Zoezi la uvaaji barakoa kwenye vyombo vya usafiri linazingatiwa huko ulipo?

Zoezi la uvaaji barakoa kwenye vyombo vya usafiri linazingatiwa huko ulipo?

Mama tangu amkamate mbowe, na kupiga marufuku Uhuru wa kukutana kwa watu mambo yamekuwa shaghalabagala.
 
Wakuu kufuatia tangazo la Serikali kwamba marufuku mtu kupanda kwenye chombo cha usafiri bila barakoa, vipi linazingatiwa huko ulipo?

Mimi huku daladala za Gongo la Mboto hamna kitu, maisha ni kama zamani tu.
mm mkoa nilipo kama huvai hata gari hupandi. ni lazima si ombi
 
Kwenye Panton Kigamboni ni kama hakuna hilo Tangazo na hiyo ni sehemu ambayo watu zaidi ya 400 hukusanyika mahala pamoja kwa zaidibya dakika 20-30 (muda wa kwenye Passengers Lounge+ muda wa kuvuka mkiwa kwenye Chombo)

TAMESA ninyi ndio wasimamizi wa hivi vyombo, toeni utaratibu wa kufuata Tangazo la Serikali.
 
Wakuu kufuatia tangazo la Serikali kwamba marufuku mtu kupanda kwenye chombo cha usafiri bila barakoa, vipi linazingatiwa huko ulipo?

Mimi huku daladala za Gongo la Mboto hamna kitu, maisha ni kama zamani tu.
Hao wanatoa hayo matamko wanatimiza wajibu tu na waingize siku na posho.!
 
Yaani ni janga. Kwenye vyombo vya usafiri hakuna anayejali kuvaa barakoa

Kinachotokea ni kwamba kila mmoja anayo mfukoni lakini sijui ni kuona aibu au kutoona umuhimu, au kutokuwa na imani kama kweli unaweza ambukizwa... hapa inachanganya kwa kweli;

Juzi tu nilipanda mwendokasi, barakoa yangu mfukoni, nimetokea mbezi... kufika ubungo basi limejaa kichizi akaingia mtu mmoja anakohoa sana sana... watu tukaaanza kuangaliana kama vile tunaulizana ; "kuna usalama hapa".... yule mtu alivyozidi kukohoa sana pamoja na kwamba alikuwa anajizuia kwa mikono lakini mmmmm ..... kila mtu aliogopa.... nikaona isiwe tabu nikatoa barakoa yangu nikavaaa.... kile kitendo cha kutoa barakoa na kuvaa nikashangaa basi zima kila mtu anatafuta barakoa yake! wengine kwenye mapochi wengine mfukoni .... ndani ya dakika moja basi karibu lote watu walivaa barakoa.... nilicheka kwa sauti ... maana dah.... basi zima tulicheka! kimya kikapita....

Sasa bado najiuliza tuna nini watanzania??!!!!
Ni uoga tu ndugu, hofu ni mbaya sana!! Alafu kibaya zaidi viongozi ndo wanaogopesha wananchi bila sababu ya msingi, wakati huo wao kila siku wanaanza watu kwenye mikutano yao!! Mambo ya ajabu sana
 
Hakuna anayevaa kana kwamba watu hawajasikia tangazo.
Uzuri wa corona inaua mafisadi tu huku makapuku wapanda daladala wakibaki salama
 
Mkuu Mungu atusaidie! Kwa magari ya Mwendokasi hapa Dar,wasafiri hatujali kabisa!
 
watu wanavaa barakoa lkn jambo la kushangaza hawavai kwa usahihi.
kama barakoa tu tunashindwa kuvaa kwa usahihi vipi kuhusu kondomu?!!
je hili linasababishwa na ukosefu wa maarifa au ni kupuuza?
Korona inaua tujikinge.
 
Hkn Niko mwendokaz apa hkuna kitu Kama hcho na hapa naelekea ofis ya umma labda ndio wanizuie
 
Unaataka wajali nini? Nyie watu mbona wapumbavu Sana na hiyo corona yenu?
Kwa hiyo usipopaga corona hutakufa?
Acha tuitwe tu wapumbavu na ninyi mbaki na werevu wenu! Lakini tunapaswa kufuata Miongozo na taratibu nyingine za afya ili kujikinga na Korona! Wewe ambaye huogopi kufa mbona ukiugua magonjwa mengine unaenda hospitali?
 
Wakuu kufuatia tangazo la Serikali kwamba marufuku mtu kupanda kwenye chombo cha usafiri bila barakoa, vipi linazingatiwa huko ulipo?

Mimi huku daladala za Gongo la Mboto hamna kitu, maisha ni kama zamani tu.
Leo nilipanda basi mimi tu ndio nilivaa barakoa
 
Kwani ni corona tu inaua??? Msitishe watu bhana, mbona watu wanakufa kila siku na ajali, na magonjwa mengine, mbona mnaikuza sana corona??? Mm na familia yangu nilishaawambia hamna cha barakoa wala chanjo hapa!! YESU muumba mbingu na nchi aliyetuvusha 2020 ataendelea kutulinda hata leo
Tusije kuwa tunadanganyana humu - wengine wameshachanjwa
 
Back
Top Bottom