Zongo ni aina ya uchawi unaokaa machoni

Zongo ni aina ya uchawi unaokaa machoni

Siku zote uchawi hauwaminiki uwepo wake au nguvu yake ispokuwa kwa wale waliodhurika nao.

Mwenye nao akikuangalia tu utaumwa tumbo hadi kufa, au akikiangalia chakula hata kipikweje hakiivi na kikiiva kinakuwa hakina ladha kabisa na watakaokila lazima matumbo yawaume sana halafu waharishe sana.

Zongo inaweza kupigwa kwa mtoto mchanga, mama mjamzito, n.k Zongo huwa ni Husda ya mchawi kwa kile unachokifanya au unacho jifagharisha nacho. Zongo inaweza kupigwa pia kwenye vyombo vya usafiri, kama umeshawahi kusikia gari hili limerogwa au kila wakati lina haribika na kutengenezwa, au kama umewahi kusikia boti hili linaharibika kila likipakia abiria au injini yake kufeli kila likipata mzigo wa kusafirisha.

Kujikomboa:
Dumu katika ibada, na pia Choma chumvi ya mawe nyumbani kwako na katika vyumba pia, huondoa sana nuksi katika nyumba, vyumba na sehemu ya bishara na katika vyombo vya usafiri.

da!!! noma sana~~~
 
Zongo (Al-A'yn/kijicho) ni aina ya Sihr/ uchawi ambao unadhuru mtu kutokana na kuhusudiwa. Kijicho kipo kweli kama alivyosema Mtume Muhammad (pbuh).

Husdah/Hasadi hizi hutokea pale mtu anapotamani kitu kutoka kwa mtu mwingine. Tunashauriwa pindi unapoona kitu kizuri kwa nduguyo au jirani yako basi kiombee dua kitu/ mtu huyo baraka kutoka kwa Mungu. Hii ndio kinga ya kutokumhusudu mtu/kitu.

Inawezekana umemuona jirani/nduguyo ana mtoto mzuri na ww nafsi yako kupitia macho yako ikatamani uwe nae ww, basi hapa mashetani husafiri kupitia uono wako huu kwenda kumdhuru huyo mtoto . Zongo huwa linaweza kumfanya mtoto akawa analia tu non-stop, kinachomliza hakijulikani, mtoto akagoma kunyonya titi la mama ake, homa ikapanda juu, tumbo kujaa gesi mithili ya kuvimbiwa, kutapika na kuharisha n.k .

Zongo ni kijicho ambacho kinaweza kiwa ni cha kudhamiria au kutokudhamiria. Tunashauriwa tusipende kukodolea sana macho vitu walivyoruzukiwa wenzetu na ikiwa itatokea tumetazama kwa matamanio kuwa nasi tuwe navyo hivyo vitu basi inatakiwa tuviombee baraka na kisha tumuombe Mungu atujaalie nasi tupate kama hivyo.
 
Kihistoria tunaambiwa uchawi huu ulikuwa ukitumiwa na wawindaji kupigia wanyama pori ambapo husababisha walegee ili iwe rahisi kwa muwindaji kuwapata.

Ila watu sasa wakauchukua utaalamu huo na kuja kuwadhuru wanaadamu wenzao
 
Jinsi ya kulitoa Zongo au kijicho.

Inatakiwa yule unayemuhisi kakupiga zongo au yule ambae ana fahamika kiwa ndie mfanyaji wa matukio hayo katika eneo hilo, apewe maji kisha anawe kwa kutia wudhu huku maji yake yakusanywe kisha akamwagiwe yule aliyedhurika na uchawi huu.

Lau kama hajulikani aliyesababisha uchawi huu basi yule aliyefanyiwa uchawi huu, anatakiwa apewe maji yaliyosomewa kisomo cha Ruqyah (Surat al fatha na muawidhatayn ( surat an-nas na falaq) kisha anywe baadhi ya maji hayo na mengine atilie wudhu mwilini mwake au ajipake tu mwili mzima.

Kwa uwezo wa ALLAH kijicho hicho kitatoka na mtu atarejea ktk hali yake ya uzima
 
Dah kweli kwa Yesu ni raha. Yaani nje huku kuna mahangaiko kweli kweli. Kuchoma chumvi tena?
Ndugu rudi kwa Mungu wako, Yesu ndio njia. Hautakuwa na haja ya kuchoma chumvi na mambo kama hayo.
Ukibarikiwa na Yesu hakuna wa kukulaani, awe shetani au vinyangara vyake.

Hakuna nuksi kwa mwana wa Mungu. Tafuta amani na Mungu wako na hutakuwa na haja ya kutahayari!
Acha ushamba ww ukiumwa unakula Dawa sasa nani anakuponesha yesu au Dawa Mjomba utakufa mapema wewe,mungu hakusaidii ikiwa huoneshi juhudi ya kutaka kusaidiwa
 
Acha ushamba ww ukiumwa unakula Dawa sasa nani anakuponesha yesu au Dawa Mjomba utakufa mapema wewe,mungu hakusaidii ikiwa huoneshi juhudi ya kutaka kusaidiwa
kweli!! mdo manake YESU alisema,"omba nawe utapewa,piga hodi nawe utafunguliwa,tafuta nawe utapata,"......mjomba umenikumbusha wale wasabato miaka ya tisini waliweka kambi air-port wakimsubiriri YESU alete ndege iliwa safiri wamfuate,,,walikaa hapo mpaka wakajaza vinyesi kwenye mapagala ya wa2...inzi wakazidi mitaani ikabdi serikali ikawafukuza!!
 
Back
Top Bottom