Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

Uchaguzi 2020 Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

Tulikua tunasubiri figisu za nec na ccm maana kimsingi ilikua Lissu akipitishwa basi membe harudishi form kwa hiyo saaizi ni kwamba membe hatafanya kampeni kujinadi yeye bali atamnadi Tundu Lissu.....

Wamecheza lkn bado wamefeeli
 
Tulikua tunasubiri figisu za nec na ccm maana kimsingi ilikua Lissu akipitishwa basi membe harudishi form kwa hiyo saaizi ni kwamba membe hatafanya kampeni kujinadi yeye bali atamnadi Tundu Lissu.....

Wamecheza lkn bado wamefeeli
Una roho ngumu sana, wewe hata motoni unaweza kuishi!
 
Hilo halikubaliki kisheria kama hamjaungana. Kwa sasa hilo haliwezekani. Kinachowezekana kwa sasa ni kuachiana majimbo bila vyama kushare jukwaa moja.
Muungano wa shetani huwa haudumu
 
Pendekezo la watanzania wengi ni kuona Membe akimpa support Lissu!! pia CDM nao kwa umoja wao wakimpa Support Maalim kule Zanzibar.
Sisi Watanzania tulio wengi tunataka KAZI NA BATA hizi mbwembwe zingine tunajua haziwezi kuchomoa
BM atabomoa ngome ya ccm maana ana watu huko kuanzia system na Makada werevu.

Huyu TL tamanio langu agombee Ubunge Ikungi ili bunge liwe na makali, akigombea Urais atakosa naubunge asipate, labda kwa huruma za ubunge wa kuteuliwa
 
Zitto ana unafiki ndani yake. Ilitakiwa kabla ya wagombea wa vyama hawajapendekezwa ndio atoe hilo pendekezo lake lakini walikaa kimya. Muda wa kampeni umefika ndio anasema wapinzani waungane. Ni uhuni na ubinafsi ndani yake. Kuna game linataka kuchezwa hapa.
Zitto anachosema ni kweli tupu, hivi vyama maslahi sheeda. Chadema wanajiita permanent kambi ya upinzani bungeni
 
Mi nataka kuuliza kitu.

Kwani mambo ya sheria yanasemaje ikiwa vyama vitaunganisha matokeo yao baada ya mshindi kutangazwa? Mfano kama vile enzi zile Zanzibar ZNP na ZPP walipoungana?
 
Zitto anasema watanzania hawatatusamehe
Lissu kwa maneno yake na vitendo vyake anashindana Magu na CCM kwa ujumla kwenye huu uchaguzi. Chadema wengine waliobaki wanapambana na ACT kuwa nani ni mpinzani zaidi ya mwenzake na ataunda kambi ya upinzani hiyo 2020. Patamu hapo. Yetu macho.
 
Ni wakati sasa wa ACT na Membe kutangaza kuunga juhudi za Lisu.
 
Tz tunatakiwa tubakie na vyama vifuatavyo; NCCR, ACT, CCM, na CDM.

Na itapendeza vyama hivyo vikiwa na nguvu zinazokaribiana.

Tukibakiwa na vyama viwili, siasa zetu zitakuwa kama za Zanzibar ambapo kuna mkwamo.

Nchi hii ni kubwa na ina watu wengi, hivyo inaweza ku-accomodate vyama zaidi ya viwili au vitatu vya siasa.
1598537464310.jpeg
 
Ni kweli Muungano wa Upinzani ni muhimu jana leo na kesho ila ni lazima kujua ni aina gani ya Muungano ambao hautaruhusu wenye nia mbaya (wasio wapinzani na "hata wapinzani wenyewe") kupenyeza usaliti na magomvi ndani ya muungano huo kwa mbinu anuwai. Kwangu mimi muungano dhabiti wa Watanzania wapinzani na hata wale wasio wapinzan, pamoja na wasio na upande, ni kujikusanya sote nyuma ya Mwana wa Afrika na Mzalendo Tundu Antipas Lissu chini ya CHADEMA; hiyo ni kwa upande wa Bara. Kwa upande wa Visiwani sote kwa umoja huo huo tujikusanye nyuma ya Jemedari wetu Maalimu Sefu chini ya ACT wazalendo.
 
Zito nae buana😁😁, haya mambo walitakiwa kuyamaliza huko vikaoni na wapinzani wenzie wakubaliane kabisaaa sio kuja kuleta wazo ambalo halijajadiliwa kwa wapiga kura.
Aache ujanjaujanja wa siasa za kitapeli na kisanii. Akae akijua hata waungane hawashindiii Tanzania ya leo ni ya John Pombe Magufuli
 
Back
Top Bottom