Zlatan Ibrahimovic atua Serengeti, apost akijivinjari

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Nyota wa zamani wa klabu maarufu za Ajax, PSG, AC Milan, Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, ambaye kwa sasa ni mshauri wa uongozi wa mabingwa mara saba wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, AC Milan, yupo nchini Tanzania.

1749705569966.png
Zlatan, aliyewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Sweden, amechapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa eneo la Kogatende, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tanzania. Eneo hili linajulikana kama kitovu cha uhamaji wa wanyama, ambapo maelfu ya nyumbu huvuka Mto Mara kwa tukio la kipekee duniani, maarufu kama 'Great Migration.'

Kwa mujibu wa wataalam wa uhifadhi na utalii, mwezi huu wa Juni ni wakati ambapo wanyama wengi hasa nyumbu hujaa Kogatende, tayari kuanza kuhamia kuelekea maeneo mengine kwa ajili ya uhamaji wa kila mwaka. Hii ni fursa adimu kwa watalii na wageni kujionea tukio la kipekee la asili duniani.

Hii ni nafasi adimu kwa watalii kujionea moja ya miongoni mwa mandhari ya kipekee duniani, na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii wa utendaji wa asili na burudani.

Nyota wa zamani wa klabu maarufu za Ajax, PSG, AC Milan, Inter Milan,,Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, ambaye kwa sasa ni mshauri wa uongozi wa mabingwa mara saba wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, AC Milan, yupo nchini Tanzania.

Back
Top Bottom