Msanii wa Bongo Fleva, Zuchu, ameandika barua ya wazi kwa Diamond Platnumz akilalamikia unyanyasaji wa mara kwa mara kutoka kwa taasisi yake Wasafi FM, kupitia maudhui ya kipindi cha Mashamsham.
Zuchu amesema maudhui hayo yameathiri sanaa na afya yake ya akili, licha ya uwekezaji mkubwa wa kampuni hiyo katika kazi zake. Pia alidai familia ya Diamond inachangia kumharibia heshima.
"Kinachoendelea sasa mitandaoni kupitia maudhui ya kipindi chenu Mashamsham kimekuwa kama sehemu ya kuniumiza na kunididimiza kisanaa na kiafya ya mwili na akili. Lakini nasema nashukuru na nimeyapokea yote."
"Nimekuwa msanii wa taasisi mwenye kasi na mwenye kuipambania kazi yangu licha ya uwekezaji unaofanywa na kampuni yenu. Sikatai, ni jambo kubwa na la kheri kumkomboa binti mwenye kipaji kwa kumwekezea. Lakini nauliza, je, ni haki uwekezaji huo kutumika kama silaha pia? Au niliwakosea nini mpaka kufikia kunifanyia bullying na harassment hizi?"
"Nasibu (Diamond Platnumz), familia yako wana baya langu lipi ambalo wanaona ni haki wao hata wakiwa na mahojiano binafsi kutokuweka stara ya mambo yangu, huku wakihakikisha hawakuharibii wewe bali mimi."
"Nimefikia hatua leo naandika barua ya kisheria kwa walezi wangu kutokana na ukandamizaji wa mara kwa mara juu yangu. Inauma sana. Nitaenda mahakamani, na pengine sitaweza kushinda taasisi yenu yenye nguvu, lakini hata nikishindwa huko namwachia Mwenyezi Mungu, yeye ndiye hakimu wa mwisho."
"ASANTENI NASHUKURU kwa kuendelea kunibully na kuniharrass.
"Nimeomba sana kwako kama kiongozi, lakini mara nyingi maombi yangu hugonga mwamba na kunatengenezwa maudhui yenye kusudio la kunivunjia heshima, kuniumiza, na kuharibu afya yangu ya kiakili. Mimi ni binti na mwanamuziki, lakini sijawahi kuona media yoyote inaniharass kama ambavyo media ya taasisi yenu imekuwa ikifanya."
"Sina cha kuwafanya kikubwa. Nyinyi ni wenye nguvu, na mimi namshitakia Mwenye Ukuu na Utukufu zaidi yangu. Ninaamini zaidi kwa Mungu. ASANTENI SANA NASHUKURU."
Familia yao wanakaona kahuni tu na huyo bwana mpenzi wako angekupenda mngefunga ndoa , na familia ingemsisitiza akuoe
Wamekachoka maskini , na hv anakuspend atakavyo Dah umaskini mbaya
Msanii wa Bongo Fleva, Zuchu, ameandika barua ya wazi kwa Diamond Platnumz akilalamikia unyanyasaji wa mara kwa mara kutoka kwa taasisi yake Wasafi FM, kupitia maudhui ya kipindi cha Mashamsham. View attachment 3203758
Zuchu amesema maudhui hayo yameathiri sanaa na afya yake ya akili, licha ya uwekezaji mkubwa wa kampuni hiyo katika kazi zake. Pia alidai familia ya Diamond inachangia kumharibia heshima.
View attachment 3203767
"Kinachoendelea sasa mitandaoni kupitia maudhui ya kipindi chenu Mashamsham kimekuwa kama sehemu ya kuniumiza na kunididimiza kisanaa na kiafya ya mwili na akili. Lakini nasema nashukuru na nimeyapokea yote."
"Nimekuwa msanii wa taasisi mwenye kasi na mwenye kuipambania kazi yangu licha ya uwekezaji unaofanywa na kampuni yenu. Sikatai, ni jambo kubwa na la kheri kumkomboa binti mwenye kipaji kwa kumwekezea. Lakini nauliza, je, ni haki uwekezaji huo kutumika kama silaha pia? Au niliwakosea nini mpaka kufikia kunifanyia bullying na harassment hizi?" View attachment 3203769