mshamba_hachekwi
JF-Expert Member
- Mar 3, 2023
- 20,704
- 66,337
Mimi ni shabiki wa Zuchu kwa kiasi fulani...
Kuna huu wimbo wake mpya unaitwa "antenna" nimeusikia sikia huko mitaani nikasema ngoja nitafute video niangalie.
Aisee, kwenye ile video ameweka picha za kutisha sana, kuna sehemu amejiweka kama jini/pepo anafanya vitu vya ajabu ajabu, video inaogofya, kuna vipande vinakera.
Sijawahi kuona video ya kitanzania yenye maudhui ya kishetani namna hii.
Labda ameona aige kwa wazungu kina doja cat, lil nas x, sam smith... wale wanafanya hivyo ili kuwashangaza mashabiki, mashabiki wapate cha kuwaongelea. Na pia kuna wengine wanamuabudu shetani kabisa.
Lakini kwa hapa bongo watu wengi wanachukulia dini serious, hii video wanaweza kuiona kama dhihaka halafu wakaja kumchukia.
Na inawezekana kabisa mashabiki wake wengi ni wakristo....