Zuchu amewaza nini kwenye video ya wimbo wake wa Antenna?

mshamba_hachekwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2023
Posts
20,704
Reaction score
66,337
Mimi ni shabiki wa Zuchu kwa kiasi fulani...

Kuna huu wimbo wake mpya unaitwa "antenna" nimeusikia sikia huko mitaani nikasema ngoja nitafute video niangalie.

Aisee, kwenye ile video ameweka picha za kutisha sana, kuna sehemu amejiweka kama jini/pepo anafanya vitu vya ajabu ajabu, video inaogofya, kuna vipande vinakera.

Sijawahi kuona video ya kitanzania yenye maudhui ya kishetani namna hii.



Labda ameona aige kwa wazungu kina doja cat, lil nas x, sam smith... wale wanafanya hivyo ili kuwashangaza mashabiki, mashabiki wapate cha kuwaongelea. Na pia kuna wengine wanamuabudu shetani kabisa.

Lakini kwa hapa bongo watu wengi wanachukulia dini serious, hii video wanaweza kuiona kama dhihaka halafu wakaja kumchukia.



Na inawezekana kabisa mashabiki wake wengi ni wakristo....

 
you guys are taking things seriously!! yan hiki nako ni cha kukijadili? si ni vile king'ang'a ameamua kuja kivingine kaka?? au wenzetu ndio mmefungua third eye mkaona huo ushetani? we nipe vimacho, tikisa vimacho, lazima irudiwe sababu nataka tena!!
 
Lazima atoe homage kwa anayempa umaarufu,kifupi umaarufu anaoupata huyu na wengine kibao ninaowafahamu ni wakishetani,wengine wakipata connection kwa waganga wengine kwa cult kama Freemason and such.Wewe utasema sanaa but ulimwengu wa kiroho imeisha hiyo.Nimalize kwa kusema achana na enzi za akina kanumba,bongo haijawahi kuwa na wasanii wauza nafsi Kama wakati huu.
 
Mfano issue ya misalaba anayovaa Diamond huwa inanifikirisha Sana halafu Ijumaa utamkuta na kanzu Safi na sendo. Umaskini unafanya watu waingie kwenye vitu vya ajabu😔
 
Hakuna alichowaza zaidi ya copy and paste kutoka Kwa Rihanna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…