Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa mtuhumiwa wa ujambazi akiwa na silaha atazawadiwa Sh2 milioni.
Hayo yameelezwa leo Jumatano Juni 23, 2021 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema lengo ni kuendeleza operesheni hadi pale vitendo vya uhalifu vitakapokoma huku akihidi kuwa watakaotoa taarifa hizo hawatatajwa.
"Mwenye taarifa zinazohusu jambazi ziwe sahihi na ambazo zitafanikisha kumkamata akiwa na silaha donge hilo litatolewa palepale baada ya kufanikisha kumkamata kwa siri,” amesema.