Zuchu: Ninajenga msikiti Paje

Zuchu: Ninajenga msikiti Paje

Hii ni aina nyingine ya utakatishaji pesa..ila kwa huyu sasa amekwenda mbali zaidi anajaribu kumtumia Mungu/imani juu ya Mungu kutakatisha pesa
 
haha noma sana, ma-imam wako kimaslahi tu

Mwisho Mwampamba alijenga msikiti kwa fedha za 'bigi buraza' 😀
Mwisho alipata sh ngapi huko big braza? Acha uzushi hakulamba hata mia
 
Ajenge na shule na hospitali ndio msaada mkubwa kwa wakazi
 
mwehu uyu dada uwo msikiti wataenda kuswali yeye na mbosso..muislamu yeyote mwenye akili timamu awezi kukanyaga kwenye uwo msikiti yani mtu achume pesa zake kwa kukatika viuno leo hii aje ajenge msikiti na watu waswali? asthagafirulah
 
mwehu uyu dada uwo msikiti wataenda kuswali yeye na mbosso..muislamu yeyote mwenye akili timamu awezi kukanyaga kwenye uwo msikiti yani mtu achume pesa zake kwa kukatika viuno leo hii aje ajenge msikiti na watu waswali? asthagafirulah
Yaani, sijaelewa
Huo msikiti unaojengwa na "pesa za kukata mauno" unakua hauna milango au sakafu?

Wewe pesa zako za "harari" zime....... Nini?
 
Hongera sana dada kwa kufanya kitu ambacho moyo wako unakipenda na ni jambo jema kabisa. Watanzania ni wanafiki sana , wanamnanga utafikiri wao ni watenda mema sana. Sisi wakristu tunasema ''bwana kamawewe ungehesabu maovu yetu nani angesimama?''

Anajitahidi kutafita riziki kwa kipaji ambacho Mungu amemjalia na kaona atoe sadaka kwa kujenga nyumba ya kuabudu wewe unampangia cha kufanya?

Embu tuambie huo msikiti au kanisa unakosalia wewe unajua nani alijenga? wajua waliojenga pesa walipatia wapi? Majizi wengi, mafisadi, walarushwa, wafanya biashara haramu , watenda maovu mabalimbali wameacha nyumba zao wakfu kama sehemu ya vitubio vyao wewe sasa hivi unavitumia halafu unamnanga mtoto wa kike mdogo aliyekumbuka jambo jema. Tusubiriane siku ya mwisho ya hukumu BwanaYesu atakavyokuwa anawaumbua wanafiki
 
Hizo Pesa angejenga hata madarasa kadhaa kwenye shule ya msingi,
Znz shule zao zina hali mbaya jamani no wonder wanafeli kila siku, mazingira ya kusoma yanatia kinyaa Mtoto anakosa hamu ya shule,
Au angepeleka computer kadhaa kwenye hizo shule.
 
Yaani, sijaelewa
Huo msikiti unaojengwa na "pesa za kukata mauno" unakua hauna milango au sakafu?

Wewe pesa zako za "harari" zime....... Nini?
Uislamu unataratibu zake tumewekewa sheria mpaka za kutoa zaka, zaka ipi inakubaliwa na zaka ipi inakataliwa mziki kwa dini ya kiislamu na mfundisho yake ni haramu, mwanamke kuacha maungo,nywele zake wazi ni haramu kwenye uislamu nikuulize wewe zuchu kazi yake ni nini? mziki si ndio na mziki kwenye uislamu ni haramu kwaiyo hela yote anayoichuma kutokana na kazi anayoifanya ni haramu alafu iyo hela leo hii ajengee msikiti narudia tena ni wehu na machizi ndio wataenda kuswal kwenye msikiti wake.
 
niliwahi kusikia mawaidha ya sheikh kuhusiana na bongo fleva.

Alikua anausema vibaya sana.

Kwamba miziki ya kidunia inatoka kuzimu.
 
Back
Top Bottom