Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Mambo ni mdogomdogo mkuu. Kama ramani imebadilishwa kuna siku ya tutapigwa marufuku

Jirani akimega kiwanja chako usipomchukulia hatua kali, atavunga jamii ikishazoea kwamba eneo alilomega ni lake ndipo anakuja kuweka uzio

Nakubaliana na wewe. Sisi cha kufanya ni kusema malawi wanapotosha umma na dunia kwa kuchapisha ramani zinazoonesha uongo.
 
Nadhani hakuna jipya hapo, shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida. Meli, uvuvi na ulinzi, nothing to fear, google map kubadili mipaka ni sawa watu wanasema zanzibar ni jamhuri huru wakati huko duniani passport na nyaraka ni tanzania 🇹🇿
 
Kwa ramani ambazo Malawi wanazitumia ziwa Nyasa linaonekana hivyo na wao wanaliita Lake Malawi. Lakini kwa ramani za mitaala ya Tanzania ziwa Nyasa limegawanyika kwa dotted lines. Ukiona dotted lines kwenye ramani maana yake hiyo border iko kwenye dispute.

Hata Malawi kipindi cha Muluzi kurudi nyuma walikuwa wanaweka dotted lines, lakini alipokuja yule Rais Mwanamama wa kwanza wa Malawi, Joyce Banda akaja na ajenda ya kuwa ziwa ni la Malawi pekee kadri ya Heligoland Treaty ya 1870.

Najua maongezi ya umiliki wa ziwa Nyasa yanaendele kati ya nchi zetu 2 chini ya uratibu wa Ex President wa Mozambique Joachim Chissano
 
Tuanzie kwenye mipaka ya Tanganyika kwa pale ilipo sasa tulirithishwa kwa kutumia mkataba wa mipaka iliyowekwa mwaka gani?

Na kwa nini tuliipokea hiyo huku tukijua himaya zetu za utawala wa mababu zinavuka mipaka hiyo ya wakoloni?

Na je wakati tunapewa uhuru tuliambiwa mipaka yetu ni ipi?

Kwa katizo la hoja hasa kwa dhana ya Zanzibar na Sultanate area.
Je zile zinazosemekana kilometer 16 (au 16 miles?) za nchi kavu kutokea bahari ya hindi si za Tanganyika?

Ila Somewhere kwa kuwa England ilitawala Uganda, Kenya, Tanganyika, Malawi, Zambia na Zimbwe; walikuwa hawajali sana mipaka ya maeneo kwa kadri walivyokabidhiwa na watangulizi wao hasa kwa maeneo ya majini. Hiyo ilichangia kuvuruga mipaka iliyowekwa na wajerumani.
Again Somewhere else, ilikubaliwa kwamba kwa nchi zinazopakana kwa water bodies basi pale kati kati ya eneo la maji pawe ndio mpaka.

Na huo ndio msimamo wa Tanzania.
```````````````````````````````````````````````````
Tanzania haiwezi kuwa mlinzi wa vyanzo vya maji halafu isitumie maji hayo!

Swali je kulingana na miamba ya chini kuendelea kuserereka na hivyo kusababisha matetemeko ya ardhi, volcano, na utitio wa Ardhi. Je ikiwa itatokea Ardhi ya let say mkoa wa Njombe hasa kule Ludewa ikatitia na maji yakajaa eneo lote la mkoa wa Njombe na Mbeya (sorry for Ngoni, Wakinga and Wanyanyakusa, I assure you haitatokea), je ikitokea sasa, endapo wa juu sana kaamua tutatuimia hii kanuni ya kuwa katikati ya eneo la maji ndio uwe mpaka?
Maana tectonic plates zinaendelea zake chini kwa chini kwenye Rift Valley of East Africa!
 
Hii habari inaleta taharuki.
Nitaenda mwenyewe hadi Kyela-Matema Beach nitafikia hoteli ya Jenerali Mwamunyange nione kama haturuhusiwi kugusa hayo maji.
Hotel ya Mwamunyange ipo Ngonga kwenye makutano ya mto Kiwira na ziwa, kwa pembeni kidogo kuna makutano ya mto Songwe na ziwa ambao ni mpaka wa nchi hizi mbili,hakuna hata fujo za majini.
Ajabu ni kuwa, watu wa Nkatabay na Mbambabay, Kyela na Karonga huu mgogoro ni kama hauwahusu kwa uhusiano walio nao. Wanaishi kindugu kabisa.
 
Wanasiasa ndio wachoganishi. Wananchi hata hawajui chochote.
 
Halafu ukiwa hapo hotelini kwa Mwamunyange, tunatumiwa sms kwenye simu zinasema Welcome to Malawi.
 
Mkuu fuatilia huo mgogoro utaona kuna mazingira tunatengenezewa ya kuporwa hilo eneo.
Mbona ile rasi ya Crimea uwekezaji unaendelea kama kawaida japo liliporwa kibabe mwaka 2014?
Ishu hapo ni mafuta na gesi kifupi Mzungu hapo amefanikiwa kuingiza mgogoro (boko haramu) hivo lazima adili na jeshi moja tofauti akidili na majeshi mawili na la tz kwakua litakua na haki ya kuingilia kupambania mpaka wetu ziwani
otherwise....
Atafanya amefanya makubaliano na wakuu wa vipenyo ili diplomatically wakubali matokeo ili wapate mgao
 
Hili ni Swala na Waziri wa mambo ya ndani na Nje kulishughulikia kwa Haraka
 
Chanzo cha hii ramani ni kipi, maana kwa ufahamu wangu kuna kamati iliundwa na Umoja wa Afrika bado inaendelea kushughulikia hili suala baada ya Malawi kupeleka malalamiko kuwa hili ziwa ni mali yao, juu ya jina la ziwa kuwa ziwa Malawi, watu wa malawi wamekuwa wakiliita hili ziwa kwa jina hilo kwa miaka mingi tu. Lakini ikumbukwe pia hili ziwa halimilikiwi na Malawi na Tanzania pekee yao, Msumbiji pia wamo so mipaka haiwezi badilika kirahisi kiasi hicho!
 
Na hili ni tatizo la Kuwa na serikali masikini, kwani kwa miaka 60 sasa hatujachukua hata hatu kuwekeza kwenye hayo maziwa, hata kuweka Boti za wanajeshi Kufanya doria kuweka maboya Kuchora ramani ya nchi yetu na kuiweka Kwenye satellite, hivyo vitu vinahitaji pesa, na serikali haina pesa, Umasikini ni laana sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…