MPUNGA MMOJA
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 304
- 401
Hiyo gesi anamiliki nani, na bei ya huo umeme ingekuwa kiasi gani?Uchambuzi wa ripoti ya CAG ulofanywa na chama cha ACT WAZALENDO inasema tulidharau na kuutupa mradi wa umeme wa gesi ambao tulishakopa fedha China wenye wenye uwezo wa kuzalisha MW 3500 tukakimbilia mradi mpya wa umeme wa Maji wenye kutoa MW 2110 kwa gharama ya Tillioni 6 matokeo yake tumekopa madeni mara mbili kwenye lengo moja.
Tukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.Hiyo gesi anamiliki nani, na bei ya huo umeme ingekuwa kiasi gani?
Halafu kila siku mgao wa umeme hauishi. Utaskia mara kunguru wanalaumiwa kwa kusababisha umeme kukatika.Yaani Tanzania karibu miaka ishirini yote nasikia tu mradi wa umeme mradi wa umeme yaani hakuna anaefanikiwa akija huyu na mwingine anakuja na wake utadhani wanajenga nyumba tofauti...sema yule jamaa katupeleka chaka mno
Pamoja na mapungufu yake na foul zake, mimi sijawahi kuwa shabiki wa Hayati, ila alikua na uthubutu, kuna vitu ambavyo tunakumbana navyo hata maishani unakuta una mambo mengi yanataka pesa ila hazitoshi, inabidi ujivalishe bom kufanya unayohisi yenye manufaa kwa vizazi vijavyo.Yaani Tanzania karibu miaka ishirini yote nasikia tu mradi wa umeme mradi wa umeme yaani hakuna anaefanikiwa akija huyu na mwingine anakuja na wake utadhani wanajenga nyumba tofauti...sema yule jamaa katupeleka chaka mno
Naunga mkono hoja, moja ya kitu nilichokuwa namuunga mkono jpm ni Hilo bwawaGas hapana, labda kama ingekuwa serikali ndo wanachimba wenyewe!
Nitapinga wote wanaopiga kelele za umeme wa gas! Sababu kubwa ikiwa gas inachimbwaa na makampuni binafsi tena ya nje! Wao ndo wanapanga bei gani wauzie Tanesco! Tanesco hawatakuwa na control na huu umeme kwa hiyo wananchi tutauziwa kwa bei ya juu sana.
Hii itasababisha maisha kuwa ya gharama zaidi!
Afadhali HEP ambayo less costly, na unazalishwa na serikali ambayo watakuwa na direct control. So mwananchi hataumia sana.
Tunampinga Magufuli kwa mambo mengi ila kwa hili la Bwawa la Nyerere tupige kelele kwa kila mmoja mradi uendelee kwa 100%.
Hii project iendelee
Hakuna mwenye makende (balls) ya kuzuia au kuingilia mradi huo tena. Kama hilo ndilo wanalolitafuta litawamaliza wao kisiasa, kama sio kimaisha.Hii project iendelee
Umebainisha vyema sana nia hasa ya hawa watu inakotokea.Gas hapana, labda kama ingekuwa serikali ndo wanachimba wenyewe!
Nitapinga wote wanaopiga kelele za umeme wa gas! Sababu kubwa ikiwa gas inachimbwaa na makampuni binafsi tena ya nje! Wao ndo wanapanga bei gani wauzie Tanesco! Tanesco hawatakuwa na control na huu umeme kwa hiyo wananchi tutauziwa kwa bei ya juu sana.
JNHPP ni bora ukilinganisha na njia ya pili ambayo tayari kina JK walikua wameshaingia chaka..Mimi hapa hata ubaya wote(unaosemekana) kufanya namuunga mkonoPamoja na mapungufu yake na foul zake, mimi sijawahi kuwa shabiki wa Hayati, ila alikua na uthubutu, kuna vitu ambavyo tunakumbana navyo hata maishani unakuta una mambo mengi yanataka pesa ila hazitoshi, inabidi ujivalishe bom kufanya unayohisi yenye manufaa kwa vizazi vijavyo.
Bwawa la umeme bado ni chaguo bora kabisa hawa wanasiasa wanakaa na report siku nne anakuja kutoa hitimisho la mradi unatekelezwa na maelfu ya wataaalam.
Kwangu Mimi swala sio wingi wa MW wala gharama atakayouziwa mwananchi, Mimi najiuliza tu ni kina nani wapitisha mradi wa gesi? Walikuwa waburundi? Waliokuja kuuweka pending je wanatoka nchi gani? Sio watanzania?Swala si uwingi wa MW pekee, ni kuangalia maisha ya huo mradi, na uendeshaji wake, je ikiwa ni 10000 MW na mwananchi akauziwa 2000 kwa unit, ukombozi kwa mwananchi utakuwa wapi?
Humjui ZITTO period!Tukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.
Uliona wapi kiongozi anamfukuza mfanyakazi mwenye mkataba wa kazi kwa kuwauliza watu waliopo kwenye mkutano, 'Nimtumbue sasa hivi au nimwache?; Wananzengo nao wanajibu, "tumbua"; halafu mfalme anasema, "Kabwe, nimekwishakutumbua". Kweli unaamini huyo ni kiongozi anayeweza kutafakari kabla ya maamuzi?
Mbona siku hizi ninakubaliana kwa mengi nawe?nimemsikiliza akijumlisha 40,80 halafu 150 halafu 300 jumla akaja na figure ya 3500
Ni kweliTukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.
Uliona wapi kiongozi anamfukuza mfanyakazi mwenye mkataba wa kazi kwa kuwauliza watu waliopo kwenye mkutano, 'Nimtumbue sasa hivi au nimwache?; Wananzengo nao wanajibu, "tumbua"; halafu mfalme anasema, "Kabwe, nimekwishakutumbua". Kweli unaamini huyo ni kiongozi anayeweza kutafakari kabla ya maamuzi?
Kama mradi una feasibility studies ya miaka 70s, je bwawa linaendana kama fasheni za nguo? Kama bwawa linaendana kifasheni kwanini tunaendelea kutumia KIDATU?JNHPP ni bora ukilinganisha na njia ya pili ambayo tayari kina JK walikua wameshaingia chaka..Mimi hapa hata ubaya wote(unaosemekana) kufanya namuunga mkono
Tatizo langu ni jinsi alivyokua Anafanya miradi hiyo. Kama vile anashindana na watu Fulani/wananchi anajaribu kuprove wrong,matokeo yake aliingia kwa haraka bila utafiti wa kimazingira na kifedha
Na mwisho wake tunaona sasa mradi umemaliza hela zote mtaani na una hatihati ya kutoka milima na pia mrad unatekelezwa kwa feasibility study ya mwaka 1970. Yaaani kama haya ni kweli na ule mradi utashindikana,ntaumiq sana mimi kwakua itakua ni muda wa kupigwa vizuri sasa na hawa wa ges. Na hasara kwa vizazi na vizazi
Vyovyote iwavyo hakuna mtu atanibadilisha msimamo wangu kuwa jamaa alikua ana mapenzi sana na malengo makubwa juu ya Tanzania,ila mawazo yalikua kichwani make,kuyabadili kuyatenda hilo ni swala la debate na tutamjadili kwa toka sasa na vizazi na vizazi