McCollum
JF-Expert Member
- Jan 10, 2023
- 384
- 684
Habari kwa wanajukwaa. Ni matumaini yangu muwazima wa afya.
Awali ya yote kabla sijaenda kwenye mada nataka nielezee u-perfectionism kwa kifupi. Perfectionism ni hali ya kuwataka/kutarajia au kujitaka/kujitarajia wewe mwenyewe kufanya jambo/mambo bila ya kuwa na kosa/makosa yoyote.
Watu ambao wanapenda kufanya mambo bila makosa wanaitwa perfectionists. Mara nyingi watu hawa wako radhi kuanza upya kazi/shughuli yoyote ambayo waliifanya na hawakuyakubali matokeo yake. Kama utakutana na mtu wa namna hii kuwa tayari kuambiwa kama utakosea na ata-point kila details ambayo anaona umeikosea.
Sasa naomba niende kwenye mada. Kwa mara nyingi watu ambao ni perfectionists ni watu ambao wanakuwa na sonona, msongo wa mawazo na matatizo mengi kutokana na wanavyoyachukulia mambo. Mfano perfectionists huwa wanakerwa na rafiki au jamaa zao pale wanapoona hawafanyi kama wanavyotaraji na mengine mengi. Itakuwa ngumu kuorodhesha matatizo ya perfectionists yote ila naomba niende kwenye njia za kuzitumia kupambana na athari za u-extreme perfectionism
1. Kubali kuwa binadamu hajakamilika na hivyo hawezi kufanya mambo yasiyo na makosa (flawlessness)
2. Usi-judge watu kwa viwango vya juu ambavyo umeviweka wewe na unategemea wavivuke kwakuwa unataka wawe perfect.
3. Jifunze kukubali kwamba hakuna aliyekamili na hata wewe unayeutafuta ukamilifu kwa watu au kwako haujakamilika.
4. Stop judging and start sharing the necessary knowledge you think could in one way or another help others.
5. Usijikatae na kujitenga ukiwa mbele ya watu au jamii kwakujiona wewe ni mtu wa viwango vya juu kuwazidi wao (Utakosa mengi)
6. Jifunze communication skills na team work
7. Kubali kujifunza hata kwa watu ambao akili yako inakuambia hawana uwezo kukuzidi.
8. Usijipe ukubwa mbele za fani za watu kwakuwa unaamini katika uwezo wako ambao haujawahi kutumika kwenye hiyo field.
9. Jifunze namna ya kutoa mchango bila kuwashusha wenzio (akilini mwako au mbele yao).
Nawasilisha