mimi nadhani swala la kununua viewers ni kama online business,kuna watu hawawezi fanya biashara online wakiogopa kuibiwa na kuna wanaofanya kwakujua hata nikiibiwa nitaanzia hapa ntamalizia pale.
wasanii wengine nahisi wanajua viewers wananunuliwa lakini je wampe nani hiyo hela ili awanunulie hao viewers,je ikitokea viewers wakaondolewa watafanyaje? kuna maswali wasanii wengine wanajiuliza wanaishia kuona bora nusu hasara (kukosa viewers fake) kuliko hasara kamili (kulipia viewers halafu wasiongezeke hela ipoteee)
wcb nawafananisha na
Mwl.RCT huyu teacher yeye ananunua chochote online hata kiwe kona ya nchi gani,hajali wala haogopi kuhusu kupoteza hela,ananunua vitu vya mamilioni mtandaoni na ana amani,kwanini? kwasababu ana jua nini chakufanya ili asitapeliwe na nini cha kufanya hata akitapeliwa hela yake aipate,ndio mana haogopi.
wcb wamesha master game,wanajua nini wanataka nini chakufanya nini chakutofanya na zaidi "pesa wanayo" unakuta mambo yanawezekana kwao,kwahyo wasanii wengine sio kwamba hawajui huu mchezo "wanaujua vizuri tu" lakini hawana vitendea kazi,hawana connection,nk nk.
Mambo ni MENGI lakini mwisho ni kwamba yote hayo yanawezekana kama PESA IPO na wcb pesa ipo hawashndwi kitu ni wao kuamua tu.