Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Utaratibu wa majina haujafuata mpangilio wa majina ya watu (alfabeti) na kuchanganywa hali ambayo inasababisha usumbufu kwa wapigaji kura
Mfano Katika kituo cha kupigia kura cha National Housing Kata ya Nyakato Mwananchi aliyehitaji jina lake lisijulikane ameeleza hali hiyo amekutana nayo ambapo eneo hilo linavituo vitatu ambapo katika upangiliaji wa majina ni tofauti na ule wa awali katika zoezi la kujiandikisha kwani walijua ukijiandisha ndio hiyo sehemu utapigia kura lakini leo ni tofauti
Amesema hali hiyo imefanya kuwa na usumbufu wa kutafuta majina kwenye vituo vyote vitatu ukizingatia na hali ya mvua ilivyo .
Changamoto kama hizo zimejitokeza pia katika Mtaa wa Nyahingi Kata ya Mkolani Wilayani Nyamagana wananachi wanaeleza mbali na wasimamizi kuwasaidia kutafuta majina yao lakini imekuwa na usumbufu wa kutafuta majina yao katika vituo mbalimbali.
Wananachi pia wameeleza Changamoto nyingine ni Karatasi zilizobandikwa na kuonyesha majina ya watu yamelowa na kupekelekea kuonekana kwa majina ya mwisho tu ya wapiga kura wanaeleza labda ni kutokana na material ya karatasi hizo (Carbon Paper).
wameeleza changamoto hiyo imewafanya kusubiria kwa muda mrefu kukamilisha zoezi hilo ambalo walijua ya kwamba watakamilisha mapema na kwenda kwenye shughuli zao za kila siku.
Aidha, katika vituo vya kupigia kura cya Bwiru changamoto kama hizo wamekutana nazo japo baadhi ya wananachi wamehoji uwepo wa vyumba vya kupigia vipo zaidi ya nne kuna haja gani juu ama kuna mbinu inayotengenezwa