Zoezi la Kupitisha Rasimu ya Kanuni za Bunge linaendelea vizuri

Zoezi la Kupitisha Rasimu ya Kanuni za Bunge linaendelea vizuri

Chabruma

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
5,660
Reaction score
1,780
Wadau, kama mjuavyo ni kuwa, kuanzia chana jioni, bunge maalum limeanza zoezi la kupitisha kanuni za bunge hilo. Hii ni baada ya Rasimu ya Pili ya Kanuni hizo kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Kanuni, Prof MAHALU. Busara zilizotumika za wazee kuzungumza kutuliza jaziba miongoni mwa wabunge zimesaidia sana mchakato kuufanya uwe wa kistaarabu tofauti na ilivyokuwa inatafsiriwa hapo awali.

Kwa siku ya jana kuanzia saa 1 usiku hadi saa 3 usiku, jumla ya vifungu 3 kati ya 87 vya Rasimu ya Kanuni hiyo zimepitishwa baada ya kufanyika marekebisho. Kwa siku ya leo kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 8 mchana, Bunge hilo maalum limepitisha kuanzia vifungu vya 4 hadi 10 na zoezi litaendelea kuanzia saa 11 jioni. Hata vile vifungu vilivyoonekana kuwa vinaweza kuwa na msuguano, msuguano huo haukuhatarisha mjadala wa bunge na wote walishirikiana kutafuta ufumbuzi wa pamoja.

Nawapongeza sana wabunge wa bnge letu na hakika wanatuwakilisha vema wananchi. Ni vema wakaendelea kufanya kazi kwa maslahi ya taifa bila ya kushurutishwa na baadhi ya watu ambao imeelezwa kuwa wana malengo ya kuvuruga mchakato huu

Updates 2
zoezi la kupitisha Rasimu ya Kanuni zinaanza kwa Mwenyekiti kutoa maelezo katika mambo mawili
1. Mahudhurio, anawataka wajumbe kuhudhuria kwa wingi kwa vile hoja zinazopitishwa ni nzito na hivyo ni vema wajumbe wakahudhuria kwa wingi

2. Anawataka wajumbe kutumia ipasavyo muda. Katika hili, anawataka wajumbe wenye marekebisho kutumia muda mchache kueleza hoja zao. Na kwa wale hoja zao zimejibiwa, ni vema wakaziondoa

baada ya hayo, Upitishwaji wa Rasimu hiyo unaendelea na ibara iliyopo ni ya 10 kuhusu viapo kwa wajumbe. Katika hili kanuni zinasema kuwa wajumbe wataapa kwa pamoja. Kuna wajumbe wanaonesha wasiwasi katika hili hasa ikizingatiwa utofauti wa imani. Pia kuna wajumbe wanaohoji iwapo kutakuwa na vitabu vya kutosha vya imani za dini. Katika kutatua suala hilo, kuna wanaopendekeza kuapa kutokana na makundi ya dini zao. Yaani kama waislam waape kivyao na wakristo waape kivyao

UPDATES 3
Bunge maalum la Katiba limemaliza semina ya siku ya leo ambapo kwa kikao cha jioni ambacho kimeanza saa 11 jioni hadi saa mbili usiku kimepitisha vifungu kuanzia cha 11 hadi cha 31. Hii ni kusema kuwa jumla ya vifungu 20 vimepitishwa kwa kikao cha jioni hii pekee. Kwa mwendo huu inabashiriwa kuwa wabunge sasa wameanza kuelewa wajibu wao na wana dhamira ya dhati kuhakikisha kuwa Tanzania inapata katiba mpya. Hali ya utulivu imeendelea kushamiri na ile mivutano na mashambulizi baina ya watu yamepungua. Pia zile kejeli za kisiasa zimepungua japo zimekuwa zikijitokeza mara chache.

Kwa siku ya Kesho, Kikao kitaanza saa 10 jioni kutokana na Kamati Maalum ya Prof MAHALU kuomba muda zaidi wa kuvipitia vifungu vya 32, 33, 34, 35 na 36 ambavyo vimeonekana kuwa vina dosari ambazo ni muhimu zikarekebishwa. Mwenyekiti ameridhia ombi hilo la kamati kutokana na uzito wa kazi hiyo. Aidha, kwa siku ya kesho, inatarajiwa kuwa majadiliano yatakuwa makali hasa ikizingatiwa kuwa vile vifungu vya 37 na 38 juu ya KURA YA SIRI NA WAZI vitajadiliwa. Hata hivyo, busara iliyotolewa na Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA kuwa vile vifungu vyenye ukakasi vitafutiwe ufumbuzi kwa njia ya maridhiano nadhani itaweza kupunguza jazba kutoka kwa wajumbe. Wananchi wote wa Tanzania tuendelee kuliombea Bunge letu ili liweze kutimiza wajibu wake ipasavyo

UPDATES 4
Semina iliendelea kama ilivyopangwa leo tarehe 5.3.2014 kuanzia saa 10 jioni. Mwenyekiti alitoa taarifa kuwa lile zoezi la kupitia vifungu vya 32 hadi 37 ambalo Kamati Teule ilipewa lilikuwa limekamilika. Hata hivyo, mwenyekiti alisema kuwa kuna jambo dogo lilikuwa linaendelea na lingekamilika ndani ya dakika 15 zijazo. Zoezi hilo ni la kudurufu nakala za marekebisho ya vifungu hivyo kulingana na idadi ya wajumbe. Kutokana na hali hiyo, mwenyekiti aliwahoji wajumbe kama wasubiri hadi karatasi hizo zipatikane ndipo semina iendelee au waendelee kupitisha vifungu vya mbele. Baada ya majadiliano ya muda mfupi, wajumbe walikubaliana kuwa waendelee kujadili vifungu vinavyofuata. Kutokana na maamuzi hayo, vifungu kuanzia vya 44 hadi 53 vilipitishwa.

Baada ya vifungu hivyo kupitishwa, zile karatasi za nakala ya vifungu vilivyofanyiwa marekebisho zilikuwa zimesambazwa na ndipo Mwenyekiti wa Kamati Teule alipomkaribisha mjumbe wa Kamati kusoma vipengele vyote kama ilivyorekebishwa. Baada ya vifungu hivyo kusomwa ambapo pia ilihusu vifungu vya 39,40,41,42 na 43, mjadala uliibuka. Wapo waliotaka vifungu hivyo vipitishwe baada ya kuwasilishwa wakati wengine wakitaka wajumbe wapitie kwa nyakati zao na wale wenye marekebisho kutokana na marekebisho hayo ya Kamati wawasilishe kesho. Hoja ya kutopitishwa vifungu hivyo iliungwa mkono na wajumbe wengi na ndipo ilipoamuliwa kuwa vifungu hivyo vijadiliwe kesho tarehe 6.3.2014. Kwa vile muda ulikuwa bado haujaisha, vifungu vya 54,55 na 56 vilijadiliwa na kupitishwa. Kifungu cha 57 kilikwama kupita kutokana na kuibuka mjadala juu ya ushiriki wa watu ambao si wana kamati za Bunge Maalum kushiriki kwenye vikao vya kamati. Kuna baadhi ya wabunge waliopendekeza kuwa watu wengine hususan waandishi wa habari waruhusiwewakati msimamo wa kamati teule ni kuwa waandishi wa habari wapewe taarifa zilizokamilika kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati husika. Mjadala ulioibuka ulianza kubeba taswira ya ushabiki wa kisiasa na ndipo ilipoamuliwa kuwa Kamati ipitie upya kifungu hicho ili kutafuta muafaka wa pamoja na maamuzi yatatolewa kesho
 
Pamoja sana mkuu kazi yetu ni moja tu kutunga katiba iliyobora kabisa ambayo watanzania wanaitaka kwa sana.
 
Hongera sana wabunge wetu kwa kuweka maslahi ya taifa mbele
 
Pamoja sana mkuu kazi yetu ni moja tu kutunga katiba iliyobora kabisa ambayo watanzania wanaitaka kwa sana.

Hii iliyopo iliwasaidiaje ama ilishindwa kuwasaidia? Na katiba mpya itawasaidiaje wananchi?
 
Hii iliyopo iliwasaidiaje ama ilishindwa kuwasaidia? Na katiba mpya itawasaidiaje wananchi?
Kama hata majibu ya hii post yako huna basi hufai kuwa mtanzania kabisa.
 
Hii iliyopo iliwasaidiaje ama ilishindwa kuwasaidia? Na katiba mpya itawasaidiaje wananchi?
Mkuu, swali hilo sijui kama lina maana kwetu. Kama huna cha kuchangia ni bora ukalala tu
 
Mkuu, swali hilo sijui kama lina maana kwetu. Kama huna cha kuchangia ni bora ukalala tu
Ni kweli mkuu huyu mdau amekaa kitoto kabisa analeta mambo ya kibavicha humu wakati watu wako na dhamira ya dhati kupata katiba mpya.
 
Ni kweli mkuu huyu mdau amekaa kitoto kabisa analeta mambo ya kibavicha humu wakati watu wako na dhamira ya dhati kupata katiba mpya.

Watu gani wenye dhamira? Hao wahuni(reffer mtikila) walioko hapi dodoma wanaoongea maneno ya kanga na kutaka uenyekiti kwa vigezo vya jinsia ndo watatuletea katiba? Haupo serious wewe na genge lenu hapo lumumba.
 
Ni kweli mkuu huyu mdau amekaa kitoto kabisa analeta mambo ya kibavicha humu wakati watu wako na dhamira ya dhati kupata katiba mpya.

Watoto nyie mnaokesha JF. Hadi mnatia kinyaa! Siwezi nikajadili vitu vya maana na wewe au lizbon, betlem, hammy d, chris Lucos nk. Post zenu huwa ni hovyo mwanzo mwisho! Kwa fupi mnakera.
 
Watoto nyie mnaokesha JF. Hadi mnatia kinyaa! Siwezi nikajadili vitu vya maana na wewe au lizbon, betlem, hammy d, chris Lucos nk. Post zenu huwa ni hovyo mwanzo mwisho! Kwa fupi mnakera.
Watu wanaokufanya uishi na ule leo unawaona watoto siku wakinuna sijui utakula nini.
 
Back
Top Bottom