ya juu sana.

Hii itasababisha maisha kuwa ya gharama zaidi!

Afadhali HEP ambayo less costly, na unazalishwa na serikali ambayo watakuwa na direct control. So mwananchi hataumia sana.

Tunampinga Magufuli kwa mambo mengi ila kwa hili la Bwawa la Nyerere tupige kelele kwa kila mmoja mradi uendelee kwa 100%.

Hii project iendelee
 
Yaani Tanzania karibu miaka ishirini yote nasikia tu mradi wa umeme mradi wa umeme yaani hakuna anaefanikiwa akija huyu na mwingine anakuja na wake utadhani wanajenga nyumba tofauti...sema yule jamaa katupeleka chaka mno
Halafu kila siku mgao wa umeme hauishi. Utaskia mara kunguru wanalaumiwa kwa kusababisha umeme kukatika.

Wakati madeni ya taifa yanazidi kuongezeka. Na Raia tukapigwa marufuku kuhoji wala kuuliza chochote.
tapatalk_1581751612769.jpg
 
Yaani Tanzania karibu miaka ishirini yote nasikia tu mradi wa umeme mradi wa umeme yaani hakuna anaefanikiwa akija huyu na mwingine anakuja na wake utadhani wanajenga nyumba tofauti...sema yule jamaa katupeleka chaka mno
Pamoja na mapungufu yake na foul zake, mimi sijawahi kuwa shabiki wa Hayati, ila alikua na uthubutu, kuna vitu ambavyo tunakumbana navyo hata maishani unakuta una mambo mengi yanataka pesa ila hazitoshi, inabidi ujivalishe bom kufanya unayohisi yenye manufaa kwa vizazi vijavyo.

Bwawa la umeme bado ni chaguo bora kabisa hawa wanasiasa wanakaa na report siku nne anakuja kutoa hitimisho la mradi unatekelezwa na maelfu ya wataaalam.
 
Gas hapana, labda kama ingekuwa serikali ndo wanachimba wenyewe!

Nitapinga wote wanaopiga kelele za umeme wa gas! Sababu kubwa ikiwa gas inachimbwaa na makampuni binafsi tena ya nje! Wao ndo wanapanga bei gani wauzie Tanesco! Tanesco hawatakuwa na control na huu umeme kwa hiyo wananchi tutauziwa kwa bei ya juu sana.

Hii itasababisha maisha kuwa ya gharama zaidi!

Afadhali HEP ambayo less costly, na unazalishwa na serikali ambayo watakuwa na direct control. So mwananchi hataumia sana.

Tunampinga Magufuli kwa mambo mengi ila kwa hili la Bwawa la Nyerere tupige kelele kwa kila mmoja mradi uendelee kwa 100%.

Hii project iendelee
Naunga mkono hoja, moja ya kitu nilichokuwa namuunga mkono jpm ni Hilo bwawa
 
"Zitto: Umeme wa gesi ungezalisha mw 3,500 zaidi ya wa maji"

Haya nayo ni maajabu, kama watu wanaotarajiwa kuwa na akili timamu nao wanakuwa viherehere namna hii.

Hivi kuna kitu gani kinachosumbua hawa watu?

Kwani baada ya kupata hizo mw 2,000 za maji ndio utakuwa mwisho wa mahitaji ya umeme kwa Tanzania?

Hizo 3,500 za gesi haziwezi kuzalishwa na gesi mahitaji yatakavyozidi kuwa yanaongezeka?

Mi nadhani huenda waleta mada wanawalisha maneno ambayo hawakuyatamka baadhi ya hawa viongozi; lakini kama nikweli wameyatamka, basi kuna hitilafu kubwa sana na wanasiasa wa nchi hii.
 
Hii project iendelee
Hakuna mwenye makende (balls) ya kuzuia au kuingilia mradi huo tena. Kama hilo ndilo wanalolitafuta litawamaliza wao kisiasa, kama sio kimaisha.
Gas hapana, labda kama ingekuwa serikali ndo wanachimba wenyewe!

Nitapinga wote wanaopiga kelele za umeme wa gas! Sababu kubwa ikiwa gas inachimbwaa na makampuni binafsi tena ya nje! Wao ndo wanapanga bei gani wauzie Tanesco! Tanesco hawatakuwa na control na huu umeme kwa hiyo wananchi tutauziwa kwa bei ya juu sana.
Umebainisha vyema sana nia hasa ya hawa watu inakotokea.

Hii gesi isichimbwe kwa sasa kwa sababu naona kuna mafisi wakubwa sana wakizongazonga kama Tanzania umekuwa mzoga.
 
Pamoja na mapungufu yake na foul zake, mimi sijawahi kuwa shabiki wa Hayati, ila alikua na uthubutu, kuna vitu ambavyo tunakumbana navyo hata maishani unakuta una mambo mengi yanataka pesa ila hazitoshi, inabidi ujivalishe bom kufanya unayohisi yenye manufaa kwa vizazi vijavyo.

Bwawa la umeme bado ni chaguo bora kabisa hawa wanasiasa wanakaa na report siku nne anakuja kutoa hitimisho la mradi unatekelezwa na maelfu ya wataaalam.
JNHPP ni bora ukilinganisha na njia ya pili ambayo tayari kina JK walikua wameshaingia chaka..Mimi hapa hata ubaya wote(unaosemekana) kufanya namuunga mkono

Tatizo langu ni jinsi alivyokua Anafanya miradi hiyo. Kama vile anashindana na watu Fulani/wananchi anajaribu kuprove wrong,matokeo yake aliingia kwa haraka bila utafiti wa kimazingira na kifedha

Na mwisho wake tunaona sasa mradi umemaliza hela zote mtaani na una hatihati ya kutoka milima na pia mrad unatekelezwa kwa feasibility study ya mwaka 1970. Yaaani kama haya ni kweli na ule mradi utashindikana,ntaumiq sana mimi kwakua itakua ni muda wa kupigwa vizuri sasa na hawa wa ges. Na hasara kwa vizazi na vizazi

Vyovyote iwavyo hakuna mtu atanibadilisha msimamo wangu kuwa jamaa alikua ana mapenzi sana na malengo makubwa juu ya Tanzania,ila mawazo yalikua kichwani make,kuyabadili kuyatenda hilo ni swala la debate na tutamjadili kwa toka sasa na vizazi na vizazi
 
Swala si uwingi wa MW pekee, ni kuangalia maisha ya huo mradi, na uendeshaji wake, je ikiwa ni 10000 MW na mwananchi akauziwa 2000 kwa unit, ukombozi kwa mwananchi utakuwa wapi?
Kwangu Mimi swala sio wingi wa MW wala gharama atakayouziwa mwananchi, Mimi najiuliza tu ni kina nani wapitisha mradi wa gesi? Walikuwa waburundi? Waliokuja kuuweka pending je wanatoka nchi gani? Sio watanzania?

Magufuri alikuwepo kwenye baraza la Mawaziri lililopitisha mradi wa gesi, amekuja kuwa Rais akaja na bwawa la Nyerere! Wataalum hao hao waliopitisha gesi ndo hao hao walipigia chapuo bwawa la Nyerere

Shida yangu kubwa iko kwa aina ya viongozi na wataalum tulionao sijui wakoje

Watu makini hawawezi kupitisha vitu kwa kukurupuka! Kama nchi lazima iwe na plan ambayo hata aje nani atalazimika kuitekeleza. Hapa tutatofautiana speed tu!

Haiwezekani eti nchi ina wataalum wanakaa vikao wanajadili na kukubaliana kwamba "Tanzania tunahamia kwenye umeme wa gesi" halafu miaka kadhaa mbele wanasema " Hapana, turudi kwenye bwawa"

Miradi mikubwa Kama hii haitakiwi kuamuliwa kwa mihemuko wala mashindano!

Sina shida na mradi upi ni Bora, shida yangu kwanini wataalum hawako stable kufanya maamuzi
 
Tukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.

Uliona wapi kiongozi anamfukuza mfanyakazi mwenye mkataba wa kazi kwa kuwauliza watu waliopo kwenye mkutano, 'Nimtumbue sasa hivi au nimwache?; Wananzengo nao wanajibu, "tumbua"; halafu mfalme anasema, "Kabwe, nimekwishakutumbua". Kweli unaamini huyo ni kiongozi anayeweza kutafakari kabla ya maamuzi?
Humjui ZITTO period!
 
Tatizo hiyo miradi mikubwa ya jiwe imeghubikwa na usiri na ukurupukaji mkubwa, nafikiri alilenga kupiga 10% zake mapema kabla hajaondoka. Huwezi kutekeleza miradi mikubwa mitano at per kwa nchi kama Tanzania, utaishia kukandamiza maslahi ya watumishi, kupora pesa za wafanyabiashara nk. ili lengo lako ovu litimie huku wewe na genge lako mkiwa mmejilundukia utajiri wa kutisha ukiwaacha asilimia kubwa ya wananchi na maumivu makubwa ya kimaisha....
 
nimemsikiliza akijumlisha 40,80 halafu 150 halafu 300 jumla akaja na figure ya 3500
Mbona siku hizi ninakubaliana kwa mengi nawe?
Kumetokea kitu gani kilichobadilika?

Hizo 40 + 80 + 150 + 300...; ni vikampuni vya mfukoni walivyoshirikishwa navyo akina Kabwe, hiyo ndiyo maana yake.

Hawa watu wanatafuta kutuletea yanayotokea Kenya hapa. Sijui wanaona ni kipi kizuri huko.
 
Tukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.

Uliona wapi kiongozi anamfukuza mfanyakazi mwenye mkataba wa kazi kwa kuwauliza watu waliopo kwenye mkutano, 'Nimtumbue sasa hivi au nimwache?; Wananzengo nao wanajibu, "tumbua"; halafu mfalme anasema, "Kabwe, nimekwishakutumbua". Kweli unaamini huyo ni kiongozi anayeweza kutafakari kabla ya maamuzi?
Ni kweli
 
JNHPP ni bora ukilinganisha na njia ya pili ambayo tayari kina JK walikua wameshaingia chaka..Mimi hapa hata ubaya wote(unaosemekana) kufanya namuunga mkono

Tatizo langu ni jinsi alivyokua Anafanya miradi hiyo. Kama vile anashindana na watu Fulani/wananchi anajaribu kuprove wrong,matokeo yake aliingia kwa haraka bila utafiti wa kimazingira na kifedha

Na mwisho wake tunaona sasa mradi umemaliza hela zote mtaani na una hatihati ya kutoka milima na pia mrad unatekelezwa kwa feasibility study ya mwaka 1970. Yaaani kama haya ni kweli na ule mradi utashindikana,ntaumiq sana mimi kwakua itakua ni muda wa kupigwa vizuri sasa na hawa wa ges. Na hasara kwa vizazi na vizazi

Vyovyote iwavyo hakuna mtu atanibadilisha msimamo wangu kuwa jamaa alikua ana mapenzi sana na malengo makubwa juu ya Tanzania,ila mawazo yalikua kichwani make,kuyabadili kuyatenda hilo ni swala la debate na tutamjadili kwa toka sasa na vizazi na vizazi
Kama mradi una feasibility studies ya miaka 70s, je bwawa linaendana kama fasheni za nguo? Kama bwawa linaendana kifasheni kwanini tunaendelea kutumia KIDATU?
 
Back
Top Bottom