Zoezi la sensa 2022 lafikia asilimia 54 ikiwa leo ni siku ya 4

Zoezi la sensa 2022 lafikia asilimia 54 ikiwa leo ni siku ya 4

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Zoezi la kuhesabu watu katika sensa ya watu na makazi limefikia 54% hadi leo Agosti 26, 2022.

 
Mimi sijahesabiwa pamoja na familia yangu kwa ujumla na hadi sasa hamna uwezekano wa kuhesabiwa.

Akina Ngoswe mkitundika Vishikwambi mjue kuna watu 3 hawajahesabiwa
 
Tanzania vitu vyenye uhalisia kwa uwepo ni jua, mbalamwezi na mvua tu vingine hata siviamini.
 
Tuwasubiri na kuwapa ushirikiano makarani. hili la kupigapiga picha za hovyo na makarani si sawa kwa kweli
 
Zoezi hili lingetumia Walimu wa shule za Msingi na Serikali pamoja na Wajumbe wa nyumba kumi kama ilivyo desturi hali ingekuwa bora zaid
 
tupo hapa ila nina uhakika mpaka zoezi linafungwa kuna watu watakuwa hawajahesabiwa,especially huku mjini
nami kuhakikisha hilo sitatoka hapa nyumbani mpaka zoezi linaisha ili nione

Sent from my CAM-AL00 using JamiiForums mobile app
 
Zoezi limejaa mswali mengi ya kipuuzi tena yanajirudia rudia..

Wangejikita kwenye kuuliza points sidhani kama wangechukuwa muda kumaliza zoezi Kwa muda mfupi.

Karani wa sensa
-- unajuwa kusoma na kuandika Kiswahili na kingereza?
-- unajuwa kuhesabu namba na kuzidisha na kugawanya?
--Hivi kuanzia asubuhi hadi jioni unashinda sehemu gani?
--unafanya kazi gn?
--Hapa ni kwako au umepanga!?
--hivi hii nyumba ina Choo?
--ni flash au cha shimo?
--hivi Una simu janja?
--kiswaswadu je?
-- Una laptop?
--mara ya mwisho kutumia laptop lini?
--hivi ulihamia hapa dar au ulizaliwa?
--kwann ulikuja hapa dar?
--hivi Una fridge?
--,pasi je?
--ni ya mkaa au umeme?
--una TV?
-- Una gari?
-- Una eneo lingine?
-- unalima?
--,mara ya mwisho kulima ni lini?

Yaani maswali ya kipuuzi ni mengi kuliko point..
Tusiwalaumu makarani wa sensa,

Tuwalaumu walioandaa mfumo mzima wa maswali ya sensa.

Naona aibu kujiita mtanzania.
 
Anna Makinda. Speaker, Mwenyekiti sijui PSSSF. Bado Commissioner wa Sensa , bibi kabisaaaa. Sisi Vijana eti Taifa la kesho. Huu ni wizi.
FB_IMG_1661544390221.jpg
 
Zoezi hili lingetumia Walimu wa shule za Msingi na Serikali pamoja na Wajumbe wa nyumba kumi kama ilivyo
Acha wote tule hii national cake. Walimu kila kitu wao tu khaa mridhike lakini nanyi wajumbe posho za kesi za wanakaya haziwatoshi mnataka na sensa pia😂
 
Back
Top Bottom