Hivi hawa Polisi uwezo wao wa kufikiri umefikiri umeishia wapi
Je wanajua madhara ya hili wanalofanya?Je wameshasahau nini kilifanyika wakati wa mkuu wa upelelezi Zombe
Kufanya Watanzania tuanze kuchunguzana ni kitu kibaya sana..
Nakumbuka kuna wakati Polisi walipewa agizo la kuuwa mtu yoyote anaehusishwa na ujambazi
matokeo yake wafanya biashara wa dhahabu wasiokuwa na hatia yoyote waliuliwa kikatili na Polisi kwa kusingiziwa majambazi..
Polisi kuwaruhusu raia wachunguzane ni sawa na kuruhusu raia waanze kulipizana visasi,raia waanza kuwajaza Polisi habari za uongo,ni kufanya raia waanze kuogopana
Kwa umasikini tulionao milioni mbili ni pesa nyingi sana,raia wataanza kuwalisha Polisi habari za uongo ili wapate hizo pesa
Kule Marekani ni kosa kubwa kwa Polisi kitumia "informer" kwa kupata habari zake,ijapokuwa wako wanaotumia informers kisirisiri
Polisi wa Marekani hawaruhusiwi kutumia mainfoma kwa sababu kama nilizozitaja hapo juu
Polisi waache kutaka easy solutions,easy answers,waache kucheza na maisha ya Watanzania..