Zitto Zuberi Kabwe: Yeyote atakayemsaidia Seth katika sakata la IPTL ataanguka naye

Tajiri wa kinyankole

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,977
Reaction score
4,912
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo na mtaalamu wa uchumi, Zitto Kabwe, ametoa onyo kali kwa watu wote- ndani na nje ya Serikali wanaojihusisha au kupanga kumsaidia mfanyabiashara Harbinder Seth katika madai yanayohusiana na fedha za umma zilizotokana na sakata la IPTL na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumapili Mei 18, 2025 mkoani Dar es Salaam, Zitto amesema, “Yeyote serikalini, yeyote yule au nje ya serikali, ambaye kwa namna yoyote ile anasaidia au yuko kwenye mpango wa kuchota fedha za umma ili kumpatia bwana huyu Seth, ataanguka na bwana huyu.

Katika historia ya IPTL tangu wameanza, hajawahi kupona mtu, mtu yeyote ambaye amejihusisha na IPTL tangu mwaka 1995 awe ni Waziri, awe ni Katibu Mkuu, awe ni nani, hajawahi kupona, kwahiyo watu wajiepushe na hili jambo”.

Zitto amefafanua kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia Kesi Namba 90 ya Mwaka 2018, kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati dhidi ya Harbinder Seth, ilifikia Makubaliano ya Maelewano (Consent Decree).

Kupitia kesi hiyo, Bwana Sethi alikubali kusaini Hati ya Fidia (Deed of Indemnity), akiahidi kuilipa Serikali fidia ya hasara iliyoletwa na maamuzi ya mahakama za kimataifa dhidi ya Tanzania na TANESCO – maamuzi ambayo yanaifanya Tanzania kudaiwa mabilioni.

Katika makubaliano hayo, Mahakama ilieleza wazi kuwa Sethi hana na hatakuwa na madai yoyote dhidi ya Serikali na anapaswa, pamoja na PAP, kulipa fidia hiyo. Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa hadi leo, utekelezaji wa maamuzi hayo halali bado haujafanyika.

“Kuitwa mwizi si tusi, bali ni sifa anayostahili. Huyu ni mtu ambaye tayari ana hukumu ya jinai kichwani kwake, lakini amepewa uhuru wa kudhihaki Watanzania na kodi zao,” alisema Zitto kwa ukali.

Aidha, Zitto amefichua kuwa Sethi alikubali makosa ya jinai ya uchotwaji na utakatishaji fedha kupitia makubaliano ya Plea Bargain na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ambapo aliahidi kulipa zaidi ya shilingi bilioni 26 kwa Serikali. Hadi sasa, amerejesha milioni 200 pekee, huku zaidi ya miaka minne ikiwa imepita tangu apate uhuru wake kwa masharti.

Zitto pia alieleza kuwa kampuni ya Eurasia Holdings, ambayo ilikuwa mbia katika IPTL, imefungua kesi ya kutaka kampuni hiyo ifutwe rasmi (winding up petition), jambo linalozua maswali makubwa kuhusu hatma ya fedha za umma zinazodaiwa kufidiwa na PAP na Seth.

Katika hatua nyingine, Zitto ameibua mgongano wa madai kati ya Seth na TANESCO. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ukurasa wa 35 na 36, Sethi anadai TANESCO shilingi bilioni 211. Hata hivyo, TANESCO inadai kuwa Seth ndiye anayedaiwa, kwa kuwa katika makubaliano na DPP alikubali kuilipa TANESCO dola za Marekani milioni 148, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 400.

“Kwa hiyo hata tukikubali madai yake, bado TANESCO inamdai zaidi ya anavyodai. Hivyo ni wazi kuwa yeye ndiye mdaiwa, na si TANESCO,” amesema Zitto.

Zitto amesisitiza kuwa madai hayo, pamoja na ushahidi uliopo kwenye nyaraka rasmi za Serikali, vinaweka bayana kuwa hakuna msingi wowote wa kisheria au kisiasa kwa yeyote kumsaidia Seth katika kujinufaisha kwa fedha za umma.

“Ninafurahi kuwa kesi hii inakwenda mahakamani. Huko ndiko tutakapoweka ukweli wote hadharani. Tutautaja mzoga huu mahakamani na kuhakikisha unafukiwa moja kwa moja,” amehitimisha Zitto, akimaanisha kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa dhidi yake na Seth.
 
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo na mtaalamu wa uchumi, Zitto Kabwe, ametoa onyo kali kwa watu wote- ndani na nje ya Serikali wanaojihusisha au kupanga kumsaidia mfanyabiashara Harbinder Seth katika madai yanayohusiana na fedha za umma zilizotokana na sakata la IPTL na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumapili Mei 18, 2025 mkoani Dar es Salaam, Zitto amesema, “Yeyote serikalini, yeyote yule au nje ya serikali, ambaye kwa namna yoyote ile anasaidia au yuko kwenye mpango wa kuchota fedha za umma ili kumpatia bwana huyu Seth, ataanguka na bwana huyu. Katika historia ya IPTL tangu wameanza, hajawahi kupona mtu, mtu yeyote ambaye amejihusisha na IPTL tangu mwaka 1995 awe ni Waziri, awe ni Katibu Mkuu, awe ni nani, hajawahi kupona, kwahiyo watu wajiepushe na hili jambo”.

Zitto amefafanua kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia Kesi Namba 90 ya Mwaka 2018, kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati dhidi ya Harbinder Seth, ilifikia Makubaliano ya Maelewano (Consent Decree). Kupitia kesi hiyo, Bwana Sethi alikubali kusaini Hati ya Fidia (Deed of Indemnity), akiahidi kuilipa Serikali fidia ya hasara iliyoletwa na maamuzi ya mahakama za kimataifa dhidi ya Tanzania na TANESCO – maamuzi ambayo yanaifanya Tanzania kudaiwa mabilioni.

Katika makubaliano hayo, Mahakama ilieleza wazi kuwa Sethi hana na hatakuwa na madai yoyote dhidi ya Serikali na anapaswa, pamoja na PAP, kulipa fidia hiyo. Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa hadi leo, utekelezaji wa maamuzi hayo halali bado haujafanyika.

“Kuitwa mwizi si tusi, bali ni sifa anayostahili. Huyu ni mtu ambaye tayari ana hukumu ya jinai kichwani kwake, lakini amepewa uhuru wa kudhihaki Watanzania na kodi zao,” alisema Zitto kwa ukali.

Aidha, Zitto amefichua kuwa Sethi alikubali makosa ya jinai ya uchotwaji na utakatishaji fedha kupitia makubaliano ya Plea Bargain na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ambapo aliahidi kulipa zaidi ya shilingi bilioni 26 kwa Serikali. Hadi sasa, amerejesha milioni 200 pekee, huku zaidi ya miaka minne ikiwa imepita tangu apate uhuru wake kwa masharti.

Zitto pia alieleza kuwa kampuni ya Eurasia Holdings, ambayo ilikuwa mbia katika IPTL, imefungua kesi ya kutaka kampuni hiyo ifutwe rasmi (winding up petition), jambo linalozua maswali makubwa kuhusu hatma ya fedha za umma zinazodaiwa kufidiwa na PAP na Seth.

Katika hatua nyingine, Zitto ameibua mgongano wa madai kati ya Seth na TANESCO. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ukurasa wa 35 na 36, Sethi anadai TANESCO shilingi bilioni 211. Hata hivyo, TANESCO inadai kuwa Seth ndiye anayedaiwa, kwa kuwa katika makubaliano na DPP alikubali kuilipa TANESCO dola za Marekani milioni 148, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 400.

“Kwa hiyo hata tukikubali madai yake, bado TANESCO inamdai zaidi ya anavyodai. Hivyo ni wazi kuwa yeye ndiye mdaiwa, na si TANESCO,” amesema Zitto.

Zitto amesisitiza kuwa madai hayo, pamoja na ushahidi uliopo kwenye nyaraka rasmi za Serikali, vinaweka bayana kuwa hakuna msingi wowote wa kisheria au kisiasa kwa yeyote kumsaidia Seth katika kujinufaisha kwa fedha za umma.

“Ninafurahi kuwa kesi hii inakwenda mahakamani. Huko ndiko tutakapoweka ukweli wote hadharani. Tutautaja mzoga huu mahakamani na kuhakikisha unafukiwa moja kwa moja,” amehitimisha Zitto, akimaanisha kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa dhidi yake na Seth.
Kwanini kipindi hiki? MTANIKUMBUKA
 
Tangu achomewe kibanda chake kule kigoma hana maajabu tena
 
Aache kutishia watu huyo,polisi wamwongezee kesi ya kutishia umma
 
Tapeli hilo halina maana, pesa sio bora kuliko maisha ya watu!!.
 
Zitto uwa anajikosha sana tapeli la kisiasa ila mwisho wake hauko mbali
 
Back
Top Bottom