Zoezi la kuwaondoa Wamachinga kwenye njia za Watembea kwa miguu Dar es Salaam, sijaona dalili yoyote ya wao kuondoka

Kuwaondoa hawawawezi Ng'o labda kama wako tayari kumwaga damu! Wachutame tu na aibu zao kwa kushindwa kumshauri yule kichaa wao Mwendazake!
 
Kile kibaraza chako siku ukitaka kupaka rangi ulipie kodi asee..!
 
Nipo Kariakoo hapa Gerezani mi mwenyewe nilisahau ndo umenikumbusha hapa baada ya kuona uzi wako.
 
Mna ajira za kuwapa?

Rais Samia amesema wamachinga wapangwe vizuri ili wafanye biashara kwa mujibu wa sheria na taratibu!
 
hahahah hapa mbezi mwisho ndio wajaa sana leo... naelekea kimara ntakujuza.... Makalla akifanikiwa kuwaondoa wamachinga apewe tunzo kabisa
 
Wanepewa maeneo mapya ya kazi!??
 
Naona serikali inarudia mchezo wa kufukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani kama enzi za mzee Ruksa!
 
Yaani miji imekuwa michafu utadhani majalala, yaani watu wanapikia mpaka barabarani na kutupa taka hovyo tu, fukuza wote miji iwe misafi na ya kuvutia, sio kila kona kuvuta harufu ya mbaya ya takataka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…